Sunday, February 21, 2010

HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA KWAKO CAMILLA !!

Miaka 12 imepita leo tangu binti yetu Camilla azaliwe. Ni binti ambaye anapenda sana kusoma, kuandika, kucheza mpira wa mikono (handball) pia anapenda aina ya mziki wa kupuliza au (trombone. ) Twakuomba Mwenywezi Mungu uwe /uzidi kumbari binti yetu Camilla azidi kuwa kama alivyo. Na pia twakoomba uzidi kutupa sisi wazazi/walezi nguvu ya kumlea ili azidi kuwa binti mwema na mwenye busara. CAMILLA HONGERA SANA KWA SIKU YA KUZALIWA.
mama mdogo Koero anasema

Hata hivyo ningependa kufanya sala fupi kwa ajili yako.

‘Nakutakia sherehe njema ya siku yako ya kuzaliwa na natumaini kila jema lililosemwa na wote waliokutakia sherehe njema ya siku yako ya kuzaliwa litatimia. Mungu atakubariki uwe na afya njema na ukue kwa umri na kimo na pia mungu akujaze na Hekma na Busara na uwe na uzingativu katika masomo yako’

Aaamen..............

Pia maneno haya ya mjomba Mzee wa Changamoto ni mazuri sana na ndio nimemwomba mama ayaweke hapa mbele Ahsante "mjomba"

Dah!!!
Sijui nianze na lipi hapa?
Ok.... Kwanza POLE na HONGERA kwa wazazi.
Kwa wale waliopitia uzazi na ulezi wanajua kuwa HONGERA ya kulea ni vema ikaambatana na POLE yake. Ni kwa kuwa kulea ni zaidi ya kazi. Ni zaidi ya wajibu.
Lakini HONGERA kwa mara ya tena kwa baadhi ya yale niyajuayo kwa "Mjomba" Camilla. Kwa kuendelea kupenda asili za atokako, kupenda kujua na kuongea lugha ya asili ya Mama. Kupeda na kufanya kazi kama kilimo, usafi, kuchota maji na nyingine nilizoona ukifanya wakati wa likizo ndeeefu ya Ruhuwiko.
Hongera kwa wazazi kwa kuanzisha haya yote.
Kwa "Mjomba" Camilla. Uko ulivyo na unavyotakiwa kuwa. Unayotenda ndiyo yenye uzuri kuliko mtazamo wa wengi kuhusu watu. Ninalomaanisha hapa ni kuwa UNA MATENNDO MAZURI AMBAYO NDIO TAFSIRI YA UZURI.
Tatizo pekee la umri unaokabiliana nao sasa (na pengine miaka 8 ijayo) ni kuwa watoto wenye umri huu "hujiona wenye akili zaidi ya yeyote huamini marafiki kuliko wazazi" na huamini kuwa wako mbele na sahihi kimawazo kuliko wazazi.
Najua umekuwa msikivu na mtii kwa wazazi, basi hilo ndilo nikuombealo na kukusihi uliendele.
U-mrembo kwa Taswira tuonazo na TABIA tujuazo.
Baraka kwako katika miaka teleee ijayo.
HERI YA SIKU YA KUZALIWA "Mjomba"

26 comments:

  1. Oooh Kabinti karembo! Happy birthday Camilla...Mungu akupe Miaka miiingi na hekima kwa wazazi wako na watu wengine.

    ReplyDelete
  2. Hongera mjomba Camilla kwa kusherehekea siku yako ya kuzaliwa..

    ReplyDelete
  3. Dah!!!
    Sijui nianze na lipi hapa?
    Ok.... Kwanza POLE na HONGERA kwa wazazi.
    Kwa wale waliopitia uzazi na ulezi wanajua kuwa HONGERA ya kulea ni vema ikaambatana na POLE yake. Ni kwa kuwa kulea ni zaidi ya kazi. Ni zaidi ya wajibu.
    Lakini HONGERA kwa mara ya tena kwa baadhi ya yale niyajuayo kwa "Mjomba" Camilla. Kwa kuendelea kupenda asili za atokako, kupenda kujua na kuongea lugha ya asili ya Mama. Kupeda na kufanya kazi kama kilimo, usafi, kuchota maji na nyingine nilizoona ukifanya wakati wa likizo ndeeefu ya Ruhuwiko.
    Hongera kwa wazazi kwa kuanzisha haya yote.
    Kwa "Mjomba" Camilla. Uko ulivyo na unavyotakiwa kuwa. Unayotenda ndiyo yenye uzuri kuliko mtazamo wa wengi kuhusu watu. Ninalomaanisha hapa ni kuwa UNA MATENNDO MAZURI AMBAYO NDIO TAFSIRI YA UZURI.
    Tatizo pekee la umri unaokabiliana nao sasa (na pengine miaka 8 ijayo) ni kuwa watoto wenye umri huu "hujiona wenye akili zaidi ya yeyote huamini marafiki kuliko wazazi" na huamini kuwa wako mbele na sahihi kimawazo kuliko wazazi.
    Najua umekuwa msikivu na mtii kwa wazazi, basi hilo ndilo nikuombealo na kukusihi uliendele.
    U-mrembo kwa Taswira tuonazo na TABIA tujuazo.
    Baraka kwako katika miaka teleee ijayo.
    HERI YA SIKU YA KUZALIWA "Mjomba"

    ReplyDelete
  4. Happy Birthday Camilla, Mungu akujalie maisha marefu yenye afya tele

    ReplyDelete
  5. Happy Birthday mjomba Camilla!kila kheri na baraka katika maisha yako na wazazi

    ReplyDelete
  6. Natumaini utashangazwa na mengi sku ya leo.
    Kwa kuwa wengi watakutakia kila la kheri katika kusherehekea siku yako hii kubwa ya kuzaliwa.
    Nakuona hapo umejaa tabasamu huku wazazi, kaka yako mdogo, na majirani wakikupongeza kwa furaha na bashasha…

    Mimi Shangazi yako Koero nakutakia kila la kheri katika kusherehekea siku yako hii ya kuzaliwa,

    Kuna pongezi nyingi zinazidi kumiminika kwako leo.
    Naona kila mtu ametabasamu hapo nyumbani,

    Nasikitika kuwa ingawa ni siku yako kubwa na muhimu sana, lakini sitaweza kujumuika nanyi………..

    Hata hivyo ningependa kufanya sala fupi kwa ajili yako.

    ‘Nakutakia sherehe njema ya siku yako ya kuzaliwa na natumaini kila jema lililosemwa na wote waliokutakia sherehe njema ya siku yako ya kuzaliwa litatimia. Mungu atakubariki uwe na afya njema na ukue kwa umri na kimo na pia mungu akujaze na Hekma na Busara na uwe na uzingativu katika masomo yako’

    Aaamen..............

    ReplyDelete
  7. bila keki, mi sikubali mpaka nile keki ndio nitamwimbia ule wimbo wa siku ya kuzaliwa, hongera sana Mungu akuzidishie umri mara 10

    ReplyDelete
  8. Yasinta usinambie Camilla kazaliwa tarehe moja na mwanangu.!!! Mwenzao mwingine ni Rais Mugabe. CAMILLA HAPPY BIRTHDAY, Mungu akulinde na usisahau kuzidi kuwapenda wazazi wako. AMEN.

    ReplyDelete
  9. Wakati nina maoni yangu tayri kichwani, nakutana na kuzaliwa tarehe moja na Bob Mugabe.

    Mjomba Camilla, mie napenda kukutakia maisha marefu sana yaliyojaa furaha, amani na mafanikio.

    Uwe mwenye afya njema daima.

    ReplyDelete
  10. Dada unaona miaka inavyoenda na watoto wanakua eh? Juzi juzi ulikuwa naye hospitali, kufumba na kufumbua mdada kabisa! Happy Birthday Camilla! God Bless you! xx

    ReplyDelete
  11. Camilla hongera sana kwa siku yako ya kuzaliwa,unazidi kuwa mrembo,mungu akusaidie uendelee kuwa msikivu kwa wazazi.

    ReplyDelete
  12. Kama nitakua nimechelewa lakini
    ninakutakia maisha marefu hekima upendo na moyo wa kawaida kama alivyo mama yako,kwani tuna mpena mama yako

    nimwanamke ambaye nime tokea kupenda kwa kazi zake na moyo wake!

    Maisha marefu na afya njema..

    ReplyDelete
  13. Hongera kwa siku ya kuzaliwa Camilla, kila la kheri katika maisha yako, kuwa msikivu kwa wazazi na jamii kwa ujumla. Mungu akulinde na kukupa hekima.

    ReplyDelete
  14. Kheri saaaana kwa siku yako ya kuzaliwa ankal Camila.

    Mnyazi Mungu akujaalie uzima na baraka tele ukikua na hekima ya kumpendeza Mungu na wanadamu.

    AMINA

    ReplyDelete
  15. Camilla nakutakia heri ya kuzaliwa.mwenyezi Mungu akupe afya njema na endelea kuwa mtoto mzuri.Usimsahau Mungu wako.

    Hongeerani na wazazi..endeleeni kumpa malezi bora.

    happy birthday camilla

    ReplyDelete
  16. HONGERA CAMILLA NA MUNGU AFYA NA HEKIMA NA KILA LA KHERI

    ReplyDelete
  17. HONGERA CAMILLA NA MUNGU AKUPE AFYA, HEKIMA NA KILA LA KHERI

    ReplyDelete
  18. kwa upendeleo maalumu mie naomba niwapongeze wazazi kwa kumlea binti vema na hatimaye jana katimiza muongo mmoja na miaka miwili.

    kwa binti camilla 'ongela' kwa kutimiza miaka hiyo 12. mkulima huwa havuni mazao ambayo hayajakomaa. umri huo ni upendeleo wa mkulima mkuu- MUNGU. Basi na akuzidishie miaka kadri apendavyo YEYE. ukue uje kuwa mdada mzuri. mwambie mama akutafsirie ujumbe ulioandikwa na mjomba 'musee ya changamoto' hapo juu.

    Da Mija nakuomba ufanye kama hujui kuwa watoto hawa - wa kwako na wa yasinta- walizaliwa tarehe moja na robert mugabe. kwangu ni bahati mbaya kuzaliwa tarehe moja na mugabe. nadhani mugabe 'has gate-crashed' kuzaliwa na watoto hawa ambao kwa kuwaona tu hawatakuwa kichwa ngumu, hawatakuwa kichwa tupu, hawatakuwa ving'ang'anizi, hawatakuwa waoga, hawatakuwa wajinga kama robert mugabe.

    ReplyDelete
  19. Mwaipopo unajua hadi sasa hivi sijui kama nampenda au namchukia Babu Mugabe, Wadau hebu tusaidiane hapa hivi Mugabe tunamuweka katika kundi gani? Shujaa au mkatili?

    ReplyDelete
  20. Napenda kuchukua nafasi hii kwa niaba ya Camilla na kuwashukuru wote mliojumuika nasi hata kama hamkuwa hapa lakini tulikuwa pamoja. Ahsante sana kwa upendo wenu wajomba wote na mama wakubwa/na mama wadogo. Mungu awalinde nanyi pia.Upendo Daima.

    ReplyDelete
  21. Hongera Camilla, Mungu akuzidishie umri uwaone wajukuu na vitukuu vyako.

    ReplyDelete
  22. Namtakia binti maisha marefu yenye amani, furaha na kila aina ya mafanikio.

    Kwa wazazi, kwao hongera kwa kazi adhimu na muhimu ya kumlea binti yao vyema.

    ReplyDelete
  23. HAPPY BIRTHDAY TO YOU MY FEATURE WIFE
    TAREHE 13/3/2021
    HONGERA KWA KTIMIZA MIAKA KADHAA MY

    ReplyDelete