Saturday, August 16, 2008

Agosti 16, 2008 KAMBI ZA AFRIKA KUSINI




Zaidi ya watu 60 waliuawa kutokana na ghasia dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini
Maafisa wa serikali ya Afrika Kusini wameamua kuongeza muda zaidi hadi Jumatatu, kabla ya kutoa amri ya kufungwa kwa kambi sita ambazo ziliwapokea wakimbizi nchini humo, kufuatia ghasia dhidi ya wageni mwezi Mei.
Muda huo utatoa nafasi kwa mahakama ya katiba kupata nafasi zaidi, kabla ya kutoa uamuzi wake, baada ya makundi ya kutetea haki za binadamu kupinga hatua ya kutaka kuzifunga kambi hizo.
Mamlaka ya serikali katika mkoa wa Gauteng inaeleza kwamba ni salama sasa kwa wageni kuweza kurudi katika makazi yao.
Kambi hizo zilianzishwa mwezi Mei, baada ya zaidi ya watu 60 kuawa, na maelfu kupoteza makao yao, kufuatia ghasia dhidi ya wageni.
Mapema wiki hii, jaji mmoja wa mahakama kuu alikataa rufaa kutoka kwa makundi yanayotetea haki za binadamu, ambayo yanasema kwamba kuzifunga kambi hizo ni kuwanyima haki wakimbizi wanaoishi humo.
Awali mahakama ya katiba ilikuwa inatazamiwa kutoa uamuzi Ijumaa.
Ghasia hizo dhidi ya wageni ndizo zilizokuwa mbaya tangu siku za uongozi wa ubaguzi wa rangi uliokomeshwa mwaka 1994.
Zilianza katika mtaa mmoja kaskazini mwa Johannesburg, na kuenea kote nchini.
Walioshambuliwa walilaumiwa kwa kuchangia katika ukosefu wa ajira na kuzidi kwa uhalifu nchini humo.
Raia 21 wa Afrika Kusini ni kati ya wale waliouawa, baada ya kudhaniwa kwamba walikuwa ni wageni.

3 comments:

  1. Kwa nini jamani acheni fujo tuwe na amani.

    ReplyDelete
  2. [url=http://kfarbair.com][img]http://www.kfarbair.com/_images/logo.png[/img][/url]

    בית מלון [url=http://www.kfarbair.com]כפר בעיר[/url] - אווירה כפרית, [url=http://www.kfarbair.com/about.html]חדרים[/url] מרווחים, שירות חדרים, אינטימיות, שלווה, [url=http://kfarbair.com/services.html]שקט[/url] . אנחנו מספקים שירותי אירוח מגוונים גם ישנו במקום שירות חדרים המכיל [url=http://www.kfarbair.com/eng/index.html]סעודות רומנטיות[/url] במחירים מיוחדים אשר מוגשות ישירות לחדרכם!

    לפרטים נוספים אנא לפנות לאתר האינטרנט שלנו - [url=http://kfarbair.com]כפר בעיר[/url] [url=http://www.kfarbair.com/contact.html][img]http://www.kfarbair.com/_images/apixel.gif[/img][/url]

    ReplyDelete
  3. Hi,

    I begin on internet with a directory

    ReplyDelete