Monday, June 29, 2009

TUENDELEE KUANGALIA NINI KINAWEZA KUTOKEA BAADA YA KUACHANA (NDOA KUVUNJIKA)

Kwa vile nishaanza kuongelea kuhusu -WANAWAKE UGHAIBUNI(SWEDEN)basi nimeona si vibaya kama pia tukijua:-

Baada ya kuachana mume na mke ambao walikuwa wanaishi pamoja. Unakuja mzozoz sasa kila kitu kichokuwa ndani ya nyumba ni lazima kugawana sawa.
Pia kama mlikua na nyumba ni lazima kuiuza na kugawana pesa, au kama mmoja wenu anataka kuishi katika nyumba hiyo. Basi ni lazima wewe umlipe yule atayeondoka nusu ya thamani ya nyumba. Gari pia vivyo hivyo kama nyumba.

Na halafu kitu kingine ambacho wengi wetu mtaona ni kinyume na Afrika kwetu (Tanzania). Najua Afrika hasa Tanzania watu au niseme mke na mume wakiachana watoto ambao ni wakubwa wanabaki kwa baba. Isipokuwa wale wadogo yaani ambao bado wananyonya ndio mama ataondoka nao/naye.

Hapa Sweden HAKUNA hiyo watoto wanakuwa mali ya mama mpaka watakapokuwa 18 ambapo wanaweza kuamua wapi wanataka kuishi. Lakini uzuri wake wakati huu wote watoto au mtoto anakuwa na mawasiliano na wote baba na mama. Huwa wazazi hawa wanawekeana zamu wiki moja au mbili kwa baba na nyingine kwa mama. Kama nilivyosema kwenye ile mada iliyopita ya KUOA BILA MAHALI au ile ya mke kuwa na sauti zaidi ndani ya nyumba. Hapa inawezekana kabisa mwanamke akawapa watoto jina lake la ukoo lakini hii inatokea hasa kama hawajafunga ndoa. MAMA AU MKE ANAKUWA NI MUAMUZI

Miaka hii ya karibuni imegundulika ya kwamba kutokana na hili jambo la kuachana achana limeongezeka kwa idadi kubwa. Na kwa mtindo huo watoto wengi wamekuwa na mafanikio /matokea dhaifu shuleni. Wanasema wao wanapata HUZUNI na pia wanapata MSONGO kiasi kwamba wanashindwa kumuda masomo. Ninachotaka kusema ni kwamba watoto katika maisha wanahitaji malezi ya wazazi wote wawili, wakiwa katika nyumba moja. Nyumba yenye amani na upendo. Kwani wazazi wakiwa na FURAHA, WATOTO pia watakuwa na FURAHA pia AMANI.

2 comments:

  1. Hayo maisha ya ndoa huko naona ni ya bandia au artificial.
    Inasikitisha kuona wanaoumia ni watoto.
    Jamani watu mkiingia kwenye ndoa, basi mjiheshimu na kujua kuna sehemu ya uhuru inabidi uugawe aaah

    ReplyDelete
  2. Majuu hamnazo!
    Huwa sijui aliyeianzisha kolamu hiyo kwenye gazeti la nyumbani aliwaza nini.

    Tuache hayo.

    Kwa Ulaya sina hakika mambo ya watoto huwaje kimaadili.

    Huku kwetu nadhani mambo huharibika. Kwangu huwa naumia sana watoto wanapopoteza mwelekeo kisa wazazi wameachana. Kuna wakati kundi hili husababisa watoto wa mitaani.

    Sijui hisia za wengine ni zipi. Hisia zangu huchochewa na hayati Lucky Dube katika Children in the Street. Hasa pale anapomzungumzia mtoto wa mitaani kwa kusema, "His father is being resting in the best place in town.." halafu tena, "His mother is kissing on another man."

    Kwamba wasingekuwa kila mtu kivyake, wale watoto wasingekuwa kitaa.

    Mmh., unanisoma vema?

    Ni hayo tu.!

    ReplyDelete