Friday, March 31, 2017

KUMBUKUMBU...VYAKULA NIVIPENDAVYO..MWISHO WA JUMA PIA MWEZI UWE MWEMA....


 Mboga ya maboga...Karibuni nitaanza bustani yangu hii ni kaka yangu kanitumia ili nitamani zaidi:-) na kweli nimetamani sana na mpaka nimepitiliza na kutamani .....
...ugali na mlenda pori..duh! nimekumbuka mbali sana.... kila la kheri na mwisho wa juma mwema  pia mwishi wa mwezi...  

Wednesday, March 29, 2017

NI JUMATANO YA MWISHO NA HILI NI NENO LA LEO JUMATANO HII YA MWISHO WA MWEZI HUU WA TATU...

KUKUMBWA NA CHANGAMOTO ZA MAISHA NI LAZIMA , LAKINI KUSHINDWA NI HIARI YA MTU.
NAWATAKIENI WOTE MTAKAIPOTA HAPA SIKU NJEMA SANA!...Kapulya.

Tuesday, March 28, 2017

JE? UNGEKUWA WEWE UNGEFANYA NINI?

Pale unapotuma pesa nyumbani kwenu  zaidi ya miaka mitano urekebishiwe nyumba yako. Halafu siku ya kurudi unakuta hali kama hii. Je? hapo unafanyaje?
Ndiyo;- Niliwahi kusimuliwa kisa kama hiki na rafiki mmoja yalimpata kama haya. Uaminifu umepotea siku hizi .

Monday, March 27, 2017

NILIBAHATIKA KUWA KWENYE KOZI YA :- FUNCA- ADMNITRATORS IN HAMMARÖ MUNICIPALITY

Funca-administratörer i Hammarö kommun

22 mars 2017
För att förbättra arbetet inom LSS (lagen om stöd och service) på Hammarö har personal och enhetschefer i kommunen blivit utbildade till Funca-administratörer. Funca är ett arbetsverktyg som ska förebygga och minska utmanande beteenden hos vuxna personer med kognitiv nedsättning inom LSS.
Nimejaribu kutafsiri kwa kiswahili toka hapo juu:- Ili kuboresha kazi ya LSS (Sheria juu ya msaada na huduma) katika Hammarö, wafanyakazi na kitengo katika manispaa wamepata mafunzo kwa Funca watawala. Funca ni chombo cha kuzuia na kupunguza tabia zenye changamoto kwa watu wazima na (wenye shida ya mtindio wa akili) kuharibika kwa utambuzi katika LSS.
Funca arbetar för en bättre livskvalitet och ökad självständighet för personer inom LSS och för en minskning av begränsningsåtgärder. Verktyget kommer hjälpa personal att arbeta förebyggande, jobba mot samma mål, ha ett gemensamt språk och hur en person med svåra symtom ska bemötas med siktet inställt på att minska läkemedelsanvändning.
Hammarö kommuns första administratörer är nu utbildade och fler kommer utbildas till hösten. Det kommer att finnas administratörer på alla LSS-enheter i kommunen.
Tafsiri ya kiswahili:- Funca ni kufanya kazi kwa bora wa maisha na kuongezeka kwa uhuru kwa watu katika LSS, na kwa ajili ya kupunguza hatua ya kiwango cha juu. mfumo huu wa utasaidia wafanyakazi kufanya kazi kwa vitendo, kufanya kazi kwa lengo moja, kuwa na lugha ya kawaida na jinsi mtu aliye na dalili kali wanapaswa kutibiwa kwa lengo la kupunguza matumizi ya madawa.
Hawa ni watendaji wa kwanza kwa Hammarö kwa kupata haya mafunzo na wengine zaidi watapewa mafunzo hapo baadaye. Kutakuwa na watendaji wa vitengo vyote vya LSS katika manispaa hii.

Friday, March 24, 2017

HAYA MWISHO WA JUMA NDIO UNAKARIBIA SASA...NA HIZI ZIWE PICHA ZA WIKI HII........

Huyo dada kafunga mstari makande kwa bia...duh! kaaazi kwelikweli. Haya ndugu zanguni muwe na mwisho mwema wa juma kama  ni kwa mtindo huu kama huyo dada au tu
 kwa mtindo huu  na pengine labda....
...kwa mtindo huu .
na labda pia kwa mtindo wa kuwa na familia mkiwa mmetulia nyumbani  baada ya kazi ya wiki nzima. Kwa mtindo wa kuwa pamoja na kusimuliana hadithi mbalimbali na vipi wiki kwa ujula imekuwaje? HAYA KAPULYA WENU ANAWATAKIENI MWISHO MWEMA WA WIKI. TUPO PAMOJA DAIMA. 

Thursday, March 23, 2017

MAISHA:- WATOTO WANAPOCHEZA NDIO HUJIFUNZA MAISHA

Sisi binadamu hujifunza mambo mengi katika michezo...lakini baadhi ya walezi/wazazi huona watoto wachezapo wanapoteza muda na huwakatisha na kutaka wafanye kazi nyingine... WAZAZI/WALEZI TUWAACHE WATOTO WAWE WATOTO......

Tuesday, March 21, 2017

TASWIRA YA WATU NI KAMA MTI WENYE MAJANI,MATAWI NA MIZIZI PIA

Nikiangalia mti napata taswira ya watu wanaotuzunguka katika maisha yetu. Kama ujuavyo mti, huwa kuna majani, matawi na mizizi. Vivyo hivyo watu wanaotuzunguka, wapo ambao ni majani, wapo ambao ni matawi na pia wapo ambao ni mizizi. Kuna watu  wanakuja katika maisha yetu kama majani kwenye  mti. Huwa wapo kwa msimu tu, huwezi kuwategemea muda wote, kwa sababu wao ni dhaifu. Ila wapo kwa ajili ya kutoa kivuli. Hivyo si wakuwapuuza. Kama yalivyo majani kwenye mti wapo kwa ajili ya kunyonya chochote kutoka kwako. Nakufanya wapendeze kisha wachanue maua mazuri. Lakini kuna kipindi cha kiangazi kikifika jua huwa, ni kali na upepo makali wao hunyauka na kupeperushwa na upepo huondoka na kukuacha mpweke. Huwezi kuwalaumu kwa kuwa hivyo ndivyo walivyoumbwa.
Aina ya pili wa watu wanaotuzunguka ni kama matawi kwenye  mti wao huhimili vishindo kuliko majani, watakuwa na wewe katika kipindi kirefu katika maisha yako. Ukipata misikitiko mikali mara mbili au tatu ni rahisi kuwapoteza. Mara nyingi hawa huwa na subira. Lakini hali ikiwa ngumu sasa sana hukuacha mpweke, ingawa wana msikamano kuliko majani. Unatakiwa kuwachambua sana kabla hujawekaeza muda wako mwingi kwao. Lakini, usiwalaumu kwa kuwa hivyo ndivyo walivyoumbwa.
Aina ya tatu ni watu wanaokuja kwako kama mizizi kwenye mti ukiwapata hawa shukuru MUNGU ni vigumu kuwaona au kuwapata huwa hawajionyeshi. Kazi yao ni kushikilia usianguke, uweze kufanikiwa na kuishi maisha yenye afya na furaha tele.  Unapofanikiwa hukutakia mafanikio zaidi, hukaa nyuma ya pazia, na hawatoi nafasi kwa walimwengu kugundua kuwa wapo kwa ajili yako. Ukipata mitikisiko mikali katika maisha yako huvumilia na kuishi na wewe hadi mwisho. Chochote kikikutokea kiwe kibaya au kizuri wao wapo. Kama ulivyo mti una majanai mengi, matawi mengi, lakini mizizi michache sana na ni vigumu kuiona.
Tuangalie maisha yetu kuna matawi na majani mangapi yanayotuzunguka, Na je? kuna mizizi mingapi?  Na swali la mwisho ambalo pia ni muhimu je? wewe ni nani kwa watu wanaokuzunguka?

Monday, March 20, 2017

JUMATATU YA LEO TUENDELEE NA TAMADUNI ZETU ZA ASILI:- HAPA TUNAONA GHALA ZETU ZA ASILI

Hii ni ghala ambalo lilitumika kuhifadhi chakula/nafaka na mpaka leo ghala kama hii bado hutumika katika jamii zetu.

Friday, March 17, 2017

TUDUMISHE UTAMADUNI WETU

 NI NGOMA YA ASILI YA KINGONI KWA JINA LA LIZOMBE(KITOTO)
NA HII PIA NI NGOMA YA SILI YA KINGONI KWA JINA LA LIGIU

Thursday, March 16, 2017

MAKAMU WA RAIS JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AMEWASILI MJINI MBABENE-SWAZILAND

KITAMADUNI HASWAAA
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Mbabene-Swaziland kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika-SADC. Katika mkutano huu Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan anamuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta John Magufuli Katika mkutano huo.
CHANZO: Na Emanuel Amas wa Tasnia ya Habari.

Wednesday, March 15, 2017

MCHEZO WA BAO ENZI HIZO AMBAO LILITUMIKA NA MACHIFU

Hii ni bao ambalo lilitumika na MACHIFU kushindana, kwa mfano wao walikuwa hawapigi kura wakati wanachagua kiongozi wa eneo lao. Ila machifu hao walitumia bao kushindania  madaraka na aliyemfunga mwenzake kete nyingi ndiye aliyetawazwa kuwa CHIFU wa eneo fulani.

Tuesday, March 14, 2017

MAISHA:- BAADA YA KUISHI MIKA 60 SASA WAFUNGA NDOA

Mzee wa miaka 98 aoa bibi  wa miaka 88 baada ya kuishi pamoja muda wa miaka 60 huku wakichunguzana.
WAZO: NIMEPENDA UAMUZI WAO.

Monday, March 13, 2017

Sunday, March 12, 2017

NAPENDA KUWATAKIENI JUMAPILI NJEMA WOTE ...

"Msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake" WAFILIPI 2:3....
JUMAPILI NJEMA  BARAKA ZA BWANA NA ZITAWALE NYUMBANI MWENU.

Friday, March 10, 2017

PALE WATU WAZIMA WANAPOKUMBUKA NYIMBO ZA UTOTONI ..NIMEPENDA SANA HII


Ndugu zanguni wapendwa hizi nyimbo ni hazina yabidi tuzihifadhi na pia tuwafundishe wanetu. Yaani laeo nimekumbuka sana enzi za utoto wangu...kama sio chekechea basi shule ya msingi na kama sio huko basi usiku wa mbalawezi.. IJUMAA NJEMA NA PIA MWISHO MWISHO WA JUMA UWE MWEMA SANA KWA WOTE MLIOPITA HAPA.....NI KAPULYA WENU:-)

Thursday, March 9, 2017

MNAKUMBUKA HII?

Mimi nakumbuka sana.....wazazi wanaondoka kwenda shamba nawe unaachiwa wadogo zako uwatunze na papo hapo labda kuchochea maharege. Nakumbuka siku moja niliunguza maharage, ila hata hivi niliachiwa mdogo wangu mmoja...ila sasa kucheza nako. Ila kusema kweli binafsi ninapenda sana utamaduni huu ingeendelea. Maana hapa ndipo mtoto/watoto wanapojifunza kazi  za nyumbani... Kwa hiyo naweza nikasema nayapenda zaidi maisha ya kale/enzi zangu.

Tuesday, March 7, 2017

LUCIANA DANDA, MJAMZITO ALIYEKUWA AKIPOTEZA DAMU KILA MWEZI

Leo kama desturi yangu ilivyo, katika pitapita nikakutana na hii habari ya dada Luciana Danda ...Imenigusa sana na nimeona niiweka hapa kibarazani kwetu pia. Nimeipata hapa.  

Lusiana Danda (26) alipokuwa na Ujauzito wa miezi nane (Oktoba 2012), alikuwaanatokwa na damu ya mwezi.

Hali hii ambayo ni hatarishi kwa mjamzito na mimba yake ilianza ujauzito ukiwa na miezi minne, baada ya kuugua malaria. 

Lusiana, ambaye ni mkulima na mkazi wa kijiji cha Ifinga, Songea mkoani Ruvuma, alipata matibabu katika zahanati ya Ifinga.

Alivyokutwa na malaria, alipewa dozi ya dawa ya mseto ambayo hakuimaliza. “Niliamua kuacha kumeza dawa baada ya kusikia naendelea vema. Pia, nilipokuwa nameza dawa hizo nilikuwa nasikia maumivu chini ya kitovu; nikahofia mimba yangu isije kutoka,” alisema Lusiana.

Dada huyu hakuwa na mume na hakuwa na mahusiano na mwanaume aliyempa mimba aliyokuwa nayo wakati huu. 

Kwa kuwa tayari alikuwa na watoto wawili na pasipokuwa na mtu mwingine wa kumtegemea, Lusiana aliendelea na kazi za kulima kama kibarua bila ya kupumzika, japokuwa alikuwa mjamzito na anaumwa.

Anasema siku moja, Lusiana akiwa shambani na baada ya kulima kwa saa mbili, ghafla aliaanza kusikia maumivu makali chini ya kitovu.

Maumivu hayo yalikuwa yakizidi kadiri muda ulivyokwenda na alikuwa akijisikia hali ya kutaka kujisaidia haja ndogo.

Alipoenda msalani kujisaidia, ndipo akashtukia kuwa haukuwa mkojo bali ilikuwa ni damu. Damu hii iliendelea kutoka kidogokidogo kwa siku tatu bila kukatika, ndipo Lusiana aliamua kwenda zahanati ya Ifinga kupima kama ujauzito wake bado ulikuwa salama.

“Nilipofika zahanati niliambiwa nitoe Tsh. 2,000 ili nipimwe kujua kama mimba bado ipo. Nilikuwa sina pesa kwa hiyo nilirudi nyumbani nikiwa sina raha,” alisema Lusiana.

Japokuwa damu ilikoma kutoka siku hiyo hiyo ya tatu, baada ya wiki mbili, Lusiana alifanikiwa kupata Sh10, 000 na kurudi tena kwenye zahanati kufanya kipimo cha ujauzito.

Kipimo kilionesha kwamba bado alikuwa mjamzito lakini, mwezi uliofuata damu iliendelea kutoka tena na Lusiana aliporudi kwenye zahanati ya Ifinga kwa ajili ya kujua kwa nini, hakufanikiwa.

“Niliambiwa hakuna vifaa vya kuchunguza kujua kama damu inayotoka inasababishwa na nini; na mhudumu wa afya aliniambia kuwa hajasomea kujua damu inayotoka kwa mjamzito inasababishwa na nini,” alisema Lusiana.

Kwa mujibu wa Dk. Ahmed Makuani, mtaalam wa magonjwa ya wanawake na uzazi salama kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kutokwa na damu kwa mjamzito ni kiashirio cha hatari sana.

Mjamzito akiona damu inatoka anatakiwa kuwahi haraka hospitali. Dk. Makuani alisema wanawake walio na umri wa zaidi ya miaka 35 wakishika mimba wako katika hatari ya kupoteza damu kwa sababu ya kondo la nyuma kuning’inia katika shingo ya kizazi upande wa ndani.

Tatizo hili linajulikana kama placenta previa. Kitendo cha kondo la nyuma kuvumba kinaweza kusababisha kuachia sehemu iliyojishika na kutoa damu sehemu ile iliyoachia, pamoja na kuziba njia ya uzazi kuwa ndogo na mtoto kushindwa kutoka vizuri, kuzaliwa mtoto mfuu kwa kukandamizwa na kondo hilo, kuzaliwa mtoto njiti pamoja na kuzaliwa mtoto mwenye uzito mdogo.

Naye aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Seif Rashid anasema kuwa tatizo la mjamzito kupoteza damu ni tatizo sugu na kubwa sana hapa nchini Tanzania na ndio chanzo kikubwa cha wajawazito kufariki.

Dk. Rashid alisema kuwa, wataalam wa kulitatua tatizo hilo wapo wachache sana katika zahanati mbalimbali za vijijini ambako asilimia 75 ya watanzania ndio wanaishi huko.

“Kwa sasa tupo katika mkakati wa kuboresha zahanati mbalimbali kwa kuwapeleka watumishi wa sekta ya afya kusoma, masuala ya uuguzi kwa miaka miwili ili muuguzi anapokutana na tatizo hilo awe na ujuzi wa kumsaidia mjamzito,”alisema Dk. Rashid.

Wakati Sera ya Afya ya 2007 inasistiza utoaji wa huduma bora na bure kwa mjamzito, hili bado ni changamoto kwa maeneo kama Ifinga, Songea.

Zahanati ya Ifinga ina nesi mmoja na muhudumu wa afya aliyefika darasa la saba mmoja. Pia, katika zahanati hiyo, kuna mganga moja na mpimaji magonjwa maabara mmoja.

Hakuna mtaalam wa magonjwa ya mjamzito na wala hakuna vifaa tiba kama mashine ya kumsaidia mtoto kupumua akizaliwa.

Kwa wakati huu, ambapo Lusiana alikuwa ni mjamzito na kuhitaji huduma hizi, kulikuwa hakuna dawa za kumchoma sindano mama ili mfuko wa uzazi usinyae baada ya kujifungua na mzani wa kupimia mtoto akizaliwa mbovu.

Japokuwa ameshindwa kupata ufumbuzi wa tatizo lake, Lusiana anatarajia kujifungua katika zahanati ya Ifinga. Hana uwezo wa kwenda katika hospitali ya Peramiho inayomilikiwa na Kanisa Katoriki Jimbo la Ruvuma, ambapo ni kilometa 243 kutoka katika kijiji cha ifinga.

Nauli ya kwenda ni Tsh.38,000 na gharama za kujifungua ni Tsh. 11,000; hapo bado gharama za kuishi. Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Songea Dk. Daniel Masawe alisema kuwa katika wilaya hiyo, wajawazito 95 kati ya 100,000 kila mwaka wanapoteza maisha kwa sababu ya upungufu wa damu.

Alithibitisha kwamba vifo hivi vinachangiwa na ukosefu wa vifaa tiba pamoja na wataalam wa kumsaidia mjamzito kujifungua salama katika zahanati mbalimbali kwenye wilaya hiyo. "Kwa sasa watalaam wa kumsaidia mjamzito kujifungua salama ambao wamebobea katika ukunga hapa Songea ni wanne tu, ukilinganisha na zahanati 35 tulizonazo," alisema Dk. Masawe.

Mtaalam wa magonjwa ya akinamama katika hospitali ya Peramiho Dk. Marieta Mtumbuka alisema kuwa mwezi Septemba mwaka 2012, wajawazito wawili walifika katika hospitali hiyo wakiwa na tatizo la kupoteza damu.

Kati ya hao ni mmoja alikuwa na miaka 37. Mjamzito akiumwa malaria na kucheleweshwa au kutokumaliza matibabu, anakuwa hatarini kupatwa na tatizo la kutokwa na damu.

Ndiyo maana, kwa mujibu wa Dk. Rashid kuna umuhimu wa mjamzito kutumia dawa ya mseto kwa sababu ndio dawa pekee iliyofanyiwa utafiti na kugundulika inaweza kutibu na kumkinga mjamzito na mtoto aliye tumboni na malaria akitumia kipindi ambacho haumwi malaria.

“Wizara imeamua kupitisha dawa ya mseto baada ya tafiti mbalimbali kubaini dawa ya chloroquin inausugu wa kuzoeleka na wadudu wa malaria. Tulipotoka katika dawa ya chloroquin tukaanza matumizi ya dawa ya fansider lakini nayo ikaonesha uwezo mdogo wa kukabiliana na wadudu wa malaria.

Baada ya utafiti ndio tumegundua dawa mbadala ya kumkinga mjamzito na malaria ni dawa mseto,” alisema na kuongeza kuwa mjamzito anapewa dawa ya mseto akiwa na mimba ya wiki 20 na wiki ya 28.

Katika kitabu cha hotuba ya makadilio ya mapato na matumizi ya mwaka wa fedha 2012/2013, kinafafanua kuwa jumla ya dozi 9,196,080 za dawa mseto pamoja na kusambaza vyandarua vya hati punguzo vyenye viuatilifu 5,412579 kwa wanawake wajawazito lakini Lusiana hana chandarua.
















"Nilipoanza kwenda zahanati kupima ujauzito wangu, sikupewa chandarua. Niliambiwa vimekwisha na sina uwezo wa kununua chandarua hivyo nalala bila ya kutumia hicho chandarua,"alisema Lusiana.

Aidha kwa mujibu wa bajeti ya afya ya mwaka 2012/2013, kumekuwa na ongezeko la vituo vya afya na zahanati za serikali na binafsi, kuanzia mwaka 2005 kutoka zahanati 4,322 hadi zahanati zahanati 4,679 mwaka 2012.

Kwa upande wa vituo vya afya, kumekuwa na ongezeko kutoka 481 mwaka 2006 hadi kufikia 742 mwaka 2012 na kwa upande wa hospitali kutoka 219 hadi kufikia 241.

Bado kuna wanawake kama Lusiana wanaoshindwa kupata huduma za afya zenye ubora na kwa gharama wanazoweza kuzimudu.

Monday, March 6, 2017

JUMATATU HII YA KWANZA YA MWEZI HUU MACHI/TATU KIVIHI...MAUA...

HISTORIA FUPI :- Maua haya jina lake lina fanana na jina langu kidogo...yanaitwa Hyacint... nami naitwa Yasinta. Lakini pia nimewahi kusikia Hyacint ni jina la kiume... Sasa cha kuchekesha mimi haya maua yananidhuru(Allergic) :-)

Friday, March 3, 2017

TUANZA MWISHO WA WIKI HII KWA HIZI KUMBUKUMBU ZETU ZA ASILI AMBAZO KWA SASA ZINAPOTEA...


Napatwa na faraja kubwa sana pia furaha nionapo vitu kama hivi ambavyo nimekuwa navyo vya asili. Ambavyo yatupasa kuviendeleza ili kizazi chetu kijue tumetoka wapi nao waweza kuwaeleza kizazi chao...NAWATAKIENI WOTE MWISHO WA JUMA UWE MWEMA SANA. Kapulya wenu...

Thursday, March 2, 2017

VAZI LA LEO LA KAPULYA WENU AKA MMILIKI WA MAISHA NA MAFANIKIO...

Hili vazi nimelipenda sana nimelinunua leo leo...hapo ni pozi tu  hapo nadhani mtafikiri najaribu kuruka lakini hapana ni kutaka tu kuonyesha hizo picha za kwenye vazi....
 Na hapa mdada kajikunyata .....baridi  hiyo sio mchezo

 Hapa anawaza kiasi kwamba anajikuna kichwa
Hapa napo inaonekana kama vile  yupo katika dimbwi la mawazo ... ila hapa ni pozi tu...:-)