Sijui mngekuwa wenzangu mngesema /fanya nini? Ni hivi kuna rafiki yangu mmoja ameniomba msaada/ ushauri ya kuwa katika familia yake hakuna mawasiliano. Kila mmoja anafanya kama anavyotaka. Na hivi leo ninavyosema ameniambia amepatwa na mshtuko kusikia kanisani wanatangaza tangazo la kwanaza la ndoa kati ya baba yake na mwanamke ambaye hajapokelewa katika familia. Labda, sijasema tangia mwanzo huyu rafiki yangu mama yake mzazi alishafariki na sasa baba yake anataka kufunga ndoa na mwanamke mwingine baada ya miaka mitatu tu na huyu mwanamke hajakubalika na watoto wa huyu baba. Je? ungekuwa /mngekuwa wewe /ninyi u/mngemshaurije ili nimpe jibu huyu rafiki yangu?
Na; Yasinta Ngonyani
Nianze na mfano huu; katika familia yetu tupo 9 kati yao hao hatujazaliwa katika mama mmoja.Watoto watano tumezaliwa kwa mama wa pili na wanne wamezaliwa katika mama wa kwanza.Sababu baab yetu alipofiwa na mkewe yaani mama wa ndugu zangu,alimwachia watoto wanne.Baadaye akaenda kusoma kwa miezi kama sita hivi,lakini alimuomba mfanyakazi mwenzie ambaye ni mama yetu sasa amtunzie watoto wake wanne mpaka atakaporejea.ikaw hivyo.baada ya miezi kadhaa baba yetu akarejea nyumbani na kuwakuta watoto wake wapo katika hali nzuri tu.Mwishowe aliibuka na wazo la kumwoa mama yetu shauri amemtunzia watoto wake vizuri,lakini awali mama yetu alikataa wazo hilo.Matokeo yake ni kwamba hadi leo hii ameoana na mama yetu na kubapa watoto watano ukijumlisha na wale wanne inakuwa tisa.Baba yetu alioa mke mwingine baada ya yule wa awali kufariki lakini alikaa kwa muda wa mwaka mmoja tu tokana na kazi alizokuwa kaifanya kulazimu kuacha mtu wa kulea watoto.Kimsingi wattoto aliowakuta mama yetu aliwalea kama kazaa mwenyewe na hadi kushriki katika kuwasomesha na leo hii wanajivunia huyo kama mama yao mzazi.Nasi tulizaliwa na mama huyu wa pili tunaishi kwa amani na ndugu zetu kwani wao licha ya kuelewa kwamba mama yao alikufa lakini walikutwa wakiwa wadogo nawamelelewa na mama yetu wanajikuta hawana huzuni kwani wanafurahi kama wapo na mama yao mzazi.
ReplyDeleteJambo kuu katika familia ni maelewano,upendo,hekima,heshima na imani.Hata kama baba anapenda kuoa lakini lazima awasikilize watoto wake wanachosema kwani inawezekana kabisa mama huyo akaja kuishi kwa kinyongo kwani anajua watoto hawataki.Hii itaadhiri sana maelewano ya familia na kugombana ndugu.Baba atambue kwamba watoto wake kwa sasa wananafasi kubwa sana katika maamuzi yake kwani nia yao siyo kugombana na mama bali kujenga familia iliyo bora bila kujali utofauti.Hata kama yeye ndiye mwenye maamuzi lakini anapaswa kuelewa lengo la watoto wake kukataa siyo kwamba wanataka kuleta ugomvi bali maelewano yao kama familia moja bila kujali mama yao kuwazaa au kutowazaa.Naomba sna baba asikilize watoto wake wanataka nini kwani lengo lao siyo ugomvi katika familia bali upendo na mshikamano daima