Sunday, April 26, 2009

BINADAMU NA MAZINGIRA:- INAPENDEZA WATU KUWA NA MALENGO KATIKA MAISHA

Bila shaka haijawahi kutokea mtuakapanda garimoshi au ndege bila kujua anakwenda wapi na kwa nini anakwenda huko. Lakini kwenye maisha ndivyo ilivyo kwa wengi. Wengi wamepanda garimoshi la maisha lakini hawajui wanaelekea wapi na kwa nini?

Hivi sasa vijana wengi ambao wanalalamika kwamba hawana ajira au hwana la kufanya, watu wengi ambao wanalalamika kwamba mambo yao au kila jambo wanalofanya linakataa, wanakabiliwa na tatizo hili. Wengi wamepanda garimoshi la maisha lakini hawajui hasa wanakwenda wapi.
Kwenye maisha hakuna tofauti. Mtu ambaye hajui hasa anataka kufanya nini au anataka kuwa nani maishani, hawezi hata siku moja kutulia na kupata mafanikio. Bila shaka atakuwa ni mtu wa kuhangaika kwa kufuata harufu au uzuri bila kujua kwamba hivyo sivyo anavyovitaka.

Mahangaiko hususani shughuli:- Kuna wengi sana miongoni mwetu ambao hufanya shughuli hii kidogo na kuiacha na kurudia ten hii hadi wanazeeka na kufa. Kuna watu ambao wana vipaji na ujuzi wa mambo fulani, lakini watu hawa ni kama vipepeo, wanatua ua hili na huruka tena kwenda ua lile na tena na tena. Kwa nini? Ni kwa sababu hawajaamua mahali pa kwenda, ingawa wako kwenye garimoshi wanasafiri. Kwa sababu tu wana ujuzi au vipaji wanadhani na kuamini kwamba hawapaswi kujiuliza wanataka nini maishani na wanaelekea wapi hasa.

Kila binadamu anatakiwa ajue anakoelekea, ajue anataka kuwa nani. Kwa mtu kujua anataka kwenda wapi au anataka kuwa nani, anajiweka kwenye nafasi ya kuwa na malengo na mipango maishani.Malengo na mipango hiyo ndiyo ambayo inaweza kumsaidia kuwa na dira.

Kama ilivyo kwenye garimoshi. Abiria anayejua kwamba anakwenda mahali fulani hata kama garimoshi litafia njiani, hatakwama kwani anajua safari yake ni ya kwenda mahali maalum, hayo yote ni matatizo ya safari. Lakini yule asiyejua anakoenda anaweza kudandia garimoshi lolote na kushuka popote. Kwa kushindwa kwetu kujua hasa tunakwenda wapi tunataka kuwa nani ndiyo unakuta mtu anafanya shughuli fulani, akitetereka kidogo anaiacha na kuanza nyingine ambayo wala haijui vizuri na wala hajawahi kuifikiria. Akikwama kigogo anakata tamaa na kuacha na kuingia kwenye shughuli nyingine ngumu zaidi.

Kutokujua tunataka nini maishani na tunataka kuwa nani ndiyo maana tunajikuta tunahama na kubadili shughuli kila siku na bado miaka nenda rudi tuko palepale. Kwa sababu hatuja mipango na malengo kuhusu uamuzi wa kile tunachokifanya, tunakuwa ni watu wa kubahatisha maisha tu.

Utakutaa mtu ana genge mahali, lakini hajui kama anataka kuwa na genge kwa sababu kichwani mwake anataka kila kitu. Akiona watu wanapata fedha kwenye biashara ya kuchoma mahindi anaacha genge na kwenda huko. Kesho akiona watu wanauza korosho na wanapata fedha, anaacha kuchoma mahindi na kuhamia huko. Anakuwa ni mtu wa kubahatisha maisha. Unaweza kuhusisha mifano mingi ya aina hii ambayo inatokea katika jamii tunamoishi, iwe katika familia, utawa na hata vyuoni, mtu anabadili masomo ghafla bila maandalizi ya kina.

Kufanya uamuzi ni muhimu:- Maisha hayaendi hiyo na hata siku moja haijatokea mtu asiyejua anataka nini maishani kufanikiwa au kutulia. Kama mtu ameamua kufanya biashara ya genge anashauriwa kuishikilia biashara hiyo na kuipangia mipango yote ya kuikuza. Kama wewe umeamua kusoma masomo fulani au kufanya kazi aina fulani, basi zingatia hilo wala usiyumbe. Kila siku huwa tunasikia watu wakisema “yule jamaa alianza kuuza ndizi na nyanya tu, sasa ametajirika ana maduka ya vyakula mji mzima”. Au utasikia wakisema “yuke jamaa alianza masomo yake kwa njia ya posta tu lakini sasa yuko chuo kikuu” Huwa tunatamka sana kauli hizi lakini bila shaka hatujawahi kujiuliza inakuwaje hadi mtu kama huyu kufikia juu kiasi hicho kutokea chini chini chini sana ambako kunadhalauliwa.

Tukianza kujiuliza tutajua kwamba sababu kubwa ni mipangi inayotokana na kujua kwao wanataka kitu gani maishani mwao. Kwa sababu wanajua wanakokwenda na wanachokitafuta, hata mambo yakienda kombo watangángánia tu kwenye shughuli zao. Wale wasiojua wapokwenda ndiyo ambao wakiyumba kidogo tu huacha kile wakifanyacho na kukimbilia kingine.

Ebu muulize jirani yako:- Hapo ulipo, wakati ukiyasoma makala haya kama kuna mtu unayemfahamu muulize anataka kuwa nani au kwenda wapi kwenye maisha yake? Ni lazima atakuambia, “mahali popote mambo yakikubali naenda...”
Mtu unatakiwa kuwa na malengo kwenye maisha hata kama malengo hayo yatafikiwa baada ya miaka kumi. Kwa kuwa ni malengo ndiyo ambapo utaweza kwanza kutulia na baadaye kufika kule unakokutaka.

Bila shaka unajua wengi ambao wamejaribu kila kitu kuanzia kulima mchicha, biashara ya magari, uongozi hadi uuzaji wa madawa ya kulevya, na bado wanahangaika. Haiwezekanai wakatulia kwa sababu ndivyo ilivyo, hawajui wanakoelekea maishani, ingawa wako safarini. Je?, wewe msomaji wangu unajua ukoelekea maishani?

7 comments:

  1. Asante sana Yasinta, umesema vema sana, ni muhimu kuwa na malengo na kusimama katika kile tunachoamua kukifanya.

    ReplyDelete
  2. Duh! mi mbona naona kama gari moshi langu linaenda taratibu sana kiasi kwamba ninakoenda nitachelewa, je kama lipo la haraka na linaenda huko huko si ninabadilisha tu na kupanda lingine au nikatumia usafiri mwingine kufika ninakotaka ambako ni MAISHA BORA.

    Mimi kwa mawazo yangu ni kwamba tusife moyo kwenye maisha madhali unaweka juhudi, kujituma, maarifa na uvumilivu, lakini pia kuna ubunifu kama unafanya mambo yako binafsi kama mimi pamoja na ujuzi ukiwemo wa darasani na wamazingira halisi (under field conditions) pia ikiwezekana uwe na ujuzi zaidi ya mmoja (mult-skilled)

    ReplyDelete
  3. Kaka Bannet,angalia haraka haraka haina baraka,hilo gari moshi la mwendo kasi wapandao ni mafisadi,sasa kaka kama na wewe unatamani kufika haraka haya segerea sio pa kusogelea,hahahhaha! hilo hilo la mwendo wa jongoo utafika tu tena salama kabisa.

    Tufanye kazi kwa bidii tutafika tu huko kwenye maisha bora,hayaji kwa kujibweteka ni juhudi na maarifa.

    ReplyDelete
  4. Hili ni zaidi ya darasa. Kutojua uendako ni tatizo. Lakini pia kuna baya zaidi kuwa watu hata hawajui watokako kwa undani wake. Ina maana usipojua utokako hutaweza kupanga vema uendako na mwisho wa haya ni kugota anakosema Da Yasinta.
    Nashukuru kwa UELIMISHAJI HUU na naamini utatufaa wengi.
    Pamoja daima

    ReplyDelete
  5. Ahsante da Yasinta, umelonga, au kwa maneno mengine umenena!congrats!

    ReplyDelete
  6. Ahsanteni sana wote. Maisha ni safari ndefu. Ambayo ni lazima iwe na lengo.

    ReplyDelete
  7. However, remember this advice: Do not make the topic too broad; for example, if you decide to write about global warming, don't try to discuss each and every aspect of global warming, which would turn your paper into a book, but, instead, choose a focus this manageable and, therefore, can be discussed adequately in a student paper. A meal plan can be very detailed and it can be tied to eating great things like fish and nuts to eat. Eating based on your mood is not the path to healthy weight gain.

    Here is my blog - how to gain weight naturally for women

    ReplyDelete