Friday, May 15, 2009

NGOJA LEO TUTEMBELEE KIJIJI CHA LIULI


Hap ni hospital ya Liuli

Na hapa ni kanisa la Liuli

8 comments:

  1. safi sana, hiyo ni hospital muhimu sana kwa ukanda wa ziwa Nyasa. wamisionari walifanya jambo la maana sana kujenga hiyo hospital pamoja na ile ya Litembo.

    ReplyDelete
  2. Najua na leo nimekumbuka kwani kwa sababu Mpendwa na rafiki yangu bibi aliugulia hapo na kufa miaka minne iliyopita.

    ReplyDelete
  3. Pole sana kwa kumkumbuka bibi yako. ningekuwa na kamuda ningeweza kuandika kuhusu imani za babu zetu wa kingoni kuhusu maisha baada ya kifo, lakini mhh haya majukumu yananikaba sana na hii habari ni ndefu. ila kama unafahamu imani yao ilikuwa vipi kuhusu maisha baada ya kifo (kabla ya kuja hizi dini za kigeni) basi unaweza kuandika kwa faida ya wasomaji wako wapendwa.

    ReplyDelete
  4. Mie sijawahi fika huko. Lakini inaonekana ni Hospitali nzuri na muhimu kwa Maisha ya Wakaazi wa Eneo hilo. Umefanya vema kutuonesha.

    ReplyDelete
  5. Asante kwa kumbukumbu nzuri Da Yasinta. Na pia Anon nashukuru kwa usemayo. Na kama alivyosema hapo huyo Anon, ninakuwa mmoja wa ambao wangefurahia kujua hizo imani zao za maisha baada ya kifo. Hizi imani zilikuwepo na zinaonekana kupuuzwa hivi sasa. Ndugu zangu Shaban Kaluse na Kamala wamekuwa wakizieleza saana na ukiwa makini kuzihusisha na maisha yetu, utaona uhusiano wa karibu na wa ndani uliopo kati ya imani hizo na maisha tuliyokuwa na tunayoishi na kizuri zaidi (labda niseme kibaya) utagundua namna zisivyotofautiana na hizi za "kisasa" ambazo zimeonekana kutaka KUZIPUMBAZA hizo ziliokuwa na ambazo zinaifaa jamii yetu.
    Ijumaa njema

    ReplyDelete
  6. Hapo imekosekana shule tu kama unafuatilia gia za mmishenari wa kikristo akiingia sehemu.

    Ataanza na Kanisa, hospitali, halafu shule , na ukishanogewanavyo atadai umestaarabika.

    Ni wazo tu!

    ReplyDelete
  7. Mkuu Kituturu, shule ipo hapo, kuna ya msingi na sekondari inaitwa St. Paul's,

    ReplyDelete
  8. Naona wameamua kutumia hilo L/cruiser hard top a.k.a mkonga maana kwa hali za barabara zetu wakati wa mvua inakuwa ni kasheshe.
    Hongereni kwa kuwa na huduma hizi muhimu kwa jamii karibu nanyi maana kuna sehemu Tanganyika hii ukienda hata dawa za malaria tu kuzipata inakuwa kazi

    ReplyDelete