Wednesday, November 25, 2009

Hata miguu nayo hupendezeshwa!!!! Swali je ni vibaya?

Vikuku ni urembo au?
KUNA mtu kanitumia hiyo picha anauliza hizo shanga za miguuni zinavaliwa kujiremba au zina maana nyingine?
Kwa mujibu wa maelezo yake, amewahi kusikia kwamba, shanga hizo a.k.a vikuku zina maana yake hivyo anaomba kufahamu kama ni kweli.
Anasema, kaelezwa kwamba, kikuku kikivaliwa mguu wa kulia ina maana yake, na kikivaliwa kushoto kinakuwa na maana nyingine, ni kweli?
Kama kila mguu una maana yake, vikivaliwa miguu yote inamaanisha nini?

10 comments:

  1. unaniliiiiiiiiiiiiino au ku.........

    labda sijui na maanayake si kuvaa. kwani nguo zina maana gani? unadhani zinaficha uchi? nani hajaona uchi, si kuvaa tu, na hizi wanavaatu

    ReplyDelete
  2. sasa Yasinta ungepaswa kutuambia kwanza huyoo aliyekutumia maana umedai amekwambia maana zake.Lakini cha kustaajabisha ujaweka hapa.

    Itakuwa vema uweke hizo maana hapa then sisi tuendelee kunyumbua..

    tutafika tu

    ReplyDelete
  3. Mimi naona haina ubaya wowote,ni urembo tu kama vile tunavyovaa hereni,saa,bangili n.k
    Napenda blog yako dada Yasinta,endelea kutuelimisha.

    ReplyDelete
  4. Nasubiri majibu maana nasikia tu ina "maana" yake ila hiyo maana hata siijui...

    ReplyDelete
  5. maana yake ni ngumu hata mtu aliyemwambia dada yasinta hakutaja waziwazi ni hayo tu!

    ReplyDelete
  6. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!November 26, 2009 at 5:38 AM

    naona wote mnazungukazunguka, mbona hamsemi?

    nilikuwa mwanza kwa siku 10 na mojawapo ya jambo ambalo nilijifunza ni kuwa ukimwona mdada kavaa kikuku (haikusemwa ni mguu gani) basi huyo hutoa 'jicho'. Kwa maana nyingine ukiwa katika mambo fulani ukmwambia naomba 'jicho' basi anageuka mweeeenyeweee...lol

    inakuwa kama ile story kuwa samaki ana pande mbili ukishakula upande wa mbele sherti AGEUZWE....lol

    na kuna nadharia hiyo hyo pengine kwa wakaka ambao wanavaa heleni pengine tungependa kusikia toka kwa wadau....lol jeni sikio gani mkaka anavaa tunajua kuwa si riziki?....lol

    ReplyDelete
  7. halafu Da Yasinta una mguu mzuri....lol

    ReplyDelete
  8. Shukrani kwa wote mliotoa maoni na naomba mjadala uendelee. Na usiye na jina samahani mguu sio wangu. pole sana:-)

    ReplyDelete
  9. Ha ha ha ha,nimelipenda jibu la Dada Yasinta kwenda kwa asiye na jina.
    Chacha asante kwa jibu la 1 kwa 1 maana naona watu walikuwa wanazunguka tu wakati majibu wanayo.
    Nilivyowahi kusikia mimi ni kuwa kuna mguu mmoja kikuku kikivaliwa hapo ndo humaanisha kutumika kwa mlango wa uani,sasa tungewekwa wazi hapa ili tujue ni mguu wa kushoto/kulia? hii itasaidia hata tukikutana nao basi tuelewe in which business they are in.
    Halikadharika kwa Wa'kaka,zile heleni zao kama zinatoa picha fulani na yenyewe tuambiwe ili tukikutana nao wametinga kwenye hilo sikio tuelewe mipango yao pia.
    Kwa nia njema tu lakini.

    ReplyDelete