Huu mchezo unafikirisha saana. Unafikirisha kwa kutaka ujue ukianzia wapi utaishia wapi na itakupa nafasi ya "kusafiri" mizunguko mingapi na mizunguko hiyo itakufanya "ule" mara ngapi na mwishoni waweza "kulala" wapi na hiyo itampa nafasi gani mpinzani wako katika uchezaji wake. Ni mchezo mzuri ukichezwa kwa kiasi. Naamini ndio maana Prof Matondo akaita njia bora ya kufunbza hesabu. Ijumaa njema Dada
Kweli Mzee wa changamoto umesema kweli, mchezo huu unahitaji mahesabu makali.
Mchezo huu umenikumbusha mbali kwani sisi hatukuwa na vifaa maalumu vya kucheza mchezo huo.Tulikuwa tunachimba vishimo vidogo chini na kisha tunatumia ndulele(ngogwe chungu) sijui wengine wanaziitaje.Nimemkumbuka jamaa mmoja ambaye alikuwa akitufunga sana kwenye mchezo huu.
Huu mchezo unafikirisha saana. Unafikirisha kwa kutaka ujue ukianzia wapi utaishia wapi na itakupa nafasi ya "kusafiri" mizunguko mingapi na mizunguko hiyo itakufanya "ule" mara ngapi na mwishoni waweza "kulala" wapi na hiyo itampa nafasi gani mpinzani wako katika uchezaji wake.
ReplyDeleteNi mchezo mzuri ukichezwa kwa kiasi.
Naamini ndio maana Prof Matondo akaita njia bora ya kufunbza hesabu.
Ijumaa njema Dada
Kweli Mzee wa changamoto umesema kweli, mchezo huu unahitaji mahesabu makali.
ReplyDeleteMchezo huu umenikumbusha mbali kwani sisi hatukuwa na vifaa maalumu vya kucheza mchezo huo.Tulikuwa tunachimba vishimo vidogo chini na kisha tunatumia ndulele(ngogwe chungu) sijui wengine wanaziitaje.Nimemkumbuka jamaa mmoja ambaye alikuwa akitufunga sana kwenye mchezo huu.