Tuesday, June 30, 2009

USAFIRISHAJI WA HARAMU WA WATU/BIASHARA YA WATU

Tatizo ni lipi?
Hiki ni kitendo cha kinyama sana kumuamisha mtu kutoka kwenye jumuiya yake na kwenda sehemu nyingine ndani au nje ya nchi kwa ahadi za uongo. Matokeo yake ni kunyanyaswa na kutumikishwa kwa kupita kiasi bila ya ujira kwa faida ya mtu mwingine. Hii hujulikana kama utumwa mamboleo na ni moja ya matishio makubwa ya haki za binadamu. Inasemaekena usafirishaji na biashara haramu wa watu huwatokea zaidi wanawake na watoto, Ingawa pia huwatokea wanaume kwa kiwango kidogo sana ukilinganisha na makundi hayo mawili.

Usafirishaji na biashara haramu ya watu hutokea duniani kote na unyonyaji wa watu kutofautiana kati ya nchi na nchi. Kwa mfano huko Afrika Magharibi hususana Togo watoto wanatumikishwa na kunyanyashwa katika mashamba ya kokoa yaliyopo huko Ghana. Wasichana huko Colombia wanalazimishwa ukahaba huko Japan nk, nk.

Pia tatizo hili halijaziacha nchi za afrika mashariki na kati zikiwemo Malawi,Burundi, na Rwanda, Jambo hili linaonekana linazidi kutapakaa sana ndani kwa ndani na linalenga zaidi watoto wanotumikishwa kazi za ndani maarufu kama house Girls.

Inasemekana Tanzania inatumiwa na wafanyabiashara hawa haramu kama nchi ya kupitishia wahanga hawa kutoka nchi za Ethiopia na Somalia na kupelekwa Afrika kusini.

Kwa watoto mara nyingi au kwa kawaida hutolewa vijijini. Kwa kuahidiwa MAISHA bora na ELIMU mjini na ndugu zao wa karibu au watu wanaoaminiwa na wazazi wao. Wakati mwingine watoto hao hutolewa na wazazi wao kwa ndugu kwa mategemeo watoto wao watapata MAISHA BORA wakiwa mjini.

Lakini wakati hali huwa sio kama walivyotegemea. Unyonyaji ni pamoja na kulazimisha muhanga kufanya ukahaba, kazi za ndani, biashara za mitaani, kuosha magari, na bila kupewa nafasi ya elimu na matibabu na mbaya zaidi bila kupewa chakula hata kidogo. Kunyanyaswa kwa jinsia, kutukanwa kupigwa, kutishiwa na kufanyishwa kazi bila ya ujira. Watoto wengi hufanikiwa kutoroka na mwisho huishia mitaani.

Sababu
Nadhani elimu itakuwa ni moja ya sababu kubwa. Upatikanaji mkubwa wa elimu mjini huvutia vijana wa kike na kiume kutoka vijijini. Wahanga wengi waliosaidiwa na Internatinal Organization for Migration (IOM) ni watoto walioacha shule au hawajawahi kwenda shule kabisa vijijini kwao. Watoto waliosaidiwa na IOM ni kutoka Uganda, Tanzania, Kenya Burudi pia Oman na nchi nyingine za uarabuni. Mpaka kufikia leo, zaidi ya wahanga 118. Taarifa nyingine zinasema IOM imefanikiwa kuwasaidia wanawake 115 na watoto wahanga wa usafirishaji na biashara haramu ya watu kurudi na kuungana na familia zao toka Uganda.Pia kupoteza wazazi wote wawili. Hali hii husabisha watoto kulazimika kutegemea walezi.

Aina ambayo inatambulika zaidi, zaidi Tanzania:-
Watoto:- vijana wa kike na kiume husafirishwa katika biashara haramu kutoka vijijini kwenda mjini kwa ajili ya utumishi wa ndani ya nyumba (house girl and house boys). Wasichana husafirishwa katika biashara haramu na kuletwa mjini na katika maeneo ya kitalii.

Ebu tujiulize maswali:-
1. Je nini hatima au mustakabali wa mtoto huyu ambaye amehamishwa toka katika jamii yake kwa sababu ameahidiwa au familia yake imeahidiwa kuboreshewa maisha?

2. Je ni namna gani jamii na serikali kwa ujumla inaweza kuwajibika ili kutokomeza tatizo hili ambalo inaonekana kuwa kikwazo kwa ustawi wa vijana wetu ambao inasemekana kuwa ndio taifa la kesho?

4 comments:

  1. Huu ni unyama mkubwa sana kwa sababu familia zinazotoa ndugu zao ili wakafanye hizo kazi za ahadi huwa ni za mafukara na duni, wanakubali ndugu yao akafanye hivyo vibarua kwa matumaini ya kutuma pesa nyumbani ili ziwasaidie waliobaki lakini matokeo huwa kinyume
    Tatizo kubwa ni umasikini na njaa ndio maana nasema hakuna maendeleo kama watu wana njaa na mapinduzi ya kilimo ndio suluhisho pekee

    ReplyDelete
  2. Hi biashara bado ipo, nashangaa sana. Walaaniwe

    ReplyDelete
  3. Mmm jamani hii ingepaswa iwe imeshaisha. Hii si haki hata kidogo.Inafaa kulaaniwa kwa nguvu zote.

    ReplyDelete
  4. Nina mashaka na maoni yangu.

    Nitarudi baadae.

    ReplyDelete