Friday, September 4, 2009

ENZI HIZO....MWAKA 1947 WAKATI WA UJANA WANGUUUUUU!!!!


Leo nimeikumbuka picha hii wakati naishi kule Lundo- Nyasa kila siku kumenya mihogo si mnajua ugali wa mihogo na samaki kila siku. IJUMAA NJEMA JAMANI.

18 comments:

  1. Naomba nikuulize swali. katika picha hii kuna wadada watatu wewe ni yupi? Nimejaribu kulinganisha mmoja mmoja wa hao 'mabinti' na ulivyo sasa hakika nimeshindwa. si unajua miaka imepita halafu sehemu fulani hapa duniani watu husema mume na mke hufanana miaka inavyoenda, inawezekana umeanza kurandika ili ufanane na mmeo, au?

    ReplyDelete
  2. Akina kaka wako wapi?
    Au ilikuwa akina kaka kusogelea eneo mwiko?

    ReplyDelete
  3. Ndio raha ya taswira hii. Hivi kama kungekuwa na shindano la wewe kujieleza ulivyokuwa mwaka huo ungeweza kueleza kama ambavyo picha inatueleza?
    Raha saaaana. Nimeipenda hii.Hii ndio ilistahili kukaa kwenye portion ya MTANZANIA HALISI sio hiyo ya ki-Swidi (Lol)
    Niiiiiice one.
    Nasubiri ya Kaka Mkodo alipokuwa ndio anaanza sarandia mitaa mitaa. Lol

    ReplyDelete
  4. Hahahaha,mzee wa Changamoto mimi sina mbavu hapo,ya kale dhahabu hakika watu tunatoka mbali.

    ReplyDelete
  5. @Mzee wa Changamoto: : -) Nitakuwekea! Lakini mbona huwa naweka picha za longi kibandani mwangu?

    ReplyDelete
  6. Ha ha haaa. Mzee wa changamoto.
    Simon, bora umemkamua mzee, labda za kibandani kwako hajawahi kuziona.
    Da Yasinta, bila viatu, vp kila J'mosi walikuwa hawakutoi Tunga penetrans (SORRY KWA WALE AMBAO WAMETOKA KAPA)

    ReplyDelete
  7. ha ha haaaa......kaaazi kweli kweli, duh! dada hii imenikumbusha mbaaali kwa bibi Koero kule upareni..........jamani kwa kweli tumetoka mbali sana...

    Mzee wa changamoto acha uchokozi, unaitakiani picha ya mzee Mkodo Kitururu, unataka umuone akipiga baragumu kuwaita watu mkutanoni kule upareni nini? .....LOL

    Inabidi wanablog wote tuweke mambo yetu hadharani enzi hizoooo....LOL

    ReplyDelete
  8. Da Yasinta upo juuuuuuuuu kama maghorofa ya Dubai.
    Bila shaka we ndo mwenye twende kilioni kichwani.
    Duh,! Mwanangu kila kitu hapo orijino halafu bila shaka mambo ya dot.com ndo baaaado, kitu maadili ya dini ukijumlisha ukali wa mdingi, basi wauza sera walikuwa wanafulia tu.
    Kama anavyosema da Koero, wadau wekeni 47s zenu.
    Mumyhery nasubiri yako.

    ReplyDelete
  9. Koero nawe nasubiri yako. Yangu ushaiona niliyoipiga wakati nimetoka Kanisani. Nilikuwa napiga picha Jumapili nikitoka kusali tuu. Lol.
    Ya Kaka Mkodo nshaiona aliyokuwa anaimba rap ya kiingereza (nimeona miwani nikajifanya mtabiri kujua mpaka lyrics. Lol) sasa nasubiri yako ya enzi zileeee ulipokuwa "unafuta kamasi kwa ngumi". Hahahahahaaaaaaaaaa
    Fadhy kamtibua mkwe. Mamaaaaaaaa! Utakuwa "mkweless" ndugu yangu. Lol

    ReplyDelete
  10. Yasinta uko wapi? hutokei tu? njoo ujibu maswali hapa mimi nasoma hizi comment sina mbavu mzee wa changamoto,mzee mkodo na Fadhy mimi mbavu sina jamani,ila Fadhy nakushauri umtake radhi mama mkwe kabla mambo hayajaharibika,siunajua tena mama na mwanae.

    ReplyDelete
  11. Jamani nimerudi tena kwa nidhamu zote. Heshima yako mama mkwe. Nisamehe bure mama yangu. Ukininyang'anya huyu malaika ntaiweka wapi sura yangu, maana sitaki hata kufikiria jinsi kina Mubelwa na Mkodo watakavyonisimanga kuwa nimefulia.
    Ila niruhusu nimwombe da Yasinta ajitokeze na kujibu maswali lukuki humu.
    Siku njema mama mkwe.

    Sasa narudi kwenu wapambe, wivu tu huo kuona mi napata raha za dunia. Mlitaka nifulie? Da Yasinta mbona upo kimya, toa maufafanuzi.
    Pamoja na hayo wanangu tupo pamwinga (pamoja-Kibena) hivyo muwe na Jumapili yenye raha pasi karaka.
    Sana tu!

    ReplyDelete
  12. NAWAPENDENI WOTE NA NIMEJIFUNZA KITU HII NDIO RAHA YA KUBLOG. TUTAONANA WAKATI MWINGINE.

    ReplyDelete