Friday, March 5, 2010

Heri ya Siku ya Kuzaliwa Mume,Baba na Shemeji pia Rafiki yetu

Ni siku yako leo mwl. Klayson
Tunaanza na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa sala hii :- SALA YA MKE KUMWOMBEA MUMEWE

Ee Bwana , ni ajabu,
Jinsi fikra zangu zinavyomrudia kila mara
Huyu, mume wangu,
Mwenzi anayeshiriki maisha yangu kwa namna ya pekee.
Ninapofagia nyumba na mazingira yake,
Nataka kutengeneza nyumba nzuri kwa ajili yake.
Ninapopika chakula vizuri,Napenda kumfurahisha.
Ninaponunua nguo mpya na kujaribu kuonekana mrembo,
Ni kwa ajili yake tena, Ee Bwana.

Na ninaweza kukuambia kwamba
Ninamwonea fahari,
Anafanya kazi kwa bidii ili kupata riziki yetu;
Ni mtu mwenye haki, mwadilifu,
Naye hujitahidi kutufurahisha.
Kwangu, yeye ni mpole na mwangalifu.
Hunijali na kuonyesha kweli kwamba anajali.
Hunifanya mimi nijiamini mwenyewe,
Anajua jinsi ya kuondoa hofu zangu,
Hunipatia usalama na upendo ambao nahitaji sana.

Ee Bwana, ninakuomba,
Umbariki na umlinde.
Katika safari zake, umfikishe salama.
Kazini mwake, umpe fanaka
Na hapa, nyumbani petu naomba apate amani na heri.

Bwana, unisaidie mimi pia
Niweze kuwa yule mke anayehitaji.
Unifanye niwe mtu anayeweza kumwamini daima,
Mwanamke ambaye anaweza kumfurahia,
Niweze kumsaidia asahau matatizo yake,
Niweze kuondolea mbali hofu zake na kupunguza uchungu wake.

Bwana, Wewe ndiwe uliyenipa mume huyu,
Na katika yeye,Umenipatia sehemu ya nafsi yako mwenyewe.
Ninakusifu kwa ajili yake, Ee Bwana.

Na leo twakumbuka siku muhimu saana maishani mwako. Siku iiliyoanzisha yote mazuri/mema tujivuniayo maishani kwa uwepo wako. Ni SIKU HII ULIYOZALIWA

Zaidi mtembelee Mwalimu Klayson http://matetereka.blogspot.com/

Tunapenda kusindikiza siku hii na mwanamziki ambaye anampenda sana kwa wimbo huu wa DR. REMMY ONGALA Uitwao NARUDI NYUMBANI ni.



23 comments:

  1. Nianze kwa shukrani kwa MUNGU kwa uwepo wa kila mmoja wetu.
    Pili naleta salaam za heri ya siku ya kuzaliwa kwa Shemeji yangu lakini si kutoka kwangu tuu, bali kwa familia nzima hapa.
    Maisha mema na yenye baraka twamuombea.
    HAPPY BIRTHDATE

    ReplyDelete
  2. Samaki tupo wengi tuuu!!!! Happy Birthday Baba. Mungu aendelee kukubariki na kuishi miaka 100 kidogo :-)

    ReplyDelete
  3. ha ha ha haaaaaa, kumbeeeeee,
    Aiseee, hata sisemi happy birthday.....LOL

    ReplyDelete
  4. Heri ya siku ya kuzaliwa bwan'shemeji. Uwe na maisha marefu sana.

    ReplyDelete
  5. Duh, Heri y a kuzaliwa, uwe namaisha mafupi ya mwili, marefu ya roho!

    ReplyDelete
  6. hongeya kwa kutimiza miaka kazaa Mwalimu Klayson. mungu akujaalie miaka tele kadri ya mapenzi yake.

    du yasinta na wewe usita ulikukosa kidogo kama upadre ulivyomkosa mzee ngonyani nini? maana hiyo mistari!

    ReplyDelete
  7. Mungu akuongezee umri mara dufu na akuope afya njema

    ReplyDelete
  8. Hongera kwa siku yako ya kuzaliwa Mwalimu K.

    Uwe na wakati mwema nawakati ukikata keki jua tuko nanyi tukisosomola pamoja!

    ReplyDelete
  9. yasinta shemeji yetu anatimiza miaka minagapi mungu ampe umri mrefu wenye siha na afya

    ReplyDelete
  10. Happy birthday shemeji yetu,mungu azidi kukupa maisha marefu,hekima zaidi na mafanikio kwa kila unalokusudia kufanya lifanikiwe.

    ReplyDelete
  11. Yasinta hiyo mistari utasema ndo uliyopewa kwenye Unyago Duuh! Kweli wewe ni Mke mwema.

    Hongera Baba Camilla, Mungu awe nawe daima.

    Furahia siku yako.

    ReplyDelete
  12. Heri katika sikukuu yako ya kuzaliwa mwalimu.
    Mtunze dada yetu naye akutunze

    ReplyDelete
  13. Happy birthday Shemeji Mungu akujalie maisha marefu afya njema na furaha tele

    ReplyDelete
  14. Asante sana mke wangu. Pia sante kwa wote.

    ReplyDelete
  15. Grattis pÄ födelsedagen....Shemeji

    ReplyDelete
  16. Mlongo hongela sana na bambu kwa siku yake ya kuzaliwa, je umtelikili ugali wa mundula na chikandi?
    Za magono mlongo wangu? Nawatakia weekend njema kwako na familie yako.

    ReplyDelete
  17. Mlongo hongela sana na bambu kwa siku yake ya kuzaliwa, je umtelikili ugali wa mundula na chikandi?
    Za magono mlongo wangu? Nawatakia weekend njema kwako na familie yako.

    ReplyDelete
  18. Hongera kwa siku yako ya kuzaliwa Shemeji,

    ReplyDelete
  19. Ahsanteni wote kwa kumpongeza baba watoto wangu. Na pia ahsante sana kwa maoni yenu mazuri.

    ReplyDelete
  20. Kila lililojema mzee! Nakutakia maisha marefu ya mwili na roho

    ReplyDelete