Wednesday, May 29, 2019

VYAKULA/MILO AIPENDAYO KAPULYA

Chakula cha asubuhi mayai, soseji na vinginevyo na bila kusahau matunda kama papai, nanasi na  zabibu. Bila kusahau chai(chingambwe) yaani chai isiyo na sukari

Hapa ni samaki mzima mkubwa aliyeokwa kwenye oven na aina nyingine za samaki kama pweza, kamba nk. Karibuni tujumuike wapendwa.
Hapa ni viazi  kwa samaki wa kuchoma/banika  yaani hapa ndo walinikumbusha kwetu LUNDO/NYASA.
PAMOJA DAIMA.

Monday, May 20, 2019

HUU NI UJUMBE WA JUMATATU YA LEO.......

Wakati mwingine unaweza kupata msaada kwa mtu ambaye hukuwahi ku/mtegemea au ulimdharau, hivyo ni kheri kuishi vizuri na kila mtu kwa kuwa hujui kesho yako.....

Friday, May 17, 2019

KWETU RUVUMA NI KUZURI VYAKULA VINGI SANA HASA VYA ASILI....KARIBUNI

Maembe sasa yanaelekea kwisha ila da ni uhondo juu ya uhondo
Hapa ni masuku, matunda pori/asili sisi wangoni huyaita pia MAPOTOPOTO
Na mwisho hapo ni matunda pori/asili nayapenda sana sijui kama yana jina la kiswahili ila sisi wangoni twayaita MADONGA.
PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA HAPA HAPA NA VYAKULA VYA ASILI AU KITU KINGINE....Kapulya wenu.

Wednesday, May 8, 2019

BADO NIPO KWETU RUVUMA NAFAIDI HIVI VYAKULA VYA ASILI

Hapa ni mchanganyika wavyakula nivyopendavyo yaani mahindi ya kuchemsha pamoja na maboga/mapondo na  halafu njugu....
......na hapa ni kikande yaani hiki ndo cha asili kabisa,  hakina radha saa lakini ni kitamu
Na hapa ni kumbikumbi napenda sana kumbikumbi. Na nafurahi kwamba miaka kadhaa ijayo karibu dunia nzima kutakuwa na chakula kama hiki, yaani kumbikumbi, nzige, mende nk. TUKUTANA TENA WIKI IJAYO....KAPULYA WENU.