Mwaka mpya huwa ni wakati wa malengo mapya na mwelekeo mpya. Kila binadamu ana malengo yake hapa duniani. Mimi nina malengo yangu na wewe pia una yako. Kila kukicha huwa tunajitahidi kuyatimiza. Tunapasua vichwa kujaribu kuyatimiza malengo yetu . Ndio maisha.
Bila shaka na wewe umeshaketi chini na kujiuliza swali hili:- ninataka kutimiza malengo gani mwaka huu? Je? ni kurudi shule kuongeza ujuzi? Je? ni kuoa au kuolewa? Je? ni kujitolea zaidi katika jamii yako? Je? ni kutunza na kulinda mazingira? Msururu wa malengo unaweza kuwa mkubwa. Kama kutimiza malengo fulani fulani ndio mkakati wako wa mwaka huu basi zingatia ushauri ufuatao:-
Weka malengo yanayotimizika au yenye uhalisia-Jiangalie ulipo, angalia vitndea kazi ulivyonavyo, tizama kwa makini ujuzi ulionao kisha yapime vizuri malengo yako.
Jiulize swali au mawswali:- Nitayatimizaje malengo yangu? ukishafanya hivyo jiwekee utaratibu wa jinsi ya kutimiza malengo yako. Wazungu wanasema weka vyema Action Plan yako.
Nenda utaratibu -Mwaka ndio kwanza umeanza, yakaribiribie malengo yako kwa mwendo wa taratibu. Usiwe na haraka wala pupa. Si unakumbuka kwamba mambo mazuri hayataki haraka?
Usiogope kurekebisha malengo-Kadri mwaka unavyoanza kusonga mbele, unaweza kugundua kwamba huenda kutimiza malengo fulani. Hiyo inawezekana kutokea kwa sababu mbalimbali zikiwemo za kiuchumi, kiafya au kibinafsi. Usihofu kurekebisha malengo yako.
Usiogope kushindwa-Yawezekana kabisa ukashindwa kutimiza malengo fulani fulani. Kwa sababu zaweza kuwa kama hizo nilizozitaja hapo juu, usiogope. Cha muhimu ni kujaribu na kujaribu na kujaribu. Jitahidi kadri unavyoweza, nina uhakika ukijaribu utafanikiwa kwa hiyo mwisho wa siku hadithi ya kushindwa wala haitokuwepo.
La muhimu ni kuomba msaada inapobidi yapo mambo mengine ambayo hutoweza kuyatekeleza peke yako. Hilo linapotokea, usiwe mgumu kuomba msaada.
Kwa mara nyingine tena nawatakieni wasomaji wa blogya MAISHA kila la kheri katika mwaka huu wa 2010
labda ni mwaka mupya
ReplyDelete..'Weka malengo yanayotimizika'... Hapo Yasinta umenipa kitu ambacho sikuwahi kukifikiria, ni kweli kabisa si kila kitu kinatimizika kwa kila mtu, inategemea sana na hali na mazingira uliyopo.
ReplyDeleteHaya sasa ngoja nikafute baadhi ya malengo yangu kwenye diary yangu.
Stay blessed.
Hakika huu ni ushauri sahihi kwa mwaka huu.
ReplyDeleteKila la heri ya mwaka 2010.
shukran kwa ushauri
ReplyDeleteunadhani nikijiwekea lengo la kunywa ugimbi kila siku sitalitimiza? :-(
ReplyDeleteMwaka mpya...hii dhana inanitatiza kidogo....:-(
Ni mwaka, mtu, mawazo, nguo ama vitu vinavokuwa vipya? kipi kinatangulia?
Mh! ugimbi wangu karibu unaflet :-))