Thursday, May 6, 2010

LEO NIMETAMANI KWELI HIKI CHAKULA KITAMUCHA NYUMBANI!!!!

Dagaa,ugali, samaki na ndizi,
mlo huu sijala muda mrefuuuu!!

Jamani mwenzenu niko katika msimu mbaya sana, mwaka jana nilichukua UNGA wa mahindi lakini sasa umeniishia. Na nimepita kila duka, nimepata unga lakini ni wa njano PALENTA kwa aliyezoea ugali kama mimi haunogi kabisa. Kwa hiyo nilipoiona picha hii mate wacha yanidondoke. Hali hii inanifanya niimbe wimbo huu NARUDI NYUMBANI EEEH, NARUDI PERAMIHO, NARUDI SONGEA NAKWENDA KULA LIKOLO LA NANYUNGU.....

19 comments:

  1. Wakati wewe unautamani kuna wengine wanautupa jalalani huku.....

    ReplyDelete
  2. Koero usiniambie mbona unanipandisha pressure jamani si vizuri hakuna anaweza kunitumia UNGAAAAAAAA!!!

    Foundation wewe ni mutu mubaya sana!!

    ReplyDelete
  3. ukisikia nyumbani ni nyumbani ndio hii inamkuta yasinta ngonyani. pole sana, ipo siku utaufakamia huo mpaka basi.

    ReplyDelete
  4. Yaani wewe Koero ndio unajua kweli kukatisha watu tamaa basi acha tujilie na lame kwa vijiti

    ReplyDelete
  5. Sasa kuna haja ya kufungua Duka la kuuza Unga wa Mahindi, Unga wa Muhogo, dagaa Nyasa, dagaa Kigoma, Mbelele, Mbasa, Migebuka, Kambale, Perege, Mangatungu, Chikandi, Ming'oko. Mmh! nilisahau viyenje na mfusulelu.

    Naomba nitafutie ka-fremu hapo mjini!!

    ReplyDelete
  6. Jacob unanitamanisha mfusulelu wa kutoka mngongoma kule Nakahuga. yaani hakuna mboga ya heshima kwangu kama hii!!

    ReplyDelete
  7. Unaweza kupata unga wa sembe mweupe mzuri kutoka South Africa (umeongezwa virutubisho kama selenium na vitamins), pamoja na dagaa na mawese, nyanya chungu na kila kitu kutoka hapa UK kwenye maduka ya wahindi. Huna rafiki au jamaa UK? Maana angalau gharama za kusafirisha zitakuwa chini, hasa miji kama London, na Birmingham kuliko kutumiwa kutoka TZ.

    Bi Mkora

    ReplyDelete
  8. Hahahaa mbavu zangu jamani,Jacob malihoja kanichekesha sana,haya dada mtafutie ka-frem hapo mjini arahisishe mambo yote.

    Jamani msimshambulie Koero bahati mbaya sio mtani wangu ila nimekaa na wachagga na mtaniwake mpare walikuwa hakinipa raha sana,mchagga alikuwa anasema kule upareni kawaida hula ugali kwa ramani ya thamaki(samaki)eti hupika ugali vizuri na mchuzi wenyewe huita "mthombe" sijui nimepatia hiyo?basi ugali utaliwa mpaka unakwisha kwa ramani ya samaki tu.

    Sasa hapo Yasinta ulitakiwa kusonga ugali wako na hiyo picha ya hicho kitamu weka mezani na mchuzi wako pembeni,aaah ukimaliza hapo unasema umekula ugali kwa samaki.

    ReplyDelete
  9. Yasinta ulitakiwa uishi Uingereza. Mimi huwa nasema tofauti ya Uingereza na Bongo ni majengo tu, ila karibu kila kitu kilichopo Bongo Uingereza kipo hadi sabuni za miche, na ukitaka kwa kipande unakatiwa.

    Kama alivyosema Bi Mkora, Yasinta hata hauhitaji kuagiza kutoka Bongo, agiza kutoka Uingereza.

    ReplyDelete
  10. Dada Schola, nimekupata, lakini nasikitika kuwa, mimi sijui niseme ni bahati mbaya au nzuri maana huku nipo na kule nipo.
    mama yangu ni Mpare na baba yangu ni Mchaga.......Mweh!!!!! balaa gani hili yarabilalamina.....LOL

    Kuna wakati nawashuhudia wazazi wangu wakibishana katika jambo halafu likageuzwa kuwa utani, inakuwa ni kichekesho kweli na sisi watoto tumeshuhudia jinsi ndoa ya wazazi wetu inavyonogeshwa kwa masihara mengi na utani hadi raha nawaambia...

    Hadi leo najiuliza hivi mie ni Mchaga au ni Mpare, kwani kwa mama ni kutamu hususan kwa bibi Koero na kwa baba ni kutamu, hasa kule kwa kina dada Subi....LOL

    Wakati Yasinta anatamani Ugali mie natamani mtori na Kisusio, au kuna wakati natamani Makande au UGALI NA PICHA YA THAMAKI kama alivyosema dada Schola hapo juu.....LOL

    Hapana sio kweli, kabisa huo ni uzushi wa Wachaga katika kuwadhalilisha wajomba na shangazi zangu, Upareni kuna neema zake kama vile uchagani kulivyo na neema, mama yangu amezaliwa katika milima ya upareni mahali ambapo mpaka leo kuna chemi chemi ya maji inayotiririka kutoka milimani na kutumika katika kilimo cha umwagiliaji....kuna vijito vidogo vidogo vingi vyenye thamaki wa kutosha...sasa iweje watu wale Ugali kwa picha ya THAMAKI?

    Nadhani na ndio sababu ya Mzee Mkundi kwenda kumuoa mama huko upareni kwani alijua faida za kuoa upareni, kwanza ni wapanga bajeti wazuri, ingawa wanakejeliwa kuwa ni WABAHILI.....LOL

    ReplyDelete
  11. Poleni sana mnaoumiss ugali sis huku kama kazi tunakula tuu kila siku kadri unavyotaka, halafu si unajua raha ya ugali mboga basi mi napenda na samaki au papa kisha weka kachumbari na pilipili kidogo bila kusahau mboga ya majani kama mchicha, spinachi au ile ya kwetu mchunga pamoja na ngogwe (nyanya chungu)

    ReplyDelete
  12. Kaka John! asante kwa pole ipo siku kweli kabisa

    Dada M! ndio hivyo tena.

    Jacob! hapo ndo umenifanya nizidi kutamani halafu umesahau likungu,mlenda poli na uyoga wee basi tu.
    Asiye na jina wa nakahuga usije ukasema huo mfusulelu ule wa kutia karanga?

    Bi mkore asante kwa taarifa hiyo nitafanya hivyo.

    Da PASSION4FASHION.TZ! nanukuu "Sasa hapo Yasinta ulitakiwa kusonga ugali wako na hiyo picha ya hicho kitamu weka mezani na mchuzi wako pembeni,aaah ukimaliza hapo unasema umekula ugali kwa samaki." mwisho wa kunukuu.

    Tatizo sio samaki tatizo sina unga ndugu yangu.
    Da Mija! basi ngoja nihamie huko Uingereza -Bongo au? LOL.
    Koero! afadhali ya wewe unatamani mtori na unaweza ukaupata muda wowote ule. Nikukuambia je mimi natamani ugali wa muhoga na mlenda pori pia mangatungu je ?

    Kaka Bennet! eeehh, jamani kutamanishani hivi ndio nini mwenzenu nazidi kupanda pressurre Duh! inabidi nifanye haraka kuhamia uingereza, mmmhh! nimestuka afadhali nirudi kwangu Bongo. ntaweza kula na pitiki.

    ReplyDelete
  13. mi na-miss sana menu yangu ya kila siku hasubuhi,yaani ilikuwa chai rangi,kama ikiwa ya maziwa basi ya unga,tena hapo ni lazima kuwe na maharage ya kutosha ambayo ntayachanganya kwa vipande vya vitumbua na kuweka sukari humo.haa,nikimaliza hapo lazima ninywe maji mengi sana,basi ilikuwa kama kunashughuli yoyote mbele yangu nitaifanya kwa ufanisi mkubwa

    ReplyDelete
  14. Umenikumbusha mbaliiiiiiiiiiiiii, utanifanya nikatafute dagaa leo, safi sana.

    ReplyDelete
  15. Bi Mkora nyie huko mna raha sana

    ReplyDelete
  16. Mumhery nakwambia huku UK wee acha tu unaenda madukani unakuta wahindi wanakuuliza kwa kiswahili unataka mhogo au sombe. Hasa huku niliko shemeji zangu kutoka Kongo wamemwaga kama njugu kutoka makambi ya Kigoma, basi wahindi wanaleta mpaka unga wa muhogo, kambare wakavu, migebuka,maharage, na hao dagaa hata ukitaka wabichi utawapata, usiulizie kisamvu, kiko kimeishatwangwa kabisa.

    Wajomba zangu waganda nao hawako nyuma, ukitaka matoke unayapata ya kutoka Uganda, sio zile ndizi za Carribean zinazoitwa sijui plantain hapana ni matoke kabisa na samaki wake kutoka Ziwa Victoria.

    Yasinta wewe tafuta rafiki tu awe anakutumia hata wale samaki wadogo kama dagaa kutoka ziwa Malawi/Nyasa, huna haja ya kuhamia huku, uzuri wa huku kuko kama Kariakoo ila mhu nikikumbuka ile mada yako ya umbea na majungu ni mwake! Ndio maana mie ninaishi zangu kijijini kabisa, nikihitaji hivyo vitu nawaagiza walioko mjini wananitumia au siku nikienda kuosha macho mjini nanunua! Pole ningelikuwa naishi huko mjini ningelikutumia unga wa sembe sio aghali hivyo.

    Hivi kwanini wenzetu wa Naija na hata Waganda wanaleta bidhaa na nyingine zinatokea kwetu sisi watz tunashindwa?

    Bi Mkora

    ReplyDelete
  17. Bi Mkora, watanzania hatupendi kuchukua risk ndiyo maana hatuleti bidhaa nje, mimi nimeona hadi uji wa ulezi kutoka Kenya, unaitwa 'uji mix'.

    Yasinta na Mumyhery wekeni anuani zenu watu wawatumie mnavyokosa huko kwenu.

    ReplyDelete
  18. Bi Mkora yaani huku tuliko basi tu Damija bora iwe hivyo maana!!!

    ReplyDelete