Sunday, April 18, 2010

HUU NI UJUMBE WA JUMAPILI HII YA LEO!!!

Wapo watu ambao nyoyo zao ni kama lulu au almasi inayongáa kwa usafi, hazibebi chuki, choyo wala kejeli, bali hubeba mapenzi, imani na ukarimu. Hakika hata wewe unayesoma hapa ni mmojawapo. NAWAPENDA NYOTE.

Tufurahia jumapili hii kwa wimbo huu SISI SOTE NI NDUGU ulioimbwa na Innocent Galinoma....karibuni sana!!

NA NI DOMINIKA YA 16 TANGU MWAKA HUU UANZE.!!!!!

12 comments:

  1. Haya, aksante kwa ujumbe murua.

    Uwe na wakati mwema.

    ReplyDelete
  2. NAKUNUKUU.......

    "Wapo watu ambao nyoyo zao ni kama lulu au almasi inayongáa kwa usafi, hazibebi chuki, choyo wala kejeli, bali hubeba mapenzi, imani na ukarimu. Hakika hata wewe unayesoma hapa ni mmojawapo"

    Kumbe nami ni mmojawapo?

    ReplyDelete
  3. Salaam kwenu nyote msomao hapa.
    Kama hujawa na moyo uliotajwa hapa, haimaanishi kuwa umepewa moyo huo na Yasinta (kama anavyodhani Da Mdogo Koero) bali wahimizwa kuwa nawe waweza kuwa mmoja wao. Anza kuishi hivyo
    Nawapenda, nawathamini na kuwaombea nyote. Kwa kuwa nanyi ni ndugu zangu. Yaani kama alivyomaliza Da Yasinta, SOTE NI NDUGU

    ReplyDelete
  4. Nimeliwazika na ujumbe, na kujihisi moyo wangu ni almasi.
    Jumapili njema

    ReplyDelete
  5. Ahsante dada Yasinta. Nasi twakupenda pia. Jumapili njema!!

    ReplyDelete
  6. Sikubahatika kupata muda wa kutosha kuwa kwenye net Jumapili, kwakweli ujumbe wa Yasinta kwa siku ya jana ni muhimu kwa kila mmoja wetu kuwa somo muhimu kwa maisha yake. Asante Yasinta kwa ujumbe huo!

    ReplyDelete
  7. Nachukua nafasi hii kwa kuwashukuruni wote kwa kutochoka kupita hapa na kuacha kitu. Nimefurahishwa sana na maoni yenuu mazuri. Mwenyezi Mungu awe nanyi na awalinde na kuwaepusha na mabaya. Upendo Daima.

    ReplyDelete