Sunday, November 30, 2008

SALA YA MKE KUMWOMBEA MUMEWE

Napenda kufunga mwezi huu wa kumi na moja kwa sala hii;-

Ee Bwana , ni ajabu,
Jinsi fikra zangu zinavyomrudia kila mara
Huyu, mume wangu,
Mwenzi anayeshiriki maisha yangu kwa namna ya pekee.
Ninapofagia nyumba na mazingira yake,
Nataka kutengeneza nyumba nzuri kwa ajili yake.
Ninapopika chakula vizuri,
Napenda kumfurahisha.
Ninaponunua nguo mpya na kujaribu kuonekana mrembo,
Ni kwa ajili yake tena, Ee Bwana.

Na ninaweza kukuambia kwamba
Ninamwonea fahari,
Anafanya kazi kwa bidii ili kupata riziki yetu;
Ni mtu mwenye haki, mwadilifu,
Naye hujitahidi kutufurahisha.
Kwangu, yeye ni mpole na mwangalifu.
Hunijali na kuonyesha kweli kwamba anajali.
Hunifanya mimi nijiamini mwenyewe,
Anajua jinsi ya kuondoa hofu zangu,
Hunipatia usalama na upendo ambao nahitaji sana.

Ee Bwana, ninakuomba,
Umbariki na umlinde.
Katika safari zake, umfikishe salama.
Kazini mwake, umpe fanaka
N hapa, nyumbani petu naomba apate amani na heri.

Bwana, unisaidie mimi pia
Niweze kuwa yule mke anayehitaji.
Unifanye niwe mtu anayeweza kumwamini daima,
Mwanamke ambaye anaweza kumfurahia,
Niweze kumsaidia asahau matatizo yake,
Niweze kuondolea mbali hofu zake na kupunguza uchungu wake.

Bwana, Wewe ndiwe uliyenipa mume huyu,
Na katika yeye,
Umenipatia sehemu ya nafsi yako mwenyewe.
Ninakusifu kwa ajili yake, Ee Bwana.


Napenda kuwatakieni wote Jumapili Njema.

10 comments:

  1. Dada Yasinta,
    Mawazo yako huwa nayaheshimu siku zote, lakini hili la leo ni zaidi ya yote. Ingekuwa nguo labda ningesema XXXXXL.
    Hii si tu ni sala ya kufunga mwezi, mi nadhani hii ni funga mwaka.
    Ni kitu kinachozidi kuwa nadra kila uchao. Hasa katika kizazi hiki cha so busy kwa kila mtu. Kizazi ambacho familia nyingi zinaakisi heri mbele ya macho ya wengine kumbe huko majumbani na mahekaluni mwao kila mtu ana chumba chake.
    Kizazi ambacho kutokana na ubize ambao mwingine unapitiliza, mwanamke hakumbuki alimpikia mumewe lini kwa mara ya mwisho. Kizazi ambacho mwanamke humtunishia kifua mumewe na hasa pindi atelezapo katika matendo ama maneno.
    Kizazi ambacho mwanaume haijali tena familia zaidi hutumia muda mwingi baada ya kazi kustarehe na vimada huku familia ikikosa hata pesa ya chumvi.
    Kizazi ambacho mwanaume ameshasahau hata umuhimu wa busu la upendo kwa mke wake.
    Hii sala kwa hakika imejaa upendo wa hali ya juu, imejaa utashi mzuri wa kifamilia. Si tu kwa wanawake. Wanaume pia tujifunze kuwaombea wanawake.
    Nina hakika, mwanamke mwenye imani kama hii, ndoa yake huwa na furaha na mafanikio daima.
    Nami namwomba Mungu nitakapopata mke, anijalie mwenye hekima, upendo na ucha Mungu, awe mwenye kuniombea daima.
    Mungu akubariki sana da Yasinta kwa kukumbuka kutoa sala hii.
    Ahsante sana.

    ReplyDelete
  2. Ahsante sana kwa sala nzuri dada Yasinta,
    Ukweli ni kwamba yale niliyotaka kusema bwana Mtanga amenisemea, kwa hiyo sina cha kuongeza.
    Mungu akubariki sana uwe na ndoa imara isiyotetereka.

    ReplyDelete
  3. Asante sana Fadhy Mtanga nina imani kabisa utapata mke mwema ambaye ataweza kukuombea. Na kweli sio wanawake tu wawaombee waaume zao. Inabidi iwe kinyume pia.Mungu akubariki nawe pia.

    Shaban nawe asante sana kwa maoni yako mungu akubariki pia.

    ReplyDelete
  4. sasa huyo mume wako (bwana wako) ni bwana harafu unamuombea kwa bwana, ohhh my God!

    ndio maana wakatoliki wanawaombea waume zao kwa bikra maria (simaanishi maombi mengine bali sara ya kweli)

    huwa siku zote naushangaa mwili wa kiumbe anayeitwa mwanamke. mwili wa kiumbe huyu ni waajabu japo biblia inautupilia mbali.

    biblia inaamini mwanamke alitoka ubavuni mwa mwanaume wakati uhalisia ni kwamba sote kwa kupitia nyeti za mwanamke hutukea tumboni mwa mwanamke. kwa maneno mengine mwanamke anamwili waajabu. mwili unaofyatua miili mingine na kuilisha, oh my God, kwa nini biblia hailitambui hili na kudai mwanamke alitoka kwa mwanamume?

    i love women

    ReplyDelete
  5. Nimegundua utamu jamani mimi ni ndugu nha yule mnyasa hapo kwenye blogu ananifundisha nianze kublogu, ngoja nitajaribu. Lakini kaka Kalama umezoea kuandika katika jifahamu nakusoma sana pale,

    nimeonyeshwa na mnyasa huyu Markus,

    mimi
    MAPAMBANO

    ReplyDelete
  6. Asante sana kwa sala nzuri kwa mumeo pia naamini ni changamoto kwa sisi wanaume kuwaombea wake zetu pia.

    Napenda kumtoa wasiwasi ndugu yangu Kamala kwa madai yake kwamba Biblia haipo wazi kuhusu mwanamke, nahisi huwa hasomi vizuri biblia maana huwezi kutenganisha Biblia na Mungu.
    Pia maelezo yako yanajichanganya unaposema kiumbe mwanamke ameumbwa kwa ajabu sana na Biblia haipo wazi na inakuchanganya inaposema mwanamke alitoka kwa ubavu wa mwanaume.
    Ukweli ni kwamba biblia imeeleza wazi kwamba mwanamke ameumbwa na mwili wa ajabu ili wewe mwanaume uridhike nao na hii inatokana na kwanza baba yetu Adamu kutoridhika na upweke pale katika bustani ya Edeni.
    Soma Bibilia kitabu cha Mwanzo sura ya kwanza na ya pili ndo utajua biblia inamsifia na kumpa nafasi namna gani kiumbe mwanamke.
    Ni kweli biblia inakubali kwamba mwanamke alitoka kwa ubavu wa mwanamke hakuna cha ajabu hapo hata kama kila mtu duniani sasa anazaliwa na mwanamke na hii hawezi kufanya Mungu na Biblia vikuchanganye.

    Upendo daima!

    ReplyDelete
  7. Hii sala si kwa ajili ya mimi kumwombea mume wangu tu ni kwa ajili ya wanawake wote waliolewa kuwaombea waume zao kwa sala hii au kwa mfano wa sala hii. Asanteni sana wote kwa maoni/mawazo yenu mazuri karibuni tena na tena.

    ReplyDelete
  8. hello, how's everybody here? I'm a newcomer to this community forum. Hope to obtain new pals and discover some thing here.

    ReplyDelete
  9. If you call to mind me I cried as I mastered Internet addiction, but what I wrote. I need start at tenure expos‚ a iota usual me to indulge known settled aspects of my person so far:
    - Since renowned boarding-school, being an introverted origin, the complex of their own sexuality (like most teenagers), I started to superintend movies and amorous magazines. It was not hanker and I started and masturbate. After I entered college, I met people from [url=http://seexzer.com]PORNO[/url], where I also enrolled myself integrating lickety-split between them. In pilgrimages made with them, I had the chance to straighten absent from varying monks at several convents and monasteries in the country.
    - When I confessed with a scrutiny the supreme in days of yore upon a time, ungainly after I renounce smoking in the same urgent and masturbated. It was wholly easy. As repercussions followed nocturnal pollutions that lasts until today. I watch live [url=http://seexzer.com]streaming[/url] sometimes. As I demand, I am shot of, not terminate (it is known malaise which care see the pollutions).
    - In appropriate of almost two years rational virtually monasticism. More specifically, I exposition power the monastic life. But arcane, I codify a unwavering elevated of agitation.
    - Returning to the Internet, I can rephrase that it has complete into a passion, because I looked and I looked at "inelegant". Although I tempo after space confessed, I persist to replication this sin. We started sooner than looking at me all sorts of unsophistication, but I got gracious to dribble at full speed and I went to eroticism more "artistic." I started my sensuality and court such is not unquestionably, are cognizant of it. At the wink of an design gather me anything, in Freudian argot, ditty potency report that this leads to an bourgeon in libido.
    Another mess is: up best I consider of, in my captain I can on, or debar myself and not watchful of, or keep only's eyes unrestricted on account of and fulfil my flesh. Why in Creator and pass more than those moments and all? Why do all bodily appetites? I bondslave and I do not like. In the meantime, looking at all these bitches cogitate on that recognizable, so living in devilry, and I can not jet plane good.
    I'm wearying of of endlessly repeating the sin. I'm starting to trim short me when I the unfinished of that can not face. I started excogitative of choosing to wilderness the monastic living, following the awareness that it's ourselves to all in the planet and I on the other side of the charterhouse, but to be in the charterhouse and to assume of the world. I set up to end a college and I'll conclusion, but at bowl impertinent are extraordinarily confused. On identical clutches, my cohort struggles passion (nocturnal pollutions and that I look at pictures and risqu‚ movies), on the other in collusion, dispute with all my thoughts that come.
    Any longer I am consummately baffling, I do not clutches what to arbiter elegantiarum plan and what to do. O how can I reside a confessor. But here is a problem. Tastefulness was unambiguous talking to confession, and I'd like to talk to me more, leisurely, to aver all they do and the whole shooting betrothal I feel.
    If you wish in requital for and you can avoid me with something, it entertainment be socialistic grateful. Just watch [url=http://seexzer.com]streaming[/url]

    ReplyDelete