Tuesday, April 13, 2010

UJUMBE WA LEO:- NI VYEMA KUIJUA SIRI HII!

Huu ndio ukweli, ukitaka kupata furaha ya maisha

1.Sema kweli
2.Furahia maisha na furahisha wengine, Penda kwa dhati bila unafiki na bila masharti
3.Jiamini
4.Chukia kusema uongo
5.Tetea unachokipenda na kukiamini
6.Ukiwa dhaifu wa kukumbwa na mawazo potofu usichukie kumbuka mawazo pototfu yameumbiwa Binadamu
7Jitahidi kufikiri na kuwaza vyema ili uzidi kujiamini, kujipenda na na kuwapenda wengine. Yote yanawezekana.

Kumbuka usemi huu “ukivuliwa nguo chutama. Ukikosea tubu haraka.
Wastara huwa haumbuki……………

17 comments:

  1. Duh!

    laiti kama wengi wetu tungeijua siri hii basi yanayoonekana mitaani sasa yasingetukia!

    Aksante Da Yasinta kwa ujumbe huu.
    Ubarikiwe kwa sana tu!

    ReplyDelete
  2. ujumbe madhubuti. Asante Yasinta kwa ujumbe huu. Hii ndio siri ya kufurahia maisha.

    ReplyDelete
  3. Nimefurahia ujumbe huu dada yangu mpendwa Yasinta,siku zote najifunza mengi nikiipitia blog yako.
    Ranatus Kiluvia.

    ReplyDelete
  4. Swaadakta dada Yas, Nimekupata vizuri. Ukweli ni kwamba kama siri nyingi zingekuwa wazi basi mambo mengi yasingekuwa matatizo kwetu...

    ReplyDelete
  5. Asante Da Yasinta,

    Umetoa ujumbe mzuri sana. Nimeipenda hiyo kwamba ukivuliwa nguo chutama, nikakumbuka ile kichaa akikimbia na nguo zako, nini ufanye.

    MAKULILO, Jr.
    www.makulilo.blogspot.com
    San Diego, CA

    ReplyDelete
  6. Nimeipenda hii.....

    "ukivuliwa nguo chutama"

    Nahisi hapa kuna dalili ya kubakwa....LOL

    ReplyDelete
  7. Dada yasinta unaposema ukivuliwa nguo chutuma, nadhani huu ni mtizamo wa mvuliwa kwani hujui dhamira ya mvuaji .mengineyo nauunga mkono ,

    ReplyDelete
  8. @Koero: kama ni kubakwa ni kwa hiari, ama?...lol

    ReplyDelete
  9. NAMBA MOJA NI SALA MENGINE YANAFUATA

    ReplyDelete
  10. Stevie sala kwa nani? Mungu wa wazungu au Mungu wa kwetu?

    ReplyDelete
  11. SALA KWA UNAEMUABUDU KUTOKA NA IMANI YAKO,KAMA MBUYU AU MLIMA CHA MHM NINI MATOKEO YA MAOMBI YAKO KWA KILE UAMINICHO/ABUDU KUTOKANA NA IMANI YAKO.

    ReplyDelete
  12. umesema kweli dada..
    hayo ni mambo ya msingi sana yanayoweza kumfanya mtu aishi vyema na afurahie maisha yake

    ReplyDelete