Watanzania kwa kweli tuna haki ya kujivunia nchi yetu nzuri yenye amani na utulivu. Halafu sasa kitu kinachonifurahisha ni kwamba Tanzania haina utajiri wa mbuga za wanyama tu na mlima wetu mrefu Kilimanjaro ambavyo watalii huja kuangalia. Hapana, Tanzania ni tajiri wa lugha mnajua hakuna nchi yenye makabila mengi kama TZ. Makabila 129(130) ambayo ni machache tu huwa wanaelewana wanapoongea, kama vile Wangoni na Wamanda, Wabena na wahehe nk. Hii ndiyo maana Hayati baba wa Taifa Mwl. J.K Nyerere aliona ni vema kuwe na lugha moja ambayo watu wote tutaweza kuongea na kuelewana ni lugha ya Taifa KISWAHILI.
Naipenda sana nchi yangu Tanzania nipo tayari kufa kwa ajili ya nchi yangu.
ReplyDelete