Sunday, September 13, 2009

NAWATAKIENI JUMAPILI NJEMA KWA MLO HUU MTAMU WA NDIZI.


VIPIMO

Ndizi Mbivu 6
Nazi Kikopo 1
Sukari Vijiko 3 vya chakula
Hiliki Kijiko 1

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1) Menya ndizi kisha zipasue kati utoe ule moyo wa kati.
2) Zikate size unayopenda mwenyewe, kisha uzipange ndani ya sufuria.
3) Weka maji kiasi na uzichemshe ndizi kidogo, karibu ya kuiva mimina tui.
4) Mimina sukari na hiliki ndani ya ndizi na ziwache zichemke mpaka tui libaki kidogo.
5) Ziondoe jikoni na uziweke kwenye sahani tayari kwa kuliwa. Huu ni mlo wangu wa leo karibuni.

KIDOKEZO:

Ni nzuri sana kuliwa na kitu cha chumvi kama nyama ya kukausha au kuku wa kuchoma.

10 comments:

  1. Mbona unachemsha sas kikopo kimoja cha nazi...nikipi????Tunakaa wote ulaya sema Kopo la ukubwa gani lol

    ReplyDelete
  2. Mama yangu anapenda saaaaaana ndizi za namna hii. Na kwa chini kwenye sufuria huwa anaweka yale maganda ya ndizi (sio ya kula though lol) yaani kama kupata brown yapate hayo maganda, sio nzidi...Love this.

    ReplyDelete
  3. Kwa mara ya kwanza nasikia na najifunza namna ya kupika ndizi mbivu na kuzitumia kama mlo,kweli msosi wavutia, da! Nitjpika wangu kisha nami nikukaribishe.
    Chakula kilichopikwa kwa ndizi mbichi na nyama kwa mfano ni machalari, sasa hichi chaitwaje? Kiluga,kisw sio mbaya.
    Jpili njema dada Yasinta.

    ReplyDelete
  4. naomba kupindisha mstari, ati ni kweli kuwa wanaume hupenda mwanamke ajuaye kupika, na kama mwanamke ana kasoro jikoni huweza hata kufikia jamaa kutoka nje(kucheat)

    ReplyDelete
  5. Natumaini wote mlikuwa na jumapili njema kwani yangu iliishia kazni na ilikuwa njema pia. Namshukuru Mungu kwa yote. Na asanteni kwa wema wenu. Amina.

    Usiye na jina ni koo la 400g.

    Candy1 asant kwa mapishi mapya ntajaribu.

    Kissima, nakuomba ujaribu kupika hivyo utajiuma hata ulimi pia vidole kwa utamu.

    Viva Afrika. Basi hilo sio penzi:-)

    ReplyDelete
  6. ahsante sana kwa mlo mzuri, lakini mimi hupendelea kupika kwa karanga au peanut butter badala ya nazi,
    Shukran

    ReplyDelete
  7. Kissima kwa msaada ndizi hizi hujulikana kama Mkono wa tembo ni ndizi maarufu sana kule kwetu waja leo warudi leo
    Asante sana Dada Yasinta kwa kunimbusha chakula cha nyumbani

    ReplyDelete
  8. dada Yasinta unanitamanisha kweli, hivi ndizi kupata kijijini kwangu kazi sana, ngoja nizitafute sasa niko Stockholm

    ReplyDelete
  9. Οn а usual Tantrіс Маssаge treatment foг гelieѵing cοnsiԁereԁ 'alternate practice of medicine' iѕ now decеnt
    maіnstгeam. Ela ? mаis in intimate sexuаl intercourѕe is disguѕt fοr rake аnԁ
    ејасulate. Аccorԁing
    to some ѕtuԁies, men and wοmen expегience ѕеxual are trained іn
    sanative massagе which іѕ bаsed on Swediѕh massаge techniques.



    Here is my web blog ... website

    ReplyDelete
  10. Jamani nimejaribu kupika nivitamu balaaa

    ReplyDelete