Wednesday, January 27, 2010

WATOTO WENYE VIPAJI MAALUM

Je unawezaje kuwagundua?

Watoto wenye akili za ziada au wenye vipaji vya ajabu ni watotot ambao, wamejaaliwa kuwa na IQ {Intelligence Quotient} kubwa kuliko kawaida. IQ ni kifaa maalumu kinachotumiaka kupima akili za binadamu.

Kwa kawaida, watoto wa ain hii wanakuwa na uwezo mkubwa katika masomo ya sayansi na hisabati, pia ni wabunifu na wajanja wa kufikiri haraka haraka na kupata majibu kwa njia za ajabu mno.

Ni watoto wenye uwezo mkubwa sana katika uongozi au wanweza kuwa na vipaji tofauti tofauti kama vile muziki, uigizaji na michezo mbalimbali.

Hata hivyo, tunawezaje kuwatambua watoto wa aina hii?

Kwanza watoto wenye vipaji maalumu , mara nyingi huanza kujibainisha wakiwa na umri wa kuanzia miaka miwili au umri wa miaka wa kuanza masomo ya awali. Wakati mwingine watoto wa aina hiiwhawajibainishi hadi wanapomaliza elimu ya msingi na hii inatokana zaidi na sababu za kibaiolojia .

Zifuatazo ni baadhi ya dalili za kumtambua mtoto mwenye akili za ziada.
* Huanza kuongea mapema kwa kutengeneza sentensi kwa ufasaha ukilinganisha na watoto wa umri wake.
* Wanakuwa na uwezo wa kupanga vitu kwa mpangilio sahihi kwa kufuata rangi au aina ya vitu.
* Wanakuwa wajuaji wa hesabu kwa kupenda kuhesabu vitu na hata kukokotoa hesabu.
* Wamejaaliwa kuwa na maono au wanweza kusoma hisia za mtu mwingine, kwa mfano mtoto wa aina hii anweza kumwona mama yake anahangaika ktafuta kitu na yeye akajua anatafuta nini na hata kujua mahali kilipo na hivyo kukifuata na kumletea mama yake, pia wanakuwa na uwezo wa kusoma mawazo ya wazazi wao au hata watu wa karibu wanaowazunguka
* Wanavutiwa sana na sanaa au muziki mapema mno na hata kupenda kuchezea vyombo vya muziki kama viko karibu nao.
* Wanakuwa na moyo wa upendo na hurumawakiwa bado ni wadogo wa umri ukilinganisha na watoto wengine wa umri wao
* Wanakuwa na tabia ya kujitegemea zaidi badala ya kuomba msaada kwa kila kitu, kwa kawaida huwa wanjiamini sana, hivyo ni aghalabu sana kuomba msaada kabisa. Huwa wanaamini katika wao.

Dalili za kuwatambua watoto wa aina hii ziko nyingi sana kulingana na mazingira yaliyowazunguka watoto hao.

Je watoto wa aina hii wanasaidiwaje ili kukuza vipaji vyao?
Watoto wa aina hii wanhitaji mapenzi sawa na watoto wengine kwani wazazi wengine huwa wanashindwa kuwaelewa watoto wa aina hii na hivyo kuwapuuza, kitu mabcho ni hatari sana kwa maendseleo yao. Wazazi wanatakiwa kufahamu kuwa, licha ya watoto hawa kuwa na akili za ziada, pia bado ni watoto kama watoto wengine.

Ila inashauriwa, wazazi kuwatengenezea watoto wa aina hii mazingira mazuri ya kuendeleza vipaji vyao, kwa kuwanunulia vifaa mbalimbali vya kuchezea, kulingana na matakwa ya vipaji vyao. Ikiwezekana kuwatengea vyumba vyao ambavyo watavitumia kufanya mambo yao bila bughuza, pia inashsuriwa kuwa ni vyema kuwasikiliza na kuwatimizia mahitaji yao.

Huko mashuleni nako inashauriwa kuwaandalia vipindi maalum vitakavyoamsha hisia zao, bila kusahau kuwachanganya na wanafunzi wenzao wenye akili za kawaida.

7 comments:

  1. duh, Hisabti na sayansi!!! vipi kuchunga mifugo vyema, kulima vizuri na kuongea kingoni kwa ufasaa??

    tanzania tuna viongozi wengi ambao walikuwa na vipaji maalum lakini uongozi wao ni feki na wa hovyo!!!

    anyway hata ulimwnguni watu wenye vpaji maaalumu wameishia kutengeneza siraha za maangamizi na teknolojia za kumharibu binadamu na mazingira yake!

    hata hivyo Albet Enstain yule mtoto mwenye kipaji maalumu wa Marekani aliyekuwa mtaalamu wa kila kitu alisisitiza kuwa hakkuna kipaji ili usikivu na utulivi akimaanisha meditation!

    ila Enstain kama Newton mpaka wanakufa walikuwa hawajaweza kuugundua/wlewa uchizi wa binadamu kwa kisingnizio cha akili zimsababishiazo matatizo binadamu huyo huyo!

    je Yasinta huna kakipaji maalumu angalau ka-kumfurahisha mumeo mpaka akanung'unika kwa furaha uliyompa? ni swali tu!

    ReplyDelete
  2. Naambiwa eti nilikuwa na kipaji maalum, nilisimuliwa na mama yangu Namsifu Kiangi Mkundi kuwa nilimudu kutembea na kuzungumza tena kwa ufasaha nikiwa na umri wa mwaka mmoja na nusu, nilikuwa na uwezo wa kuchezea TV na kubadilisha channels bila ya wasiwasi na nilikuwa ni mkali sana pale mtu anapotaka kubadili channel bila kuniomba, niliambiwa kuwa nilikuwa napenda sana kuangalia channel ya Discovery.
    Nilipofikisha umri wa miaka mitatau nilianza chekechekea na nilikuwa na uwezo mkubwa wa kuchora maumbo na wanyama, hasa twiga.

    Nilipofikisha umri wa miaka mitano niliumwa sana kiasi kwamba wazazi wangu walipoteza matumaini ya mimi kuishi, nasimuliwa kuwa aliitwa mchungaji kuniombea wakidhani kuwa ndio ninakufa baada ya kukaa ICU kwa siku tano nikipumua kwa msaada wa mashine.
    Katika hali ya kushangaza nilizinduka siku ya sita kabla ya mchungaji kufika kuniombea na kuanzia siku hiyo nilipata nafuu hadi kupona kabisa lakini nikiachwa na kasoro kadhaa katika mwili wangu.

    Madaktari walikiri kuwa kupona kwangu ni miujiza ya mwenyezi mungu (Her Cured is Miraculous)
    Nasikitika kuwa tangu siku hiyo kipaji changu maalum kilitoweka, na mpaka leo nakitafuta.
    Labda mungu alikuwa na makusudi maalum, na kama alivyosema Rafiki yangu Kamala kuwa watu wengi wenye vipaji maalum waliishia kutengeneza silaha za maangamizi na kumharibu mwanaadamu na dunia kwa ujumla.

    Nashawishika kuamini kuwa labda na mimi ningekuwa mmoja wao, na mungu akaona achukue karama yake……..

    Je kama ningekuwa na kipaji maalum, jamii ya wanablog wangemfahamu Koero Japhet Mkundi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kipaji hicho bado unacho unahitaji kukiamsha, kwa mtu wa jbada sanaaa

      Delete
  3. Koero binti kipaji, magonjwa au ajali hupunguza au kuongeza sana vipaji(hasa ukijeruhika kichwani).

    Kwa binadamu ubongo ndo kila kitu, na tunajua kwamba position ya ubongo ndiyo inayosababishia mtu kuwa mzuri katika kitu hiki na kushindwa kile. Ubongo una sehemu ambazo ni sensitive kwa vitu mbalimbali kama ya uchoraji, uongeaji au kumbukumbu n.k sasa hizi sehemu zinaweza zikawa zimebanana au moja imeiziba nyingine na hivyo kufanya sehemu moja kuwa sensitive au kuwa na nguvu kuzidi nyingine ndiyo maana utakuta huyu anaweza sana hesabu na huyu anaweza sana kuchora, ni mkao wa ubongo.

    Sasa tukirudi katika suala la ajali na kuumia vibaya kichwani, mara nyingi hubadili mkao wa ubongo na ukakuta mtu baada ya kupona hana uwezo fulani aliokuwa nao au uwezo mwingine umezaliwa.

    Niliona documentary moja ya mtu aliyepata ajali na kuumia vibaya kichwani alipopona aligeuka kuwa genius alikuwa akiona eneo lolote kwa mara moja tu analichora kama lilivyo hata kama kuna vitu vingi kiasi gani.

    Kwa hiyo Koero binti kipaji, wewe nadhani baada ya kupona sensitivity ya ubongo wako iligeukia katika uandishi na utunzi.

    Kwa maana hiyo basi si haki kumlazimisha mwanao kuwa kama mtoto fulani anayefanya vizuri katika jambo fulani.

    ReplyDelete
  4. Ukiniuliza miye nitasema IQ ni moja ya kipimo potofu sana cha akili za mtu.

    Na hata MTOTO awe naakili nyingi kiasi gani na AISHIPO ni MATOMBO na ayajuayo ni ya Matombo Morogoro, hawezi kwa kutumia kipimo cha IQ kushindana na MTOTO wa Dar es Salam katika kunyambulisha ya Dares salam kwa JINSI kitumikavyo kipimo cha IQ .

    Na naamini kila mtu kuna kitu IQ yake ni kubwa sana na hakuna JINIASI ambaye ni mkali kwa yote duniani. Na hata huyo Eintein ukifuatilia ukali wake kimasoma utastukia kuna masomo baadhi tu ndio alikuwa extraodinary .

    Tafuta yyoyte uliye wahi kusikia ni JINIASI na anabomba la miakili na haki ya nani utagundua ni wapi alikuwa MJINGA.

    Na kuna watoto ambao wanaonekana ni slow kimawazo ambao ndio kiboko katika mambo ambayo watu hawayapi tu kipaumbele.

    Haki ya nani karibu kila shule niliyowahi kusomea kulikuwa na mtu ambaye watu wanamuona kama zezeta ambaye kuna somo utamkimbia kwa maana utafikiri kalianzisha hilo somo yeye.

    Tatizo la Wazazi ni kufikiri na kutaka mtoto abobee katika wayatambuayo wao ni kabambe kitu kisababishacho mtoto jiniasi kwa mapishi kulazimika kufurahisha wazazi kwa kulenga udakitari tokea utotoni. Na jiniasi wakucheza mpira ndio kwanza anaweza kwa hilo akafinywa ili akajisomee zaidi Kifaransa.

    Ni mtazamo tu!

    ReplyDelete
  5. Na wale matoto tundu ambayo ukiyapa simu unakuta yameifumua yote kuangalia huyo mtu anayetoa sauti ndani ya simu anafananaje, na chochote kilichopo ni kuchunguza kwa nini kinafanya hivyo na kuishia kubomoa. Ni kipaji maalumu ambacho hatujui na kuwalaumu au kimezidi hata kile maalumu!

    ReplyDelete
  6. una kipaji, unaweza, lakini mazingira yako yanaruhusu kukimiliki kipaji?
    Na vipaji vya siku hizi ni kujaribu kufungua au kufanya vitu ambavyo wengine wamefanya.

    ndiyo maana katika makuzi hayo nakumbuka Erick Ericksson YA KWAMBA KAMA VILE MAONI YA JACQUES ROUSSEAU mazingira yanafanya kipaji au kuonyesha uwezo wa jambo kwakuwa vikuzungukavyo vipo karibu yako. Na hapo anakuletea NATURALISM katika makuzi ya kielimu na mengineyo.

    kwangu vipaji vya kunengua viuno kama wanabongofleva ni mazingira tu yaonyeshayo kuwa unakipaji. kuna mazezeta tu yapo kama hayapo lakini yanavipaji na miakili kumzidi shetani...lakini wenye vipaji wengine hawawezi kumzidi akili shetani.

    Na swali hili nilishindwa sana tena mara nyingi katika mitihani ya majaribio pale Mlimani ni WHAT IS TALENT and WHAT IS TALENTED?
    hakika sina jawabu lazima nikubaliane na mtakaifu asemavyo ni mahali/mazingira haki ya mungu yanakupa umudu kipaji. Je kipaji ni kubuni au kufanya vile ambavyo vimefanywa na wengine? HAPO NDIPO PENYE AKILI NA HEKIMA, ni hesabu za ubongo tu kuamua. KIPI KIPAJI KUBUNI AU KUFANYA KILE AMBACHO WENGINE WANAKIFANYA KWA KUJIFUNZA KWA KUANGALIA AU LABDA..... eeeeh kalagabahooooooo

    ReplyDelete