Pia nimekumbuka mwimbo huu nilipikuwa darasa la kwanza na pili tulikuwa tukiimba kila siku:-
1. Kwaheri baba na mama twaenda shuleni x2
Kusoma huko shuleni pamoja na mwalimu.
Kuandika huko shuleni pamoja na mwalimu.
2. Kwaheri baba na mama twaenda shuleni x2
Kuhesabu huko shuleni pamoja na mwalimu.
Kuchora huko shuleni pamoja na mwalimu.
3. Kwaheri baba na mama twaenda shuleni x2
Kuimba huko shuleni pamoja na mwalimu.
Twaimba sote pamoja pamoja na mwalimu.
hapa nakumbuka mengi, natamani ningeweza kukuimbia
ReplyDeleteHahahahaaaaaaaaaaa!!!
ReplyDeleteHii ssaaana Da Y. Na kawimbo hako tulikokuwa tunakaimba japo hatumaanishi kalikuwa poa. Yaani unaimba tofauti na unavyotamani kufanya maana hakuna waliokuwa wanapenda kwenda shule, kuhesabu namba, kufaia mazingira na wengine kupeleka manyasi ama mbolea kwa ajili ya kipindi cha Sayansi Kilimo na mwalimu nanii yule mnoko na..................
Nakumbuka zamani kwa kweli na ule ubunifu wetu wa "kutunga" vitu kwenye uzi.
Duh
Asante sana kwa kutukumbusha tuliosoma shule za mtakatifu kayumba! je wakumbuka aliyekuwa wa kwanza alivyoheshimiwa na kupewa umonita cheo chenye heshima karibu na ile ya mwalimu,je enzi za kuandikwa mpiga kelele wazikumbuka?,je kale kawimbo ka idd amini akifa nitamtupa kagera awe chakula cha mamba je wakakambuka? mimi huwa nacheka peke yangu nikumbukapo wewe unafanyaje
ReplyDeleteYasinta una mambo! yaani imebidi nicheke maana umenikumbusha tulivyokuwa tunatengeneza vihesabio vya visoda tunafurahia ukifikisha vingi.Wanetu lazima tukawaonyesha adventures hizi maana zinafurahisha sana.Kazi nzuri dada.
ReplyDeleteKamala ni kweli hapa lazima mtu ukumbuke mengi unaweza kurekodi halafu tukusikie:-)
ReplyDeleteMzee wa Changamoto! unakumbuka kawimbo haka huyo, huyo huyo ni mjinga kabisa asiyependa shule ni mjinga kabisa barua akija aitembeza kutwa x2. Ni kweli nakumbuka kipindi kile kumchotea maji mwlimu, kumlia shamba, kwa huyo mtu akifikiria hivyo Duh!
Tandasi! usiseme yaani nimecheka kweli huo mwimbo wa idi amin tulikuwa tukiuimba kweli wakati tunakimbia mchakamchaka nakumbuka mengi sana basi tu Asante nawe pia.
Da Sophia! Ni kweli tena hivyo vihesabio vya visoda ninavyo hapa nyumbani wanangu walitengeza pamoja na babangu kwani unajua babangu alikuwa mwalimu wa wangu pia wakati nasoma darasa la kwanza na pili. Kwa hiyo akawatengenezea wajukuu walifurahi kweli na wanatunza sana kama kumbukumbu. Nayapenda maisha ya zamani na ya ubunifu. Asanteni wote.