Thursday, April 15, 2010

Ubakaji unavyodidimiza elimu Karagwe

Watoto wa kike kama hawa wapo hatarini
kubakwa kama hawatopata ulinzi wa kutosha
kutoka kwa jamii



SUALA la ubakaji kwa wanafunzi ni kosa la jinai kisheria na ki jumla linadidimiza maendeleo ya wanafunzi wa kike ambao ni waathirika wakuu.
Wanafunzi hawa huishia kupata mimba au magonjwa mbalimbali hali ambayo huwaathiri kitaaluma na hata na kjamii kwa ujumla. Haja ya kulipinga suala hili hasa kipindi hiki ambacho serikali inapigania kwa nguvu zote haki za mtoto wa kike awapo shule na pindi apatapo mimba akiwa shuleni.
Serikali ilishapitisha pia utaratibu wa kumruhusu mwanafunzi apatapo mimba kurejea masomoni pindi anapojifungua kwa minajili ya kunusuru maendeleo yake kielimu.
Suala la ubakaji katika wilaya ya Karagwe iliyopo mkoa wa Kagera bado lipo juu hivyo kutishia maendeleo ya elimu kwa mtoto wa kike.
Takwimu zinaonyesha kuwa watoto zaidi ya 54 walibakwa katika kipindi cha mwaka 2009, takwimu hizo kwa mujibu wa wakazi wa karagwe wanadai ni ndogo sana ukilinganisha na idadi halisi ya kesi zinazotokea hasa vijijini.
Mbali na ubakaji, wanafunzi kupewa mimba na wengine kuolewa kwa mwaka 2009 pekee walifikia 44 Karagwe ikiwa wilaya ya pili kwa ukubwa wa tatizo hilo ikitanguliwa na wilaya ya Chato yenye wanafunzi 74 waliopata mimba kwa kipindi hicho hicho.
Kwa mkoa wa Kagera kwa ujumla, Katika kipindi cha Januari 2009 hadi Desemba 2009 jumla ya wanafunzi 365 walipata mimba katika kipindi cha Januari mpaka Desemba 2009 kati ya hao wanafunzi 148 walikuwa ni wa shule za msingi na 217 walikuwa wa sekondari.
Wilaya pia ina jumla ya shule za msingi 212, kati ya hizo, shule 204 ni za Serikali na 8 za binafsi zenye jumla ya wanafunzi 105,229 wasichana wakiwa 53,491 na wavulana 51,738.
Shule za sekondari katika wilaya ya Karagwe zipo jumla ya 43 (zikiwemo 34 za serikali na 9 za binafsi). Ongezeko hili limeenda sambamba na sera ya nchi lengo likiwa ni kuchukua ongezeko la watoto wanaomaliza darasa la saba.
Mbaraka Ismaili mkazi wa kijiji cha Kagenyi wilayani Karagwe ambaye mtoto wake wa miaka 14 Fatuma Mbaraka alibakwa na mzee wa miaka 54 Ali Migeyo mwishoni mwa mwaka jana anasema kesi nyingi za kubakwa watoto zinafichwa na kuzimaliza kimila bila kufikishwa mbele ya sheria.
“Kesi za kubakwa wanafunzi hapa kwetu Karagwe zinaishia huko mitaani, aidha wanakubaliana na kumalizana kwa kuoana au kulipana kiasi fulani cha fedha, suala hili linajumuisha uongozi wa vijiji na kata ambao ndio wapo mstari wa mbele kushauri watu wamalizane,†anasema Mbaraka.
Mbaraka pia anasema kuwa “imezoeleka kusikia kesi za wanafunzi kubakwa au kupewa mimba katika maeneo yetu, na hakuna mtu anashangaa hilo, ni tabia mbaya ambayo serikali lazima ichukue hatua ili kunusuru watoto wetu wa kike.†Kwa hapa shule ya msingi Kagenyi tu kwa mwaka jana tulishuhudia kesi tatu za watoto wadogo kubakwa na kupewa mimba, kesi mbili kati ya hizo wazazi walimalizana wao kwa wao kulipana kwa kushirikiana na polisi na ni moja tu ndiyo ilipelekwa mahakamani.
Mbaraka aliwalaumu polisi na viongozi wa vijiji kuwa kikwazo kikubwa katika upatikanaji wa haki za wanafunzi wanaobakwa na wale wanaopewa mimba kwani ndio waliokua mstari wa mbele kuwashawishi wazazi kuyamaliza bila kupelekana mahakamani.
Fatuma Mbaraka anayesadikiwa kubakwa na mzee wa miaka 54 Novemba mwaka 2009, anasema watoto wanaobakwa wengi wao huacha shule kutokana na aibu wanayoipata.
“Mimi mwenyewe baba ndiye ananilazimisha kwenda shule, ila nina mazingira magumu sana kwani kila niendako nachekwa na wenzangu na wananiita mzazi, walimu toka nimebakwa sijawahi kusikia waseme kitu wala kuniita na kuniuliza,†anasema Fatuma huku akitoa machozi.
Mkurugenzi wa wilaya ya Karagwe Consolata Kamuhabwa anasema kuwa tatizo la ubakaji kwa wanafunzi ni sugu ingawa hatua kali zinachukuliwa dhidi ya watuhumiwa pindi wanapofikishwa mbele za sheria.
Kamuhabwa anasema moja ya sababu ya kuongezeka kwa ubakaji kwa wanafunzi ni imani kuwa wanafunzi hawana magonjwa ya zinaa hasa ukimwi, hili ni tatizo kubwa katika wilaya ya Karagwe.
“Watu wengi wanaamini kuwa kumbaka mtu mzima wanajiweka katika hali ya hatari kwa kupata ukimwi lakini kwa mwanafunzi inakua si rahisi kupata magonjwa kama ukimwi,†anasema Kamuhabwa.
Kamuhabwa anatoa sababu zingine zinazosababisha kuongezeka kwa matukio ya kubakwa kwa wanafunzi kuwa ni imani za kishirikina, matumizi makubwa ya madawa ya kulevya kama bangi na pombe kali aina ya gongo.
Anasema “mkuu wa wilaya hii kanali Fabiani Masawe amekuja na mikakati mikubwa ya kutokomeza tatizo hili kwa njia ya adhabu kali, kutoa elimu kwenye vyombo vya habari hasa redio za hapa Karagwe kama radio Karagwe na Fadeco FM ambazo zinasikilizwa zaidi na wakazi wa wilaya hii."
Afisa ustawi wa jamii wa wilaya Mary Kashaija anasema changamoto kubwa inayoikabili wilaya ni wazazi wa watoto wanaobakwa na wale waliobakwa kukaa pamoja na kuelewana kutoyafikisha masuala hayo mbele ya sheria.
“Tabia hiyo inachochea kuongezeka kwa tatizo la ubakaji kwani wanajua hata wakibaka basi watamalizana au kulipa fedha kwa wazazi na hivyo kutochukuliwa hatua, hali hiyo inaturudisha nyuma katika mapambano dhidi ya ubakaji kwa wanafunzi,†anasema Kashaija.
Kashaija alisema "tatizo hili ni kubwa sana, huwezai kaa wiki tatu bila kusikia kesi ya kubakwa wanafunzi,kesi zipo nyingi sana ukilinganisha na zile ambazo hazitufikii, kesi za kubaka na kutokuletwa kwetu ni nyingi kuliko zile zinazoletwa."
Inafikia hatua hata wazazi kuharibu ushahidi kwa kutokutoa ushahidi ili masuala hayo yaishe kwa wao kulipwa, kesi nyingi zinaisha bila adhabu yoyote kwa kukosa ushahidi, hali inatisha kwa kweli lakini tunakabiliana nayo kupitia elimu kwa njia ya vyombo vya habari, alisistiza afisa huyo wa ustawi wa jamii wilaya.
Mkazi wa kayanga wilayani karagwe Ester John alisema kuwa jamii inapaswa kutafakari kwa kuangalia suala zima la ubakaji ili kutafuta ufumbuzi kwani watoto wengi wa kike ndoto zao za elimu zinazimwa kwa tamaa ya baadhi ya wanaume kwa kuwabaka na kuwapa mimba wangali shule za msingi.
“hapa Karagwe tatizo la ubakaji ni kubwa sana mpaka sasa inaonekana kama ni kawaida jambo ambalo linasikitisha kwa kweli, tunaomba serikali itusaidie watoto wetu wanaangamia jamani,†anasema Ester.
Kesi kukosa ushahidi.
Sheria ya Kujamiiana ya mwaka 1998 inaeleza wazi kuwa kufanya mapenzi na mtoto, chini ya umri wa miaka 18 ni kitendo cha ubakaji, kwa kuwa kinafanywa kwa ulaghai na si hiari ya mtoto huyo.
Hivyo, kumfukuza mtoto huyo shule ni kumuadhibu kwa mara nyingine, kwani adhabu ya kwanza kapewa na yule aliyefanya naye mapenzi kwa nguvu au kwa ulaghai na kumpa mimba na ya pili ni kufukuzwa shule.
Kesi nyingi za kubaka wanafunzi wilayani Karagwe huisha kwa watuhumiwa kuachiwa huru kutoikana na kukosa ushahidi wa kutosha kwani wakazi wengi hawana mazoea ya kutoa ushahidi pindi kesi zifikapo mahakamani.
Kashaija anasema kesi nyingi hukosa ushahidi kutokana na gharama kubwa za mashahidi kusafiri kutoka kijijini mpaka wilayani kipindi cha kutoa ushahidi jambo ambalo linakatisha tamaa wazazi kutokana na kuelemewa na gharama na hivyo kuamua kulipana bila kufika mahakamani.
“Wilaya hii ni kubwa sana, utakuta mtu anatoka umbali wa kilometa 100 ili kufika mahakama ya wilaya kutoa ushahidi, kutokana na gharama za nauli kutoka huko mpaka mjini, mashahidi hao hushindwa kusafiri na hivyo kesi kuwa na ushahidi hafifu,†anasema afisa huyo wa Ustawi wa Jamii.
Raisi Jakaya Mrisho kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wamekuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za mtoto wa kike kielimu nchini kote huku raisi akiwataka wakuu wote wa wilaya na mikoa kuhakikisha wanakomesha tabia hizi za mimba kwa watoto wa kike.
Mapambano hayo yanaenda na sera ya kumlinda mtoto wa kike inayomtaka mwanafunzi aliyepata mimba kurudi shule na kuendelea na masomo pindi wajifunguapo ingawa wengi wao wamekuwa hawapendi kurudi shule kutokana na kuona aibu.
Vincent Mnyanyika, HakiElimu (Gazeti la Mwananchi)


Ngoja tumaliza na kumsikiliza dada yetu Saida Karolina wimbo huu (nkyalimuto)

8 comments:

  1. Kamala Upoooooo.....
    Hiyo ndilo shiranga la Wahaya na Wayaya....

    "Iwe Mushobozi, nakugambira, yure Kaisiki namuwona anavyopitaga hapa akihenda shure,,,,,
    Mhhhh...kamekuwa kazuri kweri,,,,,natamani kukabaka"

    ha ha ha haaaaaa.......
    Tunapoelekea naamni kule Karagwe wazazi watalazimika kuwasindikiza watoto wao kwenda shuleni na mtutu wa Bunduki....LOL

    ReplyDelete
  2. Koero: Hata kama waktembea na bastola kuwalinda na wabakaji bado hao wabakaji watawasubiri wakati wa 'mapumziko' shuleni :-(

    Si wajua katika karne hii bado shule zetu ni za MATUNDU? Na choo za wanafunzi wetu ni za MATUNDU?

    Na kwa kuwa uwiano wa wanafunzi na MATUNDU ya choo no mdogo wengine hulazimika kujisaidia porini?

    Utaona sasa kunahitajika 'overhaul' ya mifumo toka akili za watu hadi miundombinu :-(

    ReplyDelete
  3. Nafurahishwa sana na juhudi za HakiElimu, lakini kuna ukweli fulani ambao taasisi nyingi sana zinashindwa kuutambua. HakiElimu na Asasi zingine, Serikali na jamii sasa wanapaswa kuwageukia wanafunzi wenyewe, wanafunzi wanatakiwa kupata uelewa wa kutosha juu ya namna ya kuchukua tahadhari mbali mbali, bila kufanya kampeni za kuwabadili kisaikolojia watoto, mabilioni ya fedha yatatumika bila mafanikio au mafanikio yakiwa madogo mno. Huwezi kumlinda mtu ambaye yeye mwenyewe hataki kulindwa au hajui wajibu wake katika ulinzi huo. Mfano kampeni ya FATAKI, inawatazama zaidi watu wazima kuwa ndio wanaowaharibu watoto, ukweli ni kwamba watu wazima wanaofanya vitendo hivyo kwa watoto ni asilimia ndogo mno. Msichana yeyote akimkubali mtu mzima huyo tayari alishaanza na wavulana wanaokaribiana naye kiumri. Kwahiyo mapambano haya lazima yabadili muelekeo na kuweka mikakati na mbinu mpya zaidi, ambazo ni kuwajenga kiakili (kisaikolojia) wanaolindwa.

    ReplyDelete
  4. Du yaonekana Koero kamshika pabaya swahiba wake Kamala! Hoja nzuri sana hii Malihoja. Vibint vya kisasa vinawatega sana watu wazima. vinapenda kufatakiwa, kama huamini muulize Koero anajua vizuri hizi habari.

    ReplyDelete
  5. Hivi wabakaji wakihukumiwa na wao kufanyiziwa kuna ubaya wowote jamani?

    ReplyDelete
  6. hoja ya jacob imetulia,. tatizo la asasi zetu ni kuilaumu serikali badala ya kusaidiana na serikali kutafuta suruhisho. kunahitajika elimu kwa mabinti badala ya hukumu kwa wabakaji na kazi ya kutoa elimu wanaiweza hakielimu wenyewe

    @koero, kwa taarifa yako mke wangu ni mtu wa karagwe, amesomea kijijini na sasa ni mhitimu wa versity ya dar, na anandugu kibao waliosoma na wanaosoma wakike na wamesomea kijijini kwao n a hawajawahi bakwa.

    ila kumbuka wanawake wa kwetu sio kama nyie ndo maana wanavutia kuliko nyie

    ReplyDelete
  7. Kamala kama ungebahatika kuniona kabla naamini usingemuoa huyo mkeo....LOL

    Chaga + pare = Very Prety Gal

    Hata kwenye picha tu unanimezea mate ukiniona si utazimia wewe....LOL

    ReplyDelete