Sungura mjanja wee
Mwenzenu leo nimeamka na kujikuta naimba wimbo huu yaani nimekumbuka kweli nilipokuwa darasa la kwanza na pili haya unganeni nami na tuimbe:-
1. Sungura sungura mjanja wee x 2
Ingawa mdogo hushinda wakubwa x 2
2. Akili akili zatoka wapi x2
Ingawa mdogo hushinda wakubwa x 2
3. Akili watoto sisi tunazo x 2
Hata za kumshinda mjanja sungura x 2
4. Akili watoto sisi tunazo x 2
Shuleni twafunzwa mambo mbalimbali x 2
Ya kale ni dhahabu. Hivo uko katika njia muafaka kabisaa!
ReplyDeleteHa ha haaa...umenikumbusha mali sana! Asante sana.
ReplyDeleteWimbo siukumbuki sauti yake kabisa japo maneno nayakumbuka. Itabidi tumtafute Da Subi atutengenezee tu-redio twetu kama kwa Mzee wa Changamoto ili tuwe tunajirekodi na kuposti kitu live au?
ReplyDeleteKaka Chacha Wambura ni kweli kabisa!!
ReplyDeleteKaka! baraka nafurahi kana nimekukumbusha mbali!!
Da Mija unajua nina kanda hizoo kewani wanangu wanasikiliza. Na nakubaliana nawe inabidi turekodi. J e Da subi upooooo tayariiii???