Sunday, November 16, 2008

AMRI KUMI ZA MUNGU

Leo ni jumapili nimeamka na nimeona afadhali nimkumbuke mungu kwa kuzikumbuka hizi amri.

1. Usiwe na miungu mingine ila mimi.

2. Usijifanyie sanamu ya kuchongo.

3. Usilitaje bure jina la BWANA , Mungu wako.

4. Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.

5. Waheshimu baba yako na mama yako upate heri na miaka mingi duniani

6. Usiue

7. Usizini

8. Usiibe

9. Usimshuhudie jirani yako uongo

10. Usitamani chochote alicho nacho jirani yako.

Je? Kwa mtazamo wako hizi amri zinatekelezwa kweli?

2 comments:

  1. Asante kwa AMRI HIZO.
    Ukweli ni kuwa zatekelezwa lakini si kwa usahihi. Kama ambavyo nimeshawahi kkauandika kuwa uwiano wa Amri hizo ni 3 kwa 7. Yaani 3 zatuhusu sisi na MUNGU wetu moja kwa moja na 7 zatuhusu sisi na wale tuishio nao. Yaonesha wengi wanashikilia zile 3 na kuacha 7. Yaani wanaweza kumpita mwenye uhitaji, kufanya tamaa, kusengenya na hata kuwaza uzinzi wakiwa wanaelekea kwenye KUIKUMBUKA SIKU YA BWANA (Kanisani). Hiyo nadhani ni kutotekeleza amri. Kutosaidia wenye shida kwa kuwa muda wa ibada umekaribia ni kutotimiza amri pia.
    Pengine tukumbuke kuwa kushinda mtihani wa amri 10 za Mungu lazima tuangalie uwiano na kwa kuwa 70% ni sisi na jamii tuishiyo nayo ni lazima kuijali pia. Lakini tusisahau 30% ituhusuyo sisi na Mungu.

    ReplyDelete