Thursday, August 31, 2017

NIMEONA TUBAKI KIDOGO KATIKA MKOA HUU WA RUVUMA ....HAYA KUWA SAMBAMBA NAMI....


Kama hukujua jina RUVUMA limetokana na nini sasa wajua ni kwamba:- Ruvuma ni eneo la Tanzania. Jina lake ni kutokana  na Mto Ruvuma ambao  mipaka yake ipo kusini mwa Msumbiji.
PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA...NI KAPULYA WENU.

Tuesday, August 29, 2017

HISTORIA FUPI YA WANGONI WAKIWA KATIKA ARDHI YA WASHONA WAKIJA KATIKA ARDHI YA TANZANIA

Historia ya Afrikas foto.

Mara baada ya kutokea vita vilivyofahamika kwa jina la mfekane kwenye miaka ya 1800, , vilivyokuwa vikihususisha makabila yalikuwa yakipatikana kusiniu mwa Afrika. Wangoni waliamua kuondoka na kusambaa Afrika mashariki na kati wakiwa na Kiongozi wao Zwangendaba. Wakati wanasambaaa Afrika mashariki na kati, Wangoni walipitia sehemu nyingi sana, zipo sehemu walizopokelewa kwa heri na zipo sehemu walizopokelewa kwa shari. Lakini ukweli ni kwamba Wangoni waliondoka Afrika kusini kutokana na vita vilivyotokea. Na sababu kubwa ya vita hivyo ni sera ya upanuzi ya mfalme wa kabila la Wazulu aliyefahamika kwa jina ka Tshaka Zullu. Kutokana na vita hivyo ambavyo pia vilihusisha hata watu wengine ambao hawakuwa Waafrika kama vile Wadachi na Waingereza. Hivyo Wangoni waliamua kuondoka kusini mwa Afrika na kuja Afrika ya mashariki na kati. Sasa wakati wanakuja Afrika ya kati na mashariki Wangoni walipita sehemu nyingi sana. Moja ya sehemu ni ardhi ya Washona . Kwa ufupi ni kwamba Washona ni moja ya jamii zinazopatiakana katika ardhi ya Zimbabwe. Na zaidi jamii ya Washona wanapatikana mashariki mwa jamii za Wakalanga ( hii ilikuwa moja ya sehmu ambayo Wangoni walipita mara baada ya kuvuka mto Limpopo). Washona waliamia maeneo hayo wakiongozwa na mtemi wao aliyefahamika kwa jina la Ska-vunza kwenye karne ya 18. Na ifahamike kuwa Washona ni moja ya kabila ambalo linapatiakna katika kundi hili la Wangoni. 

Monday, August 28, 2017

SWALI-: KWANINI MIAKA HII VAZILA MWANAMKE WA KIAFRIKA LINAKOSA UMAARUFU?

Tazama dada huyu alivyopendeza kwa mavazi ya kiafrika, tunapungukiwa na nini tukivaa kama hivi?

Friday, August 25, 2017

JAMANI MWENZENU BADO NIPO NYASA KWETU NAKULA SAMAKI CHAKULA NIKIPENDACHO KUPITA VYOTE:-)

Yaani ni kwenda tu ziwani na unapata samaki uwapendao...hapomie nimechagua leo MBUFU  ni huyo mkubwa na "sengefu" huku tunawaita hivyo hao samaki wa mbele ya baiskeli .....NAWATAKIENI MWISHO MWEMA WA JUMA.

Thursday, August 24, 2017

JIONI NJEMA MSIONE KIMYA NIPO NANYI

Panda, panda, panda mlima panda. Panda usichoke. ....mwapendwa wote...

Monday, August 21, 2017

HUU NDIYO MLO WETY KAMILI HUKU NYASA

Ugali wa muhogo kwa maharage, dagaa na samaki pia huwa matembele au kisamvu ila leo tumesamehe:-) KARIBUNI TUJUMUIKE. NAWATAKIENI MWANZO MWEMA WA JUMA.

Sunday, August 20, 2017

NAPENDA KUWATAKIENI JUMAPILI NJEMA KWA NENO HILI....

......Yeye ajibuye kabla hajasikia, ni mpumbavu na aibu kwake
MITHALI 18:13
JUMAPILI NJEMA IWE YENYE AMANI, FURAHA NA BARAKA. TUSIKILIZANE KWA MAKINI NA PIA TUPENDANE!

Friday, August 18, 2017

HAINA KEMEKALI HII...NI BORA ZAIDI KWA AFYA!

POMBE AINA YA KOMONI
NAPENDA KUWATAKIENI MWISHO WA JUMA MWEMA ILA KUNYWA KIDOGO USIPITILIZE. PANAPO MAJALIWA TUONANE TENA JUMA LIJALO HAPA HAPA. KAPULYA WENU...

Wednesday, August 16, 2017

KUMBUKUMBU:- LEO TUTEMBELEE MBAMBA BAY...NA UVIVU WA DAGAA...

 Kama muonavyo dagaa wakiwa katika maandalizi ya kukaushwa - kibiashara zaidi 

Tuesday, August 15, 2017

KAPULYA WENU AMETAMANI MLO HUU LEO

Hakika asiyetamani mlo huu mmmhhh yaani nimeamka leo hii nikiwa na hamu sanaya mlo kama huu .....ngoja nifanye mpango. Au nile kwa macho tu:-)

Saturday, August 12, 2017

Wednesday, August 9, 2017

FANYA KAZI PIA CHUKUA MUDA WA KUPUMZIKA PALE INAPOTAKIWA.....

Hivi kwa nini sisi binadamu daima tunafanya kazi kwa ajili ya keshe,  lakini wakati kesho ikija, badala ya kufurahi, lakini bado tutafikiria kesho tena? Hebu tufurahie leo basi !.

Tuesday, August 8, 2017

UJUMBE TOKA KWA KAPULYA KUJA KWA YEYOTE ATAKAYEPITA HAPA



Katika maisha :- Kitu kizuri ni pale unapojisikia /unapojua ya kwamba hapa  duniani mtu /watu ana/wana furaha kwa ajili yako wewe

Monday, August 7, 2017

KILIMO CHA BUSTANI KWA MTINDO MPYA ....KAZI YA MIKONO YANGU

 HAPA NI NYANYA TENA JANA TUMEANZA KULA
 PILIPILI
ZABIBU PIA ZIPO
Niwatakieni mwanza mwema wa juma hili panapo majaliwa tutaonana tena.....Kapulya wenu:-)

Thursday, August 3, 2017

LEO TUANGALIE :- SIFA ZA MTAMA NA VIRUTUBISHO VYAKE!


Sifa za mtama:- Mtama una virutubisho muhimu vinavyotakiwa katika mwili wa binadamu. Tafiti zinaonyesha kuwa mtama una kiasi cha wanga, nishati, nyuzi nyuzi, na mafuta karibu au sawa na mahindi au nafaka nyingine.

Mtama una madini aina ya chuma na chokaa kwa wingi kuliko mahindi au nafaka nyingine. Una protini kwa wingi kuliko mahindi, mchele au ngano. Mafuta yake hayanarehamu, Una vitamin B complex,vitamin C  na vitamin E kwa wingi. Mtama una madini ya zinc, phosphorus, potassium, na manganese kwa wingi kuliko nafaka nyingine.

Mtama una vimelea viitwavyo phenolica mbavyo ni mhimu sana kwa mwili kujikinga na saratani, Mtama hauna gluten  hivyo ni  salama kutumiwa na watu wenye matatizo au ugonjwa  wa Celiac.
Muhimu: Sukari yake huyeyuka taratibu sana mwilini hivyo mtama ni chakula kinachofaa kuliwa na watu wenye magonjwa kama kisukari.
HII NIMETUMIWA NA RAFIKI  NIKAONA NI SOMO ZURI KWA WENGI ....AHSANTENI.

Wednesday, August 2, 2017

HIVI NDIVYO VYAKULA AVIPENDAVYO KAPULYA WENU

Ugali wa ulezi na nyama ya kuku, na sio ugali tu ugali na mlima wake juu ukiisha huu ni lazima usingizi mnono utapatikana iwe mchana au usiku:-)
Samaki waliokaangwa kwa ustadi haswaaaa
Au tu chips MIHOGO...nimekula sana mlo huu wakati nipo chuo kwanza naupenda pia ilikuwa bei rahisi  na unashibisha . Ukipata na kachumbali yako mmmhhh utajiuma kidole au pia ulimi:-) Haya niwatakieni mlo mwema siku ya leo chochote utakachokula kiwe kitamu.....PANAPO MAJALIWA

Tuesday, August 1, 2017

KAPULYA KATALII KIDOGO

Kasafisha macho kidogo sio mbaya hapa hili jengo ni makumbusho ya vita  nchini Norway
Nashanga shangaa tu:-)
Hapa  ilikuwa ni mlima kidogo kwa hiyo ikawa kama ule wimbo wa mchakamchaka panda, panda , panda usichoke....WOTE MWAPENDWA...