Thursday, December 31, 2015

SALAMU/BARUA KUTOKA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO:- SHUKRANI KWA WOTE!!!

Mmmhh! huyu Twiga kanipita urefu nitafika huko kweli...

Habari zenu jamani!!
Yamebakia masaa machache tu kuumaliza mwaka huu 2015 na kuingia katika mwaka mpya 2016. Hakika miaka inayoyoma na watu tunazidi kuzeeka. Ninachotaka kusema ni kwamba, blog ya MAISHA NA MAFANIKIO inapenda kuwashukuru wanablog wenzake wote, wasomaji wote na watembeleaji wote kwa ushirikiano mzuri tulioonyeshana.

Najua katika maisha watu wote hawawezi kuwa sawa yaani kimawazo. Lakini katika hizi blog zetu kwa asilimia kubwa imekuwa ni changamoto kwetu. Tumekuwa hatupendi kupoteana, mara mmoja wetu anapokuwa kimya kwa muda basi wengine tunakuwa hatuna raha tunachukua hatua ya kumtafuta. Hii yote inaonyesha ni jinsi gani ukaribu wa wanaBLOG sisi tu/ulivyo, hakika najivuna sana kwa uwepo wenu na kwa hili napenda kusema SISI SOTE NI NDUGU. NA PIA NAPENDA KUWATAKIENI WOTE KILA DOGO NA PIA KILA KUBWA MTENDALO LIWE JEMA. NA MWAKA 2016 UWE WENYE MAFANIKIO. KAMA KUNA KITU ULIAHIDI KUFANYA MWAKA HUU BASI JITAHIDI UFANYA KABLA HAUJAISHA. KWANI KUMBUKA HAKUNA KISICHOWEZEKANA. NA PIA KAMA KUNA KITU AU MTU NILIMKWANZA BASI NAOMBA TUSAMEHEANE KWANI HAKUNA BINADAMU ALIYEKAMILIKA. PAMOJA DAIMA. KAPULYA WENU!!!!

Tuesday, December 29, 2015

KARIBUNI TULE EMBE.....

Wandugu mpo  ule msimu wa kula embe sasa umefika. Karibu  tujumuike...duh! Ama kweli  watu tumetoka mbali. ..maisha haya. ...

Monday, December 28, 2015

PALE HALI YA HEWA INAPOBADILIKA...LEO ASUBUHI ILIVYOKUWA/DET SNÖAR!

Mila na desturi au nisema ni mazoea ya nchi nyingi za Ughaibuni/ulaya siku ya Krismas kuwa na thaluji yaani kweupe huko nje lakini krismas hii haikuwa hivi hasa Swedan badala yake theluji imeanguka jana 27/12 mpaka leo 28/12 na kamera ya maisha na mafanikio imebahatika kupata picha hizi kama uonavyo...
Wakati mwingine ni safi kuacha gari na baiskeli na hapo ndipo utakapofaidi mambo angalia hii picha  hapa nilikuwa nikitoka mazoezi ya asubuhi:-) pia ni vizuri kutembea/kimbia na kamera......

 Basi nikalipokaona hako kajua nikaanza kuimba kala kawimbo ka mchakamchaka ....Jua lile...nikabadili nikaanza kuimba Idiamini akifa mimi siwezi kulia......Kama nilivypsema Ujenzi unabana ila leo nimepata kamuda...na pia sasa nitapumzika kidogo na ujenzi mpaka huu mwaka uishe ndo tutaendelea...Bado siku 4-3½ hivi kuufikia mwaka  mpya...TUOMBEANA  ILI TUWEZE KUUONA ...NI MIMI KAPULYA WENU!!


Friday, December 25, 2015

NAWATAKIENI WOTE KRISMASI YENYE UPENDO, AMANI, FURAHA NA BARAKA TELE!!

Kamera ya Maisha ya Mafanikio ilikuwa mitaani lao na imepata picha hii ya mtoto Yesu..Hapa Papa Franciskus akimkabidhi mtoto Yesu  ili aende akalale holini ....Mwokozi amezaliwa. Na sasa hebu tusikilize mwimbo huu ambao ni zilipendwa wale wote wenye umri kama mimi na zaidi nadhani watakuwa wanaukumbuka..KARIBUNI.

YESU NDIYO SABABU YA KUWA NA HII SHEREHE YA KRISMASI...KWA HIYO BASI TUWE NA KRISMASI YENYE UPENDO, AMANI, FURAHA NA BARAKA....KRISMASI/NOEL NJEMA.

Tuesday, December 22, 2015

KUFANIKIWA SI LELEMAMA YATAKA MOYO NA UVUMILIVU NA KUJITUMA....!

Mara nyingi nimesikia watu wakisema, aise fulani yule  ana maendeleo sijui inakuwaje. Ni kwamba amevumilia, badala ya kula nyama kala mchicha kila siku, kanywa maji kila siku, kalala kwenye mkeka na hata mwanzo wa maendeleo yake ni biashara ndogondogo/ genge. Lakini utakuta wengine wengine wakikaa na kusubiri wakidhani watashushiwa na Mungu. ...TUJITUME NA MAFANIKIO TUTAYAONA.....KILA LA KHERI TUPO PAMOJA!!!

Sunday, December 20, 2015

HII NI ZAWADI YANGU YA LEO NILIYOTUMIWA NA RAFIKI AJUAYE YA KWAMBA NAPENDA VITUMBUA

Napenda kusema AHSANTE kwa zawadi. Pia nawatakieni wote JUMAPILI HII YA MWISHO KABLA KRISMASI.....KAPULYA

Friday, December 18, 2015

Tuesday, December 15, 2015

UJENZI WA NYUMBA ....MKIONA NASUASUA BASI MJUE NIPO KATIKA ZOEZI LA UJENZI WA NYUMBA.....MBINGA

 HAPA NI MSINGI WA NYUMBA INAANZA ...NI SEHAMU YA MABANDA NIMEANZA
 BAADA YA SIKU KADHAA ILIFIKIA HAPA NI  KAMA MUONAVYO NI MATOFALI YA KUCHOMA
 HAPA NYUMBA IPO TAYARI NA SASA KENCHI ZINAPANDISHWA....NA NI MWONEKANO KWA NYUMA,,
 HAPA WAWEZA KUONA KENCHI ZIMEKWISHA PANDISHWA NA NI MWONEKANO KWA MBELE......
HAPA TAYARI TUMEEZEKA ...KAMA NILIVYOSEMA NIMEANZA NA MABADA  NA NI NUSU TU YA SAFARI........PICHA ZAIDI ZITAKUJA:-) KILA LA KHERI  PAMOJA DAIMA. KAPULYA WENU.

Thursday, December 10, 2015

IWE PICHA YA WIKI HIII....

Sasa hapo sijui atakulaje  huo ugali? Niwatakieni kila la kheri ..pamoja daima... Kapulya

Wednesday, December 9, 2015

LEO NI TAREHE 9/12 AMBAYO N I MIAKA 54 YA UHURU TANZANIA ...LAKINI MWAKA HUU RAIS KASEMA WANANCHI WOTE KATIKA SIKU HII WACHUKUE MUDA NA KUFANYA USAFI...

Na kama unavyoona katika picha wananchi wapo bega kwa bega katika zoezi hili la usafi katika hii siku.  Halafu naona hata Mh. Rais mstaafu Jakaya Kikwete naye  hayupo nyuma....

Tuesday, December 8, 2015

TUNDA LA PERA SIO TUNDA TU ISIPOKUWA :- MAJANI YA MPERA KWA NYWELE ZINAZOKATIKA NA KUPUNGUA

Wanawake wengi wanaopenda urembo wa nywele wamekuwa wakihangaika hata  kama bei mbaya kisa tu kujaza nywele kichwani na kuzifanya zisikatike.
Wasiokuwa na muda wa saluni na wasiokuwa na hela hizi ni habari njema kwao kwamba majani ya mpera ni mazuri kwa kukuza nywele na kuzitibu zile zinazokatika.
Jinsi ya kuyatengeneza kama dawa
Chukua majani yanayotosha kwenye kiganja chako kisha weka kwenye sufuria yenye lita moja ya maji, chemsha kwa muda wa dakika 15 mpaka 20.
Baada ya hapo, yaache yapoe kisha paka kwenye nywele zako kuanzia kwenye mzizi wa nywele mpaka mwisho.
Ukimaliza fanyia masaji nywele zako kama mtu anayepaka mafuta nywele zote.
Baada ya hapo unaweza kuacha kwa muda  kisha ukaosha.
Fanya hivi mara kwa mara, naamini utaona mabadiliko.

Monday, December 7, 2015

MRADI WA MAJI KUCHIMBA MTARO NA KUWEKA MABOMBA: HAPA NI KUSINI MWA TANZANIA KATIKA KIJIJI CHA MUHUKURU WANANCHI WAPO KATIKA KAZI YA KUPATA MAJI SAFI ONA WANAVYOSHIRIKIANA....

 Maji ni uhai wananchi wakiwa bega kwa bega kivhimba mtaro.
 Mtoto naye hayupo nyuma kushiriki zoezi hili muhimu.
Haikuishia hapo..Vijana nao wanashiriki kwa makini zoezi hili la mitaro.

Sunday, December 6, 2015

HII NI JUMAPILI YA PILI YA MAJILIO:- NA LEO TUANGALIE MAANA YA MAJILIO KATIKA MAISHA YA BINADAMU

JUMAPILI YA PILI(2) YA MAJILIO
Sisi binadamu hatuwezi kuishi daima katika hali ileile bila ya matazamio. Hasa kijana anatarajia mambo mapya tena mema. Hivyo tunajitahidi kuyapata. Asiyetazamia chochote amevunjika moyo, hana hamu ya kuishi. Lakini matazamio ya kibinadamu yakimfikia mtu hayamridhishi moja kwa moja. Kristo tu anatimiza hamu zote kwa kumkomboa kutoka unyonge. Majilio yanatukumbusha kila mwaka matarajio ya kweli na hivyo yanaamsha hamu ya kuishi kwa bidii ya kiroho.
BASI WOTE MUWE NA AMANI PIA UPENDO KATIKA JUMAPILI HII YA PILI YA MAJILIO NA SIKU ZOTE....AMINA!

Friday, December 4, 2015

AKAMWAMBIA MKEWE AMKATE KICHWA!

Leo nimemkumbuka sana mdogo wangu KOERO MKUNDI kumsoma zaidi gonga hapa...  http://koeromkundi.blogspot.se/

Karibu mgeni Sungura
Hapo zamani za kale Sungura alijenga urafiki na Jogoo, sasa siku moja Jogoo akamualika Sungura amtembelee nyumbani kwake. Basi sungura akajikusanyia zawadi zake na kumuaga mkewe kisha akaondoka kwenda kumtembelea rafiki yake Jogoo.

Alipofika alikaribishwa kwa bashasha na jogoo, na aliandaliwa chakula kitamu na wenyeji wake, baada ya kula Jogoo alimtoa mgeni wake huyo na kumtembeza sehemu mbali mbali ili kumuonesha fahari ya mji wao, Sungura alipendezwa sana na ziara hiyo.

Ilipofika jioni walirudi nyumbani wakamkuta mke wa Jogoo kawaandalia chakula cha jioni, baada ya kula Sungura alioneshwa mahali pa kulala, kisha jogoo na mkewe nao wakaingia chumbani kwao kulala. Lakini kabla sungura hajapitiwa na usingizi akasikia mazungumzo ya jogoo na mkewe huko chumbani kwao, na mazungumzo yenyewe yalikuwa ni haya.
Jogoo: Mke wangu nikate kichwa nataka kulala mie.
Mke wa Jogoo: Sawa mume wangu,
Sungura kusikia hivyo akataharuki, “He kumbe Jogoo kulala ni mpaka akatwe kichwa? Ilipofika alfajiri akamsikia Jogoo akimuamsha mkewe tena.
Jogoo: Mke wangu, eh, hebu nirudishie kichwa changu nataka wika mie kuwaamsha watu.
Mke wa Jogoo: Haya mume wangu ngoja nikurudishia kichwa chako. watu.

Baada ya kurudishiwa kichwa chake, jogoo akaanza kuwika kama kawaida yake,ili kuwaamsha watu…Koko rikooooo ………Kucha kucheleeeeeeee………

Basi kulipopambazuka sungura akaamka na kupata staftahi iliyoandaliwa na wenyeji zake na baada ya stafutahi akapewa zawadi za kwenda nazo nyumbani kwake, lakini kabla ya kuondoka aliamualika Jogoo naye amtembelee ili kulipa fadhila kwani alipanga kumfanyia jogoo mapokezi makubwa kushinda yale aliyoyapata.

Sunguara alipofika nyumbani kwake alimsimulia mkewe juu ya safari yake na mapokezi aliyoyapata, pia hakusahau kumweleza mkewe mshangao alioupata kuhusiana na ule utaratibu wa Jogoo kukatwa kichwa na mkewe kabla ya kulala na kurudishiwa kichwa chake alfajiri ili awike.

Sungura alimtaka taka mkewe na yeye afanye hivyo siku wakitembelewa na Jogoo, kwa kuwa amemwalika aje kuwatembelea, alimtaka mkewe amkate kichwa akitaka kulala, na kukirudishia alfajiri ili amwonyeshe jogoo kuwa na yeye anaweza kukatwa kichwa na kurejeshewa asubuhi.

Ni kweli baada ya juma moja kupita Jogoo akamtembelea Sungura, na yeye alibeba zawadi kemkem kwa ajili ya wenyeji wake.

Alipofika alipokelewa na wenyeji wake ka bashasha, na kuonyeshwa ukarimu wa hali ya juu.

Kama alivyofanyiwa kule na Jogoo, na yeye Sungura alimtembeza mwenyeji wake kumuonesha mji na maeneo ya vivutio vya mji wao.

Walirejea jioni na kupata mlo wa usiku, huku wakipiga soga. Ulipofika muda wa kulala, sungura alimuonesha jogoo mahali pa kulala, na yeye na mkewe wakaingia chumbani kwao kulala.

Mara Sungura akamwambia mkewe.

Sungura: Mke wangu eh, hebu nikate kichwa mie nilale..
Mke wa Sungura: Sawa mume wangu.
Mke wa Sungura akachukua kisu na kumkata mumewe kichwa, na kukitenganisha na kiwiliwili.

Asubuhi kulipopambazuka akaanza kumuamsha mumewe,a lakini hakuamka alijitahidi kukiunganisha kichwa ili mumewe aamke lakini hakikuunga na wala Sungura hakuamka, alikuwa amekufa tayari.

Mke wa Sungura ikabidi aombe msaada kwa Jogoo, lakini Jogoo alipofika chumbani aliona damu zimetapakaa kila mahali na kichwa cha Sungura kilikuwa kimetenganishwa na kiwiliwili.
Jogoo kuona hivyo, akataharuki, lahaulaaaa…kulikoni huyu hana kichwa, aliauliza Jogoo.
Mke wa Sungura akamsimulia Jogoo kuwa utaratibu wa kukatwa kichwa kabla ya kulala aliupata kutoka kwake alipowatembelea.

Ndipo Jogoo akamwelewesha kuwa yeye huwa hakatwi kichwa na mkewe kama vle alivyofanya Sungura bali mkewe humsaidia kuficha kichwa cheke kwenye mbawa zake kila akitaka kulala na alfajiri mkewe humsaidia kutoa kichwa chake kutoka kwenye mbawa ili aweze kuwika kuwaamsha watu.

Mke wa Sungura liaposikia hivyo akaanza kulia kwa uchungu kwa kuondokewa na mumewe.

Jogoo aliporudi kwa mkewe alimsimulia masaibu yaliyomkuta Sungura.

Hadithi hii nilisimuliwa na bibi yangu Koero, siku nyingi kidogo, wakati nilipokwenda kijijini likizo. Nimeikumbuka leo nikaona si vibaya nikiiweka hapa ili tutafakari pamoja.

Je hadithi hii inatufundisha nini? Tafakari………………………

Koero Mdogo wangu huko uliko ujue unakumbukwa sana na wote hasa mimi dada yako kwa hiyo usomapo ujumbe huu nitafuta TAFADHALI...Dadayo Yasinta /kapulya....Ahsante kwa hadithi hii.