Thursday, May 20, 2010

Ujumbe/kichekesho au sijui kucheza na lugha

Mmasai kaingia hotelini akaagiza chai na mkate. Alipomaliza kunywa akataka ankara (bill) yake. Alipopewa akakuta imeandikwa, Chai shilingi 300 na mkate shiling 200 jumla ikawa shilingi 500. Mmasai akalipa shiling 200, alipoambiwa hela haitoshi, akajibu...ero mimi nalipa mukate na mukate italipa shai. Kwa sababu mimi nakula mukate na mukate nakunywa shai. Akiwa na maana kwamba alikuwa akichovyo mkate kwenye chai na kula kwa hiyo hakunywa chai bali mkate ndio uliokunywa chai......Hii nimetumiwa na rafiki nimecheka sana nikaona tucheke pamoja

11 comments:

  1. umeifanya siku yangu iwe murua kwa sana tu :-)

    ReplyDelete
  2. JE wewe unachovya au unachovywa?

    kuna aina nyingi tu. ulimi na midomo, na south to south

    kwangu sio kichekesho ni fumboo

    ReplyDelete
  3. Ha ha ha ha ha haaaaaaaaa!!!
    Eti mukate italipa shai.....

    ReplyDelete
  4. MMASAI soda nausa bei gani
    MUUZAJI mia tano
    MMASAI fungua
    MUUZAJI tayari
    MMASAI (akitoa hela) sasa pima ya 200
    MUUZAJI @#%*&)(????

    ReplyDelete
  5. Dada Yasinta yuko wazi kwa kile kilichomchekesha. Sasa wewe ndugu yangu "kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa" unataka kutuelekza wapi? South to South, una maana kule "bondeni?" "Kwa Madiba?". Angalia usije ukawa unatupeleka taratibu Kagera kwenye shule ya "Katerero", walikochapwa mboko walimu wa kike na Mkuu wa Mkoa.

    This Is Black=Blackmannen

    ReplyDelete
  6. hahahahaha, hii kali sana! tena ukifikiria sura za hawa ndugu zetu jinsi walivyo siriaazz kwenye mambo ya malipo, lzm ucheke zaidi.

    nilidhani visa vya wamasai vimeisha...

    ReplyDelete
  7. Hiyo kali nimeipenda! unataka kucheka tena? ngoja nikupe na hii:

    Kuna mama mmoja mlokole aliyekuwa akiishi peke yake .. siku moja alirudi usiku sana amechelewa kwenye mambo ya maombi. Alipofika nyumbani baada ya kujiandaa kulala..kabla ya kulala aliamua kusali kama ilivyo kawaida yake.. aliomba mambo mengi.. ikiwemo kuwaombea wezi, vibaka na majambazi... alisema .. Eee Mungu ondoa hasira za wanadamu..uwaokoe wezi,majambazi, wakabaji na vibaka kutoka katika mikono ya hasira za wananchi.wasiuawe. wananchi wasiwauwe kwa hasira... aliendelea kuangusha sala zake..kuwaombea majambazi na vibaka...

    Mara ghafla waliibuka jamaa kutoka uvunguni mwa kitanda chake na maficho mengine na kumwambia .. Asante sana mama..tunakushukuru kwa kutuombea tusiuawe.. sisi tunaondoka na vitu vyako hivyo tunaviacha... mama wa watu alibaki ameduwaa! akamshukuru Mungu.

    ReplyDelete
  8. MMASAI: Dakitari nasani mimi inaumwa
    DAKTARI: Fungua mdomo nikuwekee hiki kipima joto...
    (Baada ya dakika mbili Daktari akakitoa kile kipima joto na kukitikisa kabla ya kusoma matokeo..)
    MMASAI: Memesa, memesa, memesa.. nafikiria ni nyu modeli ( akiwa na maana kwamba daktari alipoweka ile themometa mdomoni kwake alikuwa anajaribu kuimeza lakini akashindwa na kudhani hiyo dawa ni nyu modeli kwani haimezeki!!

    ReplyDelete
  9. kakamrope umenichekesha yaani sina mbavu maana hiyo sikuwahi kuisikia.

    ReplyDelete