Tuesday, March 23, 2010

WANYAMA TU WANAJIFUNZA YAWAJE SISI TUSHINDWE???

Wanyama jamii hii ni wepesi kufundishwa!!
Wanasaikolojia watafiti walijaribu wakati Fulani kufanya utafiti ili kuona kama kweli wanyama wana uwezo wa kujifunza. Katika maeneo mbalimbali na kwa wanyama tofauti, waligundua kwamba kwa kiasi Fulani wanyama nao wanaweza kujifunza, wanaweza kubadilika kutoka maisha duni na kwenda maisha bora zaidi kwa kuiga.

Waligundua kwa mfano kwamba mnyama kama nyani anaweza kujifunza. Waligundua hilo baada ya kumuonyesha nyani tofauti ya vitu na baadae nyani huyo akaweza kubainisha au kupambanua kutoka katika vitu vitatu alivyowekewa, kitu kimoja ambacho ni tofauti na vile vingine viwili. Kwa mnyama kama nyani kujua na kubainisha tofauti ya vitu, siyo jambo dogo kama mtu anavyoweza kufikiria.

Njiwa naye aliwahi kufundishwa na kumudu kubainisha au kuchagua picha ya binadamu kutoka katika kundi la picha za vitu tofauti alilokuwa amewekewa. Njiwa anapofikia kumudu kujua kwamba hii ni picha ya binadamu na hizi nyingine ni za vitu vingine, sio jambo dogo. Hasa pale anapomudu baada ya kupewa mafunzo Fulani, kwani ina maana kuwa anaweza kujifunza na kuelewa.

Siyo hao tu, bali hata sokwe mmoja aliyekuwa akifahamika kwa jina la Lana aliwahi kufundishwa kompyuta na kumudu kuondoa kutoka kwenye kompyuta, maumbo Fulani kufuatana na namba baada ya kuwa ameonyeshwa tarakimu 1,2,3.

Mbweha-bahari naye kwa kujifunza mwenyewe ameweza kugundua kwamba kwa kutumia jiwe lingeweza kumtoa kutoka kwenye gamba lake konokono-bahari na kuji patia mlo. Hapo kabla, mnyama huyo hakuwa na uwezo huo hadi pale ilipotokea nasibu ambapo aligundua kwamba jiwe lina uwezo wa kuvunja gamba la konokono-bahari.

Ingawa baadhi ya wanasaikolojia wanabisha kwamba huko siyo kujifunza, kwa fasili yetu ya kujifunza tunaamini kwamba huko ni kujifunza. Kwa hali hiyo, tunaona kabisa kwamba hata wanyama wana uwezo wa kujifunza, pale inapotokea nafasi ya kufundishwa.

Lakini ni jambo la kusikitisha sana kuona kwamba, binadamu ambaye ana akili na nafasi ya kujifunza, anakuwa mgumu wa kujifunza, na hata akijifunza anaweza kutokea kuwa mgumu wa kubadilika. Kama njiwa anaweza kufundishwa na akamudu kuitambua picha ya binadamu kutoka katika picha nyingi nyingine, sokwe akaweza kucheza na kompyuta na mbweha-bahari akaweza kugundua udhaifu wake, ni kwa nini binadamu ambaye ni bora kuliko viumbe wote awe au ajiweke katika kiwango cha chini kuliko hao wanyama?

Tunajua kuna mazoea na tunajua mazoea ni magumu kufutika, lakini hatuwezi kufuta mazoea yetu mabaya kama kwanza hatutakubali kwamba sisi ni viumbe bora kuliko wanyama kwa sababu tuna uwezo wa kujifunza na kubadilika kwa manufaa yetu. Kama wanyama wanaweza kufundishwa na wakaelewa, ni kwa nini nasi tusiwe tayari kujifunza kila siku? Kuna njia mbalimbali za kujifunza kuhusu maisha, tunaweza kuzitumia na kuzifuata ambapo tunaweza kubadilika kabisa.

Kila siku tunapambana na mambo ambayo kama tutakuwa weerevu yanaweza kutusaidia sana katika kubadili maisha yetu. Kila jambo linalomtokea mtu ni elimu ya kutosha kabisa. Kama umepoteza fedha, kama umedhulumiwa, kama umepata hasara, kama umeachana na mpenzi wako au kama umefanikiwa, kama umefaulu na mengine ya aina hiyo, ni matukio lakini ni elimu pia. Tujifunze kuwa na tabia ya kujifunza kupitia katika matukio yote tunayopambana nayo.

Tujiulize kila tukio Fulani linapotupata kwamba tumejifunza kitu gani, badala ya kulalamika, kulaani au kufurahia tu. Kila tukio katika maisha yetu lina elimu ambayo tukiipata inasaidia kulielewa vizuri zaidi tukio litakalofuata. Tunaposhindwa kujifunza na kubaki watu wa kulaani nakurukaruka kwa furaha tu kila tukio Fulani linapotufika, tunakuwa tumejishusha sana na pia kupoteza mengi ya manufa. Kumbuka kila tukio maishani ni elimu ya kutosha kwa ajili ya mtihani wa maisha wa kesho yake.

Habari hii chanzo ni Jitambue....

12 comments:

  1. naogopa kujifunza nikishindwa watanicheka....... nasubiri yakushinde nikucheke...... Lol...........

    ReplyDelete
  2. Hivi binadamu naye si ni mnyama tu ila kaelevuka kidogo au vipi?

    ReplyDelete
  3. @ChIB, kaelevuka kachanganyikiwa zaidi? eti kwanini wewe huna uhuru wa kujamba na kufanya ngono? ni uerevu au uchizi??

    ReplyDelete
  4. Kwa mujibu wa binett mtalamu wa IQ alisema kuwa wanyama wenye jamii kama hiyo wanaubongo kama binadamu na kama wataishi na binadamu kunauwezekano mkubwa wa kujifunza lugha ya binadamu ni hayo tu dada yasinta kwa undani zaidi tembelea www.penzilakweli.blogspot.com

    ReplyDelete
  5. Kujifunza, katika ulimwengu huu kujifunza ni kitu muhimu sana. nakumbuka wakati nakuja hapa sweden nilikuwa siwezi kuendesha baiskeli nikawa najifunza, najifunza, najifunza na najifunza na nikaweza lakini nilipata jeraha kubwa kweli gotini mpaka kushonwa nyuzi kadhaa.

    Nadhani kila kitu kina wakati wake wa kujifunza viumbe ambao nawasifu sana kwa kujifunza ni watot. wao hawana aibu wana tabia ya kuiga na hii ni nzuri kwani ndo unajifunza kwa haralka. Kwa mfano lugha kama mpo ugenini watoto wanakuwa wa kwanza kujifunza lakini wewe mtu mzima....ngó. Tuna aibu kuiga!!!

    ReplyDelete
  6. Interesting idea but I'm not sure it would work

    ReplyDelete
  7. Hi there, I found your blog via Google blogsearch and your post looks very interesting for me.
    Buy Ultram Online Without Prescription

    ReplyDelete
  8. Hello, I think this is the coollest blog I`ve seen. I really like your theme.
    Order Cheap Cialis

    ReplyDelete
  9. Hello, I think this is the coollest blog I`ve seen. I really like your theme.
    Buy Levitra Online

    ReplyDelete
  10. Hello, your blog is fantastic. Congrats.
    Cheap Medications

    ReplyDelete