Kuna wakati wanaume wanaweza kuwa na ugumu wa kujua kwamba wake au wapenzi wao hawaridhiki kimapenzi. Hiyo inatokana na uwelewa mdogo waliokuwa nao wanaume juu ya tofauti kubwa iliyopo kati ya wanawake na wanaume kuhusiana swala zima la hisia za kimapenzi.
Wanawake wana matarajio makubwa sana katika kila eneo linalohusu maisha yao, lakini linapokuja swala la tendo la ndoa mambo ni tofauti sana. Kwa kawaida wanawake wengi ambao hawaridhishwi na tendo la ndoa kwenye uhusiano wao huwa wanafanya siri.
Bila kujali kama tatizo liko kwao au kwa waume zao, wanawake hufanya siri kutoridhika kwao kimapenzi, na huweka siri kwa waume zao na hata kwa madaktari. Na ndio maana sishangai kuona kwamba wateja wa wauza dawa zinazohusiana na kuongeza hamu ya tendo la ndoa yaani Mkuyati ni wanaume.
Nilipokuwa nyumbani Tanzania, jijini Dar Es Salaamu nilishangaa sana kuona katika magazeti maarufu ya Udaku, {Tabloids} matangazo mengi ya biashara yanayotawala katika magazeti hayo ni ya kuuza dawa za kuongeza nguvu za kiume au hamu ya tendo la ndoa kwa wanaume na nyingine zilikuwa ni za kuongeza ukubwa wa maumbile ya kiume, dawa kama Mkuyati, Mzakaru, Super Shaft, Kifaru, Sekwa na nyingine chungu nzima ni maarufu sana jijini Dar Es Salaam.
Sio kwamba wanawake hawana matatizo ya tendo la ndoa, la hasha. Wanawake wanayo matatizo hayo ya tendo la ndoa lakini kwao hiyo siyo agenda, yaani si kitu cha kuwaumiza sana kichwa. Lakini kwa wanaume ni tofauti sana, wanapokuwa na tatizo la kukosa ufanisi katika tendo la ndoa huo utakuwa ni mgogoro mkubwa sana, kwani kwao hili ni jambo linalopewa kipaumbele kuliko mambo yote.
Kwa wanaume kukimbilia hospitalini au kwa mganga wa jadi na kusema “nina tatizo kubwa” ni jambo la kawaida kabisa…. Lakini wanawake hawafanyi hivyo, Badala ya kulifanya tatizo hili ni mgogoro halisi, huwekwa chini kabisa kwenye orodha ya matatizo yao, huwekwa kiporo na litashughulikiwa kwa wakati atakapojisikia kufanya hivyo kwa wakati wake.
Wanawake wanaweza kwenda kuomba ushauri au kuwasimulia mashoga zao, kuhusu matatizo ya ndoa. Lakini ni hadi wachokozwe ndipo wanapoweza kusema kwamba maisha yao ya tendo la ndoa na waume zao hayako sawasawa. Hilo halipewi uzito wa juu au naweza pia kusema hufanywa siri.
Wanawake hawaridhishwi na tendo la ndoa kwa sababu mbali mbali. Lakini bila kujali sababu hizo, kwao ni vigumu sana kusema kuhusu kutoridhishwa kwao. Ukiona mwanamke anatangaza sana kuhusu kutoridhishwa kwake na tendo la ndoa, basi ujue huyo na mumewe wako kwenye uhusiano mbaya sana. Kwani atakuwa anatumia maelezo ya kutoridhika kwake kama adhabu ya kumkomoa mumewe kwa kumuaibisha.
Lakini wale walioko kwenye ndoa imara ni vigumu kuwasikia wakilalamika kwamba hawaridhiki na tendo la ndoa. Inawezekana kutoridhika kwake kunatokana na yeye mwenyewe, yaani labda hana hamu au hafiki kileleni kutokana na matatizo mbali mbali yakiwemo ya kisaikolojia au matumizi ya baadhi ya njia za uzazi wa mpango, lakini bado sehemu kubwa wanaume huchangia. Hata hivyo pamoja na sababu hizo, mwanamke hayuko tayari kusema kuhusu kutoridhika kwake.
Kushindwa huko kunatokana na jinsi jamii ilivyomfunga mwanamke, kutoonesha kuhitaji tendo la ndoa. Akionesha kutoridhika na tendo la ndoa huonekana ni Malaya, kwa hiyo hukaa kimya na kuonesha kutojali.
Lakini bila shaka nadhani umefika muda wa wanawake kuwa huru kuhusu tendo la ndoa na kusema hisia zao wazi wazi bila kuogopa jamii itawaonaje, kwani jamii imekandamiza haki yao ya kuzungumzia tendo la ndoa kwa muda mrefu sasa.
Wanaume nao wanapaswa kujua kwamba wanawake hawapendi au hawawezi kuzungumzia kutoridhishwa kwao na tendo la ndoa, hivyo kutosema kwao kusitafsiriwe kuwa ndio wanawaridhisha, ni vyema kutoa ushirikiano kwa wake au wapenzi wao na kutafuta kujua kama wanawaridhisha. Ni jambo la busara kama mwanaume atadadisi kwa upendo na lugha ya upendo na kuonesha kama yuko tayari kutoa ushirikiano pale ambapo mke au mpenzi ataonesha kutoridhishwa na tendo la ndoa.
Ukiamua kujibu haraka haraka, naweza sema kuwa wakati wanaume wakinunua Mkuyati, akinamama wanatengeneza libwata...
ReplyDeleteanatibu magonjwa ya ini HEPATIS B ,,MAGONJWA YA FIGO,,UTI SUGU,,NGUVU ZA KIUME,,KUKUZA NA KUREFUSHA UUME,,,KUONGEZA HIPS NA MAKALIO NA SHAPE KWA DAWA ZA ASILI NA MITISHAMAA.....KUTANA NA DR KANYAS WA TIBA MBADALA 0744903557 TANGA
DeleteMkuyatii upo na dawa za majini ..biashara zipo pia
@Kibunango: DUH!
ReplyDelete@Dada Yasinta: Nawasiwasi tu na hiki usemacho kama kina ukweli kama nikunukuuvyo:
''Kwa wanaume kukimbilia hospitalini au kwa mganga wa jadi na kusema “nina tatizo kubwa” ni jambo la kawaida kabisa...''
Mie binafsi simjui Mwanaume ambaye kirahisi anaweza akakiri anakaudhafu ka kilambio na kirahisi tu akaenda hospitali kumuelezea mtu kuwa Khalufani mdogo anatambaa lakini hataki kusimama.
Ila nawajua waonao aibu hata kwa swala dogo kama la kuonekana wananunua KONDOMU na kwa hilo wanaweza mpaka ku-risk kucheza nayo kwenye kidude pekupeku:-(
Dada Yasinta, kuna moja umeisahau, inaitwa Chuma mbele......LOL
ReplyDeleteAmbiere Kitururu, nami nina wasi wasi na hicho usemacho, nakumbuka niliwahi kufanya mazungumzo na mtaalamu mmoja wa Jadi Pale maeneo ya mnazi mmoja jijini Dar. na miongoni mwa dawa ambazo alikiri kuwa zina mauzo sana ni zile za kukuza maumbile ya kiume na zile za kuongeza nguvu za kiume, cha kushangaza zaidi ni kile alichodai kuwa hata wanaume nao hufuata dawa za kutaka kuwashika wanawake wenye fedha sijui hili tuliiteje......9Limbwata la kiume au?)Lakini bila shaka kwa wale wanaoishi jijini Dar watakubaliana na mimi kuwa miongoni mwa dawa zinazoshika kasi kwa matangazo kwenye magazeti ya udaku ni yale ya dawa za kuongeza nguvu za kiume na kuongeza maumbile ya kiume......
Kwa hiyo mimi nakubaliana na utafiti wa dada yangu Yasinta kuwa wanaume ndio wanunuzi wazuri wa Mkuyati aka Mzakaru......LOL
anatibu magonjwa ya ini HEPATIS B ,,MAGONJWA YA FIGO,,UTI SUGU,,NGUVU ZA KIUME,,KUKUZA NA KUREFUSHA UUME,,,KUONGEZA HIPS NA MAKALIO NA SHAPE KWA DAWA ZA ASILI NA MITISHAMAA.....KUTANA NA DR KANYAS WA TIBA MBADALA 0744903557 TANGA
DeleteHili ni funzo zuri na elimu nzuri sana. Hongera dada Yasinta kwa makala hii murua
ReplyDeletekoeroooo!!!! 'mwanamume ananhitaji fedha au kulambisha kilambishochake chumvini?
ReplyDeleteanyway, mamboya ngono na ndoa ni magumu kidogo kwaniwengi huyafanya bila ujuzi wowote. inashangaza wanaume wanataka kuzikuzi zile lambio zao wakati G-spoti, pale pakunwako mtu akakunika na kukuheshimu iko juu juu tu na inahitaji tu kukunwa kiutaaluma na ipaswavyo ili mama alie bila kupigwa na baba atafune ganda la muwa bila kuwa na muwa karibu.
ni hofu na wasi wassitu. pia katika ulimwengu huu wa kufanya ngono huku unawasiwasi na hofu juu ya muda, kupigwa chabo nk, utamu upungua Muno.
anyway, namfahamu mama mwenye dawa ya kweli ya mapenzi inayomfanya mwanamke apende mchezo hadi kilio na kufyatua bao fyaaaaaaaaa na mume akafurahia.
yote ni kufifunza ndg
koero inaonekana una uzoefu na wale wataalamu uchwara eh??
!!!!!!
ReplyDeleteNIMEWASOMA SANA, LAKINI NOINA HALI ZENU ZIMESAWIJIKA KWA MDA HII.
ReplyDeleteNASEMA KAMA WATU WAPO, NA TATIZO LAZIMA LIWEPO. VITAMBI VIMEZIDI NA WALA HAWANA HALI ZA KUGEUKA KUWA WAKWELI. lol..... KUNA WANAWAKE WAMEOTA SUGU HATA UKAPIGA MASHUTI YA LAMPARD 10 WALA WANAONA KAMA UMEGUSA KIONJEO KWA ULIMI.
NINAMASHAKA NA MADA HII KAMA KWELI INAFANYIWA UTAFITI. KWANZA SISOMI KABISAAAAAAAAAAAAAAAA MAGZETI YA KIPUUZI KAMA HAYO. NADHANI TATIZO HILI LIPO DAR ES SALAAM! WIZI MTUPU.
KUNA JAMBO MOJA TU LA KUHIMILI HILI JAMBO NI KUMILIKI ILE KITU UKIWA MZIGONI. USITANGULIZE HISIA KUWA UTAMU UNAPOKOLOEA UKAKUFANYA UKAPOTEZA MSINGI WA KUMILI MTARO, WE CHIMBA TU........ LOL HA HA HA HA HA UKITAKA KUFIKA 3, HAKIKISHA 1 NA 2 UWE UMEPITA..... LOL KUNA HADITHI MOJA ILISEMA HIVI "NILIKUNYWA MKUYATI, NIKALA HADI NILIKOTOKA"....... YAANI AKALALA NA MAMAKE.....
UTAMU HUTAFUTWA JAMANI,..... NADHANI TUNAHITAJI UTAFITI WA KUTOSHA KATIKA HILI KULIKO KUKUBALI HAYA MATANGAZO.... NITAANZA RASMI......
KOERO...... LOL ETI KUWASHIKA WANAWAKE WENYE PESA... HA HA HA KUNA JAMAA PALE KARIAKOO ANAMILIKI VIJIDUKA VINGI KWASASA SABABU YA WANAWAKE WA AINA HIYO.... TENA LIMWANAMKE LINGINE NALIJUA LINAKAA UPANGA...... LIMKEW LA MTU, KUNA IDADI KADHAA YA MIMAMA TOKA OBEY, INAENDESHA MAGARI MODEL MPYA MPYA LAKINI YANAFUKUZI UKUNI WA MSHIKAJI..... HA HA HA LOL MNALO WANAWAKE KWANI MLIDHANI KUCHUNA MABUZI MNAWEZA NINYI TU.......... TENA SIKU HIZI WANAWAKE WAKUBWA WANAITWA AC MILAN YAANI ILE TIMU YA SOKA YA ITALI INAWACHEZAJI WENGI WAKONGWE.........
WANAWAKE WEWNYE PESAAAAAAAA, NASEMA HIVIII WANAFUATWA NA VIDUME UCHWARA..... DUME LENYE UHAKIKA HALINA MUDA HUO...... WAKATABAHU...... UTAMU WA RUNGU AUJUAYE MTWANGWA..... UTAMU KOLEEEEEEEEEEEAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
NIMEFURAHI SANA MARKUS KUKUBALIANA NA HILO LA WANAUME KUWAENDEA WANAWAKE WENYE PESA KWA WAGANGA ILI WAWASHIKE, MAANA KAMALA KANISHUSHUA KUWA SISEMEMI KWELI... SASA KAZI ANAYO KAMA YEYE ALIKUWA HAJUI BASI KACHELEWA, WENZIE WAJANJA WANA MIKWANJA NA WANAENDESHA MAGARI YA NGUVU KWA KUTEGEMEA UCHUMI KUTOKANA NA VIFANYIO VYAO......KAMALA UPOOOO.....KALAGA BAHO, UTASAGA LAMI WAKATI UCHUMI UNAO...LOL
ReplyDeleteKAKA KITURURU NA WEWE HUNA HOJA , NAONA MADA IMEKUSHINADA MAANA IMEKUWA YA MOTO...... KIBUNANGO NAWE....LOL.......KAAAAAZI KWELI KWELI, MIE SIMO NA MSINITAFUTE
anatibu magonjwa ya ini HEPATIS B ,,MAGONJWA YA FIGO,,UTI SUGU,,NGUVU ZA KIUME,,KUKUZA NA KUREFUSHA UUME,,,KUONGEZA HIPS NA MAKALIO NA SHAPE KWA DAWA ZA ASILI NA MITISHAMAA.....KUTANA NA DR KANYAS WA TIBA MBADALA 0744903557 TANGA
DeleteNafurahi kuona wote mmmeipokea hii mada vizuri nashukuru sana kwa ushirikiano wenu. Nami pia najifunza zaidi toka kwenu.
ReplyDeleteanatibu magonjwa ya ini HEPATIS B ,,MAGONJWA YA FIGO,,UTI SUGU,,NGUVU ZA KIUME,,KUKUZA NA KUREFUSHA UUME,,,KUONGEZA HIPS NA MAKALIO NA SHAPE KWA DAWA ZA ASILI NA MITISHAMAA.....KUTANA NA DR KANYAS WA TIBA MBADALA 0744903557 TANGA
ReplyDelete