Wednesday, November 4, 2009

MWANAUME WA MIAKA 112 AMUOA BINTI WA MIAKA 17

Umri ni namba tu!!
Mamia ya watu walihudhuria sherehe za harusi ya mzee Ahmed Muhamed Dore mwenye miaka 112 akiaoana na binti aitwaye Safia Adulleh mwenye miaka 17.
“Leo Mungu ameniwezesha kufikia ndoto yangu” alisema mzee Ahmed Muhamed Dore baada ya kuoana na binti mbichi kabisa kutoka maeneo ya Galguud huko katikati ya Somalia.

Mambo yanayovutia kuhusu hii ndoa
Wanafamilia wa binti wanasema binti yao amefurahi kupata mume.
Bwana harusi alikuwa anasubiri kwa karibu zaidi binti aendelea kukua hadi amshauri waoane bila kumlazimisha bali kumvutia kwa upendo ili waoane.
Ni ndoa ya aina yake kwenye eneo ya Horn of Africa kwa babu miaka 112 kuoana na binti wa miaka 17.
Wapo watu ambao hawaridhiki na tofauti ya umri ingawa katika sheria za kiislamu inaruhusiwa.
Wapo waliofurahi na kukiri kwamba umri si kizuizi linapokuja suala la ndoa na kupendana.
Bwana harusi tayari ana watoto na wajukuu 114 huku kijana wake wa kwanza akiwa na miaka 80.
Bado anaamini huyu mke mpya ataendelea kumzalia watoto.
Zaidi anakiri kwamba ni Baraka sana kuwa na mtu unayempenda na akaendelea kukutunza.

Soma zaidi BBC

12 comments:

  1. Kama mambo fulani itakuwa poouwa ndani ya nyumba kwangu mie naona ni ruksaa vinginevo atakuwa mke wa wajukuu wake...lol

    kama babu yangu ana bibi mduchumduchu na analipa...wooi! kwa nini nsipite naye?...lol

    ReplyDelete
  2. huyu muzee hana spidi inayohitajika kwa ka-binti hako na no love ni lazima vijana wamsaidie

    ReplyDelete
  3. Binti huyo anatoka familia masikini na yenye shida ya mapigano.
    Human exploitation

    ReplyDelete
  4. Nahisi huyo bint anamdanganya mzee wawatu..hayupo real..

    ReplyDelete
  5. mishemishe, wote wanadanganyana...lol

    ReplyDelete
  6. 112 bado anaweza kuzalisha? He should be a miracle man...ila hii habari...she is happy? Doesn't sound real at all

    ReplyDelete
  7. NI SHIDATU ISITOSHE TAZAMA MALAYA)
    WENGI WALIOKO APA BONGO WANAOLEWA NA
    WAZUNGU WAZEE KUTAKA PESA TU.

    ReplyDelete
  8. Ni kweli wanapendana lakini huyu babu hataweza kukaridhisha haka kabinti lazima watu watamsaidia tu

    ReplyDelete
  9. Ahsante wote kwa maoni yenu ila nisiwakatisha mjadala huu endeleeni tu. Ila ngoja nami niseme kitu ni hivi kuna wengi wanafikiri kuwa akiolewa na mzee kwa vile ni mzee nbasi atamtunza vizuri kama vile mjukuu wake atamdekeze. Ila naona hapo kuna kitu kweli huyo babu mzee atawezana na huyu binti nina maanisha tendo la ndoa na anasema anataka kuzaa naye pia mmmhhh kaaazi kweli kweli sasa sijui hili ni penzi au ni tamaa, eeeh! ngoja niache isije nikatoka nje ya mada hii.

    ReplyDelete