Monday, February 25, 2019
MLO WANGU WA JIONI YA LEO UTAKUWA HUU NA CHA KUTEREMSHIA NI MAJI...
Karibuni tujumuike ndugu/rafiki zangu ni samaki kwa viazi....Nimekumbuka sana kule nilikozaliwa Nyasa ila kule kwetu kungekuwa na ugali wa muhogo weeeee
Wednesday, February 13, 2019
UJUMBE WA LEO- TOFAUTI BAINA YA SHULE NA MAISHA.....
Shuleni unajifunza somo/masomo na baadaye unapata mtihani. LAKINI- Katika maisha , kuna mitihani ambayo tunajifunza masomo.
PANAPO MAJALIWA , Kapulya wenu!
PANAPO MAJALIWA , Kapulya wenu!
Tuesday, February 12, 2019
KUMBUKUMBU: NI SHAIRI LA SIKU NYINGI SANA NILIIMBA NIKIWA DARASA LA NNE
Nililiimba kipindi niko shule ya msingi ,nakumbuka ni darasa la nne na mpaka leo takribani miaka 30 zaidi bado nalikumbuka. Bila shaka shairi hili litakukumbusha yaliyo mema ya kipindi cha nyuma. Na cha kufurahisa zaidi kitabu hiki ambacho hili shairi lipo ninacho:-)
Monday, February 11, 2019
HIZI ZITAKUWA PICHA ZA MWZI HUU WA PILI
Nimeamka asubuhi ya leo na nikawa na hamu ya kula yai kwa kawaida huwa napenda kula yai moja tu lakini lakini leo macho yangu yakakutana na maajabu haya katika yao moja nikaona ni mawili. Cha ajabu yao halikuwa kubwa kuliko kawaida....nimeyale yote :-) Mara nikakumbuka kuna mtu alinitumia picha ....
...picha maajabu yaliyotokea mgomba mmoja umezaa mikungu minne ya ndizi. Hakika hii ni kali ya mwezi ..