Saturday, October 17, 2009

JUMAMOSI NJEMA WOTE:- TUMSIKILIZE LAMECK dITTO NA WIMBO WIVU WA KUPENDA.

Mara nyingi mapenzi huambatana na wivu, ni kama mapacha. Nimeupenda msemo huu mapenzi bila wivu ni kama chai bila sukari (chai bila sukari wala kitafuno) Ili mapenzi yakolee, wivu lazima uwepo .

6 comments:

  1. Wimbo nunau penda sana. Nausikiliza kila siku.

    ReplyDelete
  2. wivu hauna maana yoyote ile bali ujinga tu tunaouita 'kupenda'. mtaniwia radhi lakini ndo msimamo wa kikurya nilo nao...lol

    kwani wewe mdada unayemuonea wivu mskaji wako hasara ni nini hata ukimkuta na mwingine? ingekuwa ni mhogo kwamba utabebenwa uishe nadhani hapo ningeona mantiki ya wivu...lol

    Kwa hiyo kuweni wapole maswahiba wenyu wanapochelewa ama unapokuta meseji zilizopinda kama mawazo ya mtakavitu simon...lol

    mnakumbuka story ya mkubwa Kaluse katika moja ya posts zake?

    think twice kabla ya kuuamuru moyo wako uwe na wivu...lol

    ReplyDelete
  3. Kama katika watu kuna vilema, katika SWALA la wivu wa kuchukia kuna wapiga chabo:-(

    Au unafikiri hakuna wivu wa staili ya kuchukia?

    ReplyDelete
  4. mimi ni mtu! hata mimi naupenda sana huu wimbo kwani unafunza.

    Chacha Wambura Naona una msimamo mkali kweli Kwa hiyo inaonyesha wewe huna WIVU:-)

    Simon Mtakatifu:-)Ni kweli ukitaka mapenzi yakolee lazima kuwe na wivu mmmhhh, kazi kwelikweli hapa huu msemo ni mzuri sana.

    ReplyDelete
  5. YN a.k.a Kapulya, ukifikiri kabla ya kutenda nadhani unaweza kudhibiti hicho unachokiita wivu ama kupenda.

    Nimekuja kugundua kuwa kinachosababisha hicho mnachokiiita wivu na kupenda si upendo wenyewe bali hisia za upendo kwani upendo wenyewe hauchukii, hauoni wivu nk nk.

    na hisia za upendo huja na kwenda ni tofauti na upendo ambao upo tu no matter what.

    ama hujawahi kuona ama kusikia kuwa mume na mke walofunga ndoa kwa chereko hawalali chumba kimoja kisa 'upendo' haupo tena? kilichopotea si upendo bali hisia za upendo kwani wasingeweza hata kukaa nyumba moja..lol

    Na wakati mungine upendo umemaanisha hamu ya kutaka 'kitu' toka kwa huyo unayejidai unampenda...lol

    samahani kwa homilia a.k.a sermon ndeeefu inayoweza kumfanya baba mtakavitu simoni anitangaze kardinali mkuu wa kijiwe...lol

    ReplyDelete
  6. Naomba link ya kudownload wimbo huuu..

    ReplyDelete