tag:blogger.com,1999:blog-3332600689383679139.post2478695351021233014..comments2024-03-22T07:21:43.203+01:00Comments on MAISHA NA MAFANIKIO: Yasinta Ngonyanihttp://www.blogger.com/profile/09314172793959023532noreply@blogger.comBlogger3125tag:blogger.com,1999:blog-3332600689383679139.post-80165148182347543952012-02-17T11:15:00.890+01:002012-02-17T11:15:00.890+01:00Ahsante Ray kwa mchango wako...mafundisho haya.Ahsante Ray kwa mchango wako...mafundisho haya.Yasinta Ngonyanihttps://www.blogger.com/profile/09314172793959023532noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3332600689383679139.post-82720511739661900892012-02-16T08:25:46.112+01:002012-02-16T08:25:46.112+01:00Kwa hivyo kosa la kufanya ngono nje ya ndoa inawez...Kwa hivyo kosa la kufanya ngono nje ya ndoa inaweza kuwa sababu mwafaka ya talaka iwapo mwathirika ataona ni vema kufanya hivyo.ray njauhttps://www.blogger.com/profile/17305304044159231575noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3332600689383679139.post-42406845875899317642012-02-15T17:07:29.920+01:002012-02-15T17:07:29.920+01:00Kwanza ni muhimu kukumbuka maneno ya biblia katika...Kwanza ni muhimu kukumbuka maneno ya biblia katika malaki 2:16a: “ nachukia talaka, asema Bwana Mungu wa Israeli,” kulengana na biblia,mpango wa Mungu juu ya ndoa ni iwe ushikamano wa siku zote za mwanadamu duniani. “ Hata si wawili tena bali mmoja. Kwa hivyo kile Mungu amekiunganisha mwanadamu asikitenganishe” (mathayo 19:6). Mungu antambua ya kwamba kwa kuwa ndoa ni ya wenye dhambi wawili, talaka haina budi kutokea. Katika agano la kale aliweka shaeria za kulinda haki za watalaka hasa wanawake (kumbukumbu la torati 24:1-4). Yesu akasema sheria hizi zilitolewa kwa sababu ya ugumu wa mioyo ya wanadamu lakini hayakuwa mapenzi ya Mungu (Mathayo 19:8).<br /><br />Utofauti wa maoni juu ya talaka na kuoa tena unatokana na maneno ya Yesu katika Mathayo 5:32 na 19:9. “isipokuwa kwa habari za uasherati” ndicho kipengele peke yake ambacho Mungu anatoa ruhusa ya talaka na kuoa tena katika maandiko. Wengi hutafsiri maneno haya kuwa ni kile kitendo cha zinaa kinachofanyika baada ya kuolewa. Katika mila na desturi za wayahudi mke na mme walihesabiwa kuwa wameoana toka wakati wa kuposwa kwa msichana. Kitendo cha mapenzi kilichofanyika wakati huu pia kingehesabiwa sababu ya kutosha talaka.<br /><br />Neno la kigiriki lilitafsiriwa kumaanisha uasherati ni neno linaloweza kumaanisha kila aina ya uchafu wa kimapenzi kama zinaa, uasherati, ukahaba na kadhalika. Yesu anathibitisha kuwa talaka inakubalika mahali uchafu huu wa kimapenzi unapotendeka. Kitendo cha ngono ni cha umuhimu mkubwa katika ndoa “nao wawili watakuwa mwili mmoja” (mwanzo 2:24; Mathayo 19:5; waefeso 5:31). Kwa hivyo kosa la kufanya kitendo hicho nje ya ndoa inaweza kuwa sababu mwafaka ya talaka. Kama ni hivyo basi pia Yesu alikuwa na hoja ya kuoa tena. Katika kusema “na kuoa mwingine” (Mathayo 19:9) inathibitisha talaka na kuoa tena vinakubalika. Jambo muhimu ni kutambua ya kwamba ni wale waathiriwa na hali mbaya ya mapenzi nje ya ndoa pekee wanaokubaliwa kuoa tena. Kukubaliwa huku,ijapokuwa hakukutajwa moja kwa moja katika maandiko, ni huruma ya Mungu kwa yule aliyetendewa dhambi wala si kwa aliyetenda dhambi ya zinaa. Katika maandiko haya hayaelezi kama mwenye kutenda dhambi ya zinaa naye aruhusiwa kuoa au la.ray njauhttps://www.blogger.com/profile/17305304044159231575noreply@blogger.com