Sunday, June 6, 2010

JUMAPILI NJEMA KWA WOTE NA UJUMBE NI HUU UPITIOA KWA WIMBO HUU WA ZAKAYO!!!



Wimbo huu nadhani unaimbwa kwa kimasai nimeusikiliza mara nyingi na nikaona ni vema kulinukuu hili neno:-
Mtakatifu Luka 19: 1-10
”Naye alipoingia Yeriko alipita katikati yake. Na tazama, palikuwa na mtu, jina lake Zakayo, mkubwa mmoja katika watoza ushuru, naye ni tajiri. Huyu alikuwa akitafuta kumwona Yesu ni mtu wa namna gani, asiweze kwa sababu ya umati wa watu, maana ni mfupi wa kimo. Akatangulia mbio, akapanda juu ya mbuyu apate kumwona , kwa kuwa atakuja kuipitia njia ile. Na Yesu, alipofika mahali pale, alitazama juu akamwambia, Zakayo, shuka upesi, kwa kuwa leo imenipasa kushinda nyumbani mwako. Akafanya hharaka, akashuka, akamkaribisha kwa furaha. Hata watu walipoona, walinungĂșnika wote, wakisema, Ameingia kukaa kwa mtu mwenye dhambi. Zakayo akasimama, akamwambia Bwana, Tazama, Bwana nusu ya mali yangu nawapa maskini, na ikiwa nimenyang´nya mtu kitu kwa hila namrudishia mara nne. Yesu akamwambia, Leo wokovu umefika nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Ibrahimu. Kwa kuwa mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.”
TUMSIFU YESU KRISTO MILELE AMINA. JUMAPILI NJEMA WANDUGU!!!

7 comments:

  1. Ujumbe umekaa Kikristo kweli huu KIBINGWA!

    Jumapili njema Mpenzi Kiwanzabanga Bingwa hasa ukijua kuna Mwanaidi kikawaidi haamini KUNA BIKIRA MARIA aliyezaa bila kuonjwa ustaarabu!

    Pamoja daima Yasinta!:-(

    ReplyDelete
  2. Simon ha ha ha ha haaaaaaaaa!

    Da Yasinta Jumapili njema na kwako pia.

    ReplyDelete
  3. jumapili njema da Yasinta,KITURURU umeniacha hoi.

    ReplyDelete
  4. na ukitilia maanani kuwa ilikuwa BULABO mambo mswano tu!

    Pamoja sana

    ReplyDelete
  5. Yeah kila mtu hupata wokovu kwa namna ya pekee, wokovu ukifika huna ujanja hata ukiwa guest house utatoka tu na kuupokea.

    hata mtume paulo (Sauli)alipokea wokovu kwa njia ya ajabu sana.

    ReplyDelete
  6. Nawashukuruni wote kwa kutochoka kupita hapa kibarazani kwangu. Binafsi jumapili yangu imeishia kazini. Na naamini pia ndugu zanguni mmekuwa na j2 njema kabisa.

    ReplyDelete