Wednesday, June 18, 2008

JUNI 18,2008 MIDSUMMER EVE






















Sasa nadhani mtashangaa na kusema ametuletea nini sasa sawa ngoja niwaambie:- Imekuwa ni mila na desturi hapa Sweden. Yaani wakati huu ni katikati kabisa ya mwaka: Na siku hii hapa watu wanasema hivi uchume maua na uweke chini ya mto kisha ulala na usiku ule utaota nani atakuwa mchumba wako. sasa ngoja nikuambia chakula kinacholiwa siku hii, ni samaki wabichi yaani waiopikwa au kuchomwa. Samaki wabichi ambao wamewekwa kwenye maji na viungo maalum kama mwaka hivi. Bila kusahau viazi mviringo (matosani) vya kushemsha na vyakula vingine vingi. Na halafu siku hii watu wanakunywa sana pombe na hasa pombe kali, na pia nisisahau kunakuwa midsummerdance kama mnavyoona katika picha, wanatengeneza (msalaba) huuu kwa majani na maua kidogo. Maana ya huu msalaba kwa lugha ya hapa unaitwa (STÃ…NG) nitakuelezeni siku nyingine.Baadaya kupeleleza nimeambiwa sababu kubwa ya kuadhimisha au nisema kukumbuka mila hii ni kuwaomba miungu ili mazao (mavuno ) yapatikane kwa wingi . Lakini cha kushangaza ni kwamba wao(waswidi) hawaamini kuna mungu Je? sasa watapataje mazao mengi kama hawaamini? Wanasema hata kama hawaamini lakini hii siku ni safi kwani wanakula chakula na kingi na kunywa mpaka kulewa. Sijui wasomaji mmeelewa kama hamjaelewa basi nitadadisi na kuwaeleza kwa kirefu zaidi siku nyingine.


Na ; Yasinta Ngonyani

No comments:

Post a Comment