Friday, January 31, 2014

MWISHO WA MWEZI JANUARI TUUMALIZE ZILIPENDWA HATA KAMA SIELEWI ILA MZIKI UNACKEZEKA...KARIBUNI!!!!!!.....


AU TU LABDA TUSIKILIZE NA HUU WIMBO WA MONICA....


Mara nyingi ukiwa sambamba sana na walezi huwa unakumbuka vitu vingi sana.....nadhani mmenielewa...haya tuendelee kuselebuka ...tuonane mwezi ujao.  Oh! Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutulinda salama wote tulioumaliza mwezi huu na pia napenda kuwaombea wote waliotutangulia na pia wagonjwa. Na pole nyingi kwa ndugu zetu wa Morogoro /Kilosa mji kasoro bahari, Mungu awape nguvu. IJUMAA NJEMA.

Thursday, January 30, 2014

KAMA KAWAIDA NI ALHAMIS LEO...TWENDE MPAKA MBUGA YETU YA RUAHA ILIYOPO KUSINI MWA TANZANIA!!!!!!!


Mbuga ya Ruaha :- Mbuga hii ni nzuri na ndogo ambayo haijulikani sana kana SERENGETI au NGORONGORO. Ipo kusini wa Tanzania, kama uonavyo kuna simba, tembo, nyati, twiga na wanyama wengine wengi wa pori ambao wanaipendezesha Mbuga hii kwa ukamilifu mazingira yetu ya Afrika/Tanzani....ALHAMIS IJIYO NA MBUGA MPYA...

Wednesday, January 29, 2014

NIMEPENDA VITU/FANICHA/SAMANI HIVI/HIZI VYA /ZA ASILI VINAVUTIA NA NI IMARA..EBU ANGALIA

Kama kuna mtu anafahamu wapi vinapatikana nitashukuru kupata taarifa. Nilisikia vinapatikana Mfaranyaki/Songea kwetu  nimeulizia sijafanikiwa.....PAMOJA DAIMA.JUMATANO NJEMA PIA JIONI NIJEMA.

Tuesday, January 28, 2014

Monday, January 27, 2014

JUMATATU HII YA MWISHO KWA MWEZI HUU WA KWANZA TUIANZE NA KUMALIZA NA BAADHI MISEMO NA MAFUNZO YAKE!!!

1. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu. Hii ni kwamba hatuna budi kuwatii wazazi/walezi wetu tukitaka kuuelewa ulimwengu.
2. Si utu kwenda kwa uliyempa zawadi na kumwambia akarudishie zawadi yako.
3. Usimdharau adui ijapokuwa ni dhaifu.....Ni kwamba akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki.
4. Ili binadamu aishi na kufaulu katika maisha yake, hana busi kujitolea na kupambana na hali yoyote katika mazingira yake.
5. Kuwa na tamaa inaweza kuua. Kama wahenga walivyosema:- Njia mbili zilimshinda Fisi.
6. Mtu akifanya kazi kwa bidii hufanikiwa. Au, maskini hachoki, akichoka ujue amepata.
7. Ujinga na woga husababisha taabu na hasara kubwa ulimwenguni.
8. Wivu huangamiza familia nyingi ulimwenguni.
KAMA NAWE UNA NYINGINE KARIBU KUUNGANA NAMI...JUMATATU IWE NJEMA SANA!!!

Saturday, January 25, 2014

NAPENDA KUWATAKIENI WOTE JUMAMOSI NJEMA KWA KIPANDE HILI:- NASONGA MBELE....


JUMAMOSI NJEMA SANA....NA TUKUMBUKE YA KWAMBA SISI SOTE NI NDUGU NA WATOTO WA BABA MMOJA!!!!!

Thursday, January 23, 2014

LEO TWENDE KUTEMBELEA MBUGA YA NGORONGORO...KARIBU TANZANIA YETU


Kama nilivyosema ALHAMIS ya wiki iliyopita nimeanzisha kipindi kipya kila Alhamis tutakuwa karibu na Mbuga moja kutoka nyumbani TANZANIA na leo tupo NGORONGORO .....TUONANE TENA ALHAMIS IJAYO  KATIKA MBUGA NYINGINE.

Wednesday, January 22, 2014

JUMATANO YA LEO TUANGALIE:- JAMII YA KI-SUKUMA!!!

Nimefanya utafiti kidogo kuhusu ndugu zetu wasukuma..nimefanya hivi kwa vile nilipokuwa mdogo nilisimuliwa mambo mengi sana kuhusu wasukuma na babu  yangu mzaa mama pia bibi ..ni Kwamba babu yangu alikuwa fundi mwashi miaka ya hiyooooo......Na hivi ndivyo nilivyopata kuhusu Wasukuma/wanyamwezi...Karibu.
------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
KWANZA TUANGALIE MAANA YA NENO WASUKUMA:-
Wasukuma ni mkusanyiko wa makundi madodomadogo kutoka maeneo jirani, na kwamba kundi kubwa zaidi limetoka kusini wa eneo hilo la mkoa wa Mwanza. Jina hili limetokana na neno SUKUMA maana yake kwa lugha ya Kisukuma na Kinyamwezi KASKAZINI, yaani moja wapo wa pande nne za dunia yetu. Wanyamwezi ambao lugha yao inafanana sana na Kisukuma huwaita walio Kaskazini mwao "Bhasukuma" yaani watu wa KASKAZINI. Na wasukuma huwaita "Bhadakama" yaani watu wa KUSINI. Siku zote, wasukuma na wanyamwezi walijulikana kuwa wao ni "Bhantu" na kutokana na neno hilo kumekuja kujulikana kundi linaitwa WABANTU. Kundi hili mara zote limetambulika kwa lugha wanayozungumza ya KIBANTU. Hivyo, Wanyamwezi, Wakimbu hadi Wabemba walioko Zambia ni kundi kubwa la wabantu kufuatilia lugha wanazozungumza.
Karibu kujadili nami kama kuna kitu nimekikosa au sahau......JUMATANO IWE NJEMA...

Tuesday, January 21, 2014

MAISHA:- USAFIRI/USAFIRISHAJI KWA NJIA YA BAISKELI...HUPUNGUZA GHARAMA NA PIA MTUMIAJI HUWA NA AFYA NJEMA PIA NI SAFI KWA MAZINGIRA!!!

 Katika maisha usikaa tu na kungoja ..lazima kujishughulisha. Hapa kijana yupo safirini kuelekea soko la kuuza ulazi ila kujipatia kitoweo/chakula. Baiskel zinasaidia sana miaka hii tafauti na miaka tuliokulia wengine kila kitu ilikuwa na kichwani....
 Na hapa anasafirisha chakula, Ndizi hizo..
Naye huyu anaelekea sokonoi kuuza mananasi yake
Na hapa ni baiskel yangu. Kwa kweli usafiri wa baiskel ni mzuri sana na wa haraka huhitaji kusubiri foleni. SWALI:- Umegendua nini kati ya baiskel hizi nne?....Nawatakia JUMANNE NJEMA SANA WOTE

Sunday, January 19, 2014

MAOMBI YANGU YA JUMAPILI YA LEO NI KAMA YAFUATAYO.....

Mwenyezi Mungu nakuomba ulisikie ombi langu. Nakubali kwamba mimi ni mtenda dhambi. Na ninaamini ulimtuma Yesu Kristo kuniokoa, ninamkubali Yesu kama Bwana na Mkombozi wangu. Nisamehe dhambi zangu unifanye safi. Nipe nguvu za kutembea katika njia zake. Naomba hivi kwa jina la Yesu Kristo. AMINA...,,,KWA MAOMBI YANGU HAYA NAPENDA KUWATAKIENI WOTE JUMAPILI HII IWE YA UPENDO NA FURAHA. jUMAPILI NJEMA KWA WOTE.

Saturday, January 18, 2014

HAYA NI MAPISHI YA KAPULYA JIONI HII YA LEO..KITIMOTO NDANI YA UYOGA......

 Ni kitimoto, uyoga niliochuma mwezi wa kumi, cream kidogo, nyanya , chumvi na maji kidogo na viungo vingine....
 Na baada ya muda chakula kilikuwa tayari kuliwa na hapa ni shani yangu, ikiwa imeshehena na wali, kitimoto,uyoga  kama hapo juu na sallad tamuuuu ambayo ni:- nyanya, tango, carroti, majani ya salladi na chizi(fetaost) na kitunguu kwa mbaliiii...
Nikapandishia na glasi ya maji kama uonavyo...Ila usisite kuja kuna chakula bado karibu sana tena sana kujumuika nasi. JIONI NJEMA.

JUMAMOSI NA MAPUNZIKO MEMA KWA WOTE.

Nadhani wengi tunakumbuka ilivyokuwa enzi za mababu zetu...na pia miaka ya 1980 mpka 1990..Kanisa moja, shule moja rais mmoja Chama kimoja na pia kula na kunywa pamoja na sahani moja na kikombe/robo/kichonjo kimoja. Lakini sasa  mambo haya hakuna kabisa inasikitisha sana. JUMAMOSI NJEMA NDUGU ZANGUNI...PIA KUMBUKENI POMBE SI MAJI....:-) TARATIBU

Thursday, January 16, 2014

SERENGETI/TANZANIA



KARIBUNI TANZANIA YETU...KILA ALHAMIS TUTAKUWA TUKITEMBELEA MBUGA MBALIMBALI TANZANIA...TUONANE TENA ALHAMIS IJAYO...

Wednesday, January 15, 2014

WANAWAKE NA HISIA ZA USALITI: ZIJUE DALILI ZAKE!!

Inawezekana ukawa ni mke wa mtu au una mpenzi wako ambaye mna matarajio ya kufunga ndoa na kuishi pamoja. Kuna wakati unaweza kujaribiwa na kujikuta ukikabiliwa na hatari ya kumsaliti mpenzi wako. Kujaribiwa huko kunaweza kukutokea katika mazingira mbalimbali kutegemea na maeneo yako ya kazi au mahali unapofanyia shughuli zako za kila siku. Kwa mfano inaweza ikatokea umefahamiana na mwanaume mahali pako pa kazi, anaweza kuwa ni mteja au mfanyakazi mwenzio. Inatokea siku moja anakualika kwa ajili ya chakula cha mchana, baada ya mtoko huo, unajisikia kutoka naye kwa mara nyingine…………………
Kutoka kwenu mara kwa mara kwenda kupata chakula cha mchana, unagundua kwamba huyu bwana ni mtu mwenye kiwango cha juu ya usikivu, katika mazungumzo yenu anaonekana sana kwamba ni mwelewa na mwenye subira. Hana papara katika kuzungumza na mara nyingi huwa ni msikilizaji. Huyu unaweza kumwita rafiki ingawa ni wa jinsia tofauti, (Sidhani kama ni dhambi kuwa na rafiki wa jinsia tofauti……!) Kuna kitu wenzetu wazungu wanakiita Emotional infidelity, kwa tafsiri yangu naweza kusema ni hisia za usaliti katika mapenzi. Maana yake ni kwamba unaruhusu mtu mwingine wa jinsi tofauti azibe pengo la hisia ambalo lingetakiwa lizibwe na mpenzi wako au mume wako. Kama inavyofahamika kwamba wanawake ni viumbe wa hisia, wanapenda sana kusikilizwa, na wanapenda kuona wapenzi wao au waume wao wanawasikiliza. Inapotokea hitaji hilo halitekelezwi na mpenzi au mume wake, basi ni rahisi sana atakapotokea mtu mwingine ambaye bila kujua akamudu kuziba pengo hilo kuvutiwa naye na kuhitaji kuwa naye karibu mara kwa mara.
Hapa chini nitazitaja dalili ambazo zitakuonyesha kwamba ukaribu wako na huyo rafiki utakupelekea kuisaliti ndoa yako:
1. Unatamani sana kumuona ukiwa na shauku kubwa ya kuwa naye karibuna kutumia muda mwingi kuwa naye
2. Unajikuta ukichagua mavazi na kujikagua sana ukijiuliza jinsiatakavyo vutiwa na mavazi yako pale atakapokuona
3. Unapokuwa naye unajikuta ukimweleza matatizo ya mahusiano yako na mpenzi wako au mumeo
4. Unajikuta ukimgusa gusa wakati mkiongea au kufanya naye utani unaoweza kupeleka ujumbe tofauti kwake kwamba labda umevutiwa naye kimapenzi
5. Unawsiliana naye kwanza kabla ya kuwasiliana na mpenzi wako au mumeo pale unapokabiliwa na jambo lolote lenye kutatiza na linalohitaji msaada wa haraka au ushauri
6. Unajikuta ukiwaza jinsi gani ungekuwa na amani iwapo ungekuwa na uhusiano naye wa kimapenzi au ndoa
7. Inawezekana ukawa unamzuingumzia sana kwa mwenzi wako au kwa marafiki zako, au inawezekana ukawa humzungumzii kabisaaa na kuficha urafiki wenu.
8. Unajitahidi sana kuficha urafiki wenu na kutomzunguimzia rafiki huyo kwa mwenzi wako kwa sababu unajua kwamba jambo hilo linaweza kukuletea balaa.
Kwa ujumla unapojikuta umempata rafiki wa jinsia tofauti na yako halafu ukahisi kulipukwa na moyo juu yake zikiwemo dalili nilizozitaja hapo juu, basi ujue uhusiano wako na mume au mpenzi wako uko mashakani. Usipokuwa makini utamsaliti.
Habari/mada hii nimetumiwa na mkereketwa/msomaji wa Maisha na Mafanikio kwa kutaka tu mimi nisome lakini mimi nimeona ina mafundisho ndani yake nikaona ni bora niiweke hapa ili wengi wafaidike na ELIMU hii.

Tuesday, January 14, 2014

NIMEOTA NDOTO KUWA NIPO LUNDO NA KINGOLI KWENYE SHAMBA LA MPUNGA NALINDA ILI NDEGE WASILE NA PIA NAVUNA MPUNGA...

 Hapa ni mwezi wa nne mpunga huwa unakuwa umekomaa kiasi hiki kwa hiyo walaji ni wengi kama vile ndege...Kwa hiyo kwa kuokoa mpunga ni lazima kila siku kwenda shambani kulinda/kufukuzia ndege..Duh nimefanya kazi hii ...mpaka sasa naota ndoto--Maisha ya zamani kweli ni dhahabu.
Hapa mpunga umeshakauka ni mwezi wa sita na ni wakati wa kuvuna sasa kula ubwabwa/wali...Sijui kati ya hawa nipo wapi?..Mnaniona au?...Kuvuna ni raha zaidi kuliko kulinda ndege:-)KILA LA KHERI NA LOLOTE UFANYALO:-)

Sunday, January 12, 2014

JUMAPILI YA LEO HALI YA HEWA ILIKUWA HIVI, KWANGU MIMI NAWEZA NIKASEMA HALI YA HEWA IMECHAFUKA.....BARIDI -10C...HAPA BAADHI YA PICHA NILINASA LEO

 Kuanzia jana asubuhi mpaka leo bado theluji inaanguka tu ebu angalia hapa ukiangalia kwa makini sana kushoto kwako ni lile enoa ambalo tumezoea kuiona bustani ya Kapulya lakini sasa mmmhhh! haiwezekani kabisa ....hata hivyo ni lazima kutoka nje ingawa ni -10C huko nje....angalia hapa ....

 ...hapa tupo nje ni siku ya wazazi na watoto wao kuwa nje kwa vile ni siku maalumu kwa darasa la binti yetu. Ni kwamba wamepata na wageni kutoka Colombia kutokana na darasa lake kusoma lugha ya spanish wao walikuwa kule Colombia mwaka jana na sasa waColombia wamefika hapa  juzi. Kwa hiyo wazazi na watoto ni jambo la muhimu kuwapokea wageni na kuwaonyesha nini kufanya...ila duh! wameshangaa kwani ni baradi mno ...hata hivyo wanafurahia hali hii.
Mama maisha na Mafanikio alivovalia tayari kwa kupambana na baridi ya leo lakini, wee bwana haikuwa joto vidole vilikufa ganzi kabisa  hata kama ningeenda kwa daktari na kuchomwa sindano nisingesikia maumivu...Si ajabu kuonekana kama tembo maana mtu unajitahidi  kuvaa nguo nzito ila kuepukana na baridi.....Hiii ndio JUMAPILI YANGU YA LEO..PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA. JUMAPILI NJEMA KWA WOTE.


Thursday, January 9, 2014

UNAKUMBUKA HABARI/HADITH HII KITABU CHA DARASA LA SITA:- MVUMILIVU HULA MBIVU? KUMBUKUMBU!!

Hapo zamani za kale Sungura na Mbwa Mwitu walioa mabinti wa jamaa mmoja. Mbwa Mwitu alimwoa kifungua mimba na Sungura kitinda mimba. Mbwa Mwitu  alikuwa mvivu sana tena mlafi. Sungura alikuwa hodari wa kutega ndege. Kila siku nyumbani kwa Sungura kulikuwa hakukosekani kitoweo kizuri. Mbwa Mwitu akaanza kumwonea wivu Sungua kwa sababu alipendwa na watu wote wote kijijini.
Mwaka fulani njaa ilitokea katika kijiji chao. Mbwa Mwitu na Sungura wakamwendea mkwe wao kuomba ardhi ya kulima. Akawaonyesha mwitu mzuri wenye rutuba nyingi. Sungura hakupenda kufyeka msitu pamoja na Mbwa mwitu. Alikataa kwa sababu aliuelewa sana uvivu wa Mbwa Mwitu.
Kila siku asubuhi Mbwa Mwitu alipokwisha pata kifungua kinywa alikwenda shambani. Alipofika huko alikata mti mmoja, miwili au mitatu, kisha akakaa chini ya mti. Kwenye mti kulikuwa na mtambazi uliotambaa juu na kushikilia matawi imara kabisa. Mbwa Mwitu alitengeza pembea nzuri sana juu ya mtambazi huo. Ikawa kila afikapo shambani kukata miti miwili, mitatu, kisha hurukia pembea yake akijiningíniza.
Kila siku Mbwa Mwitu alirejea nyumbani mapema na kufanya fitina kubwa nyumbani kwa Sungura. Alimwambia shemeji yake kwamba Sungura hafanyi kazi yo yote ya kutayarisha shamba. Kazi anayoifanya ni kutege ndege tu. Kwa kuwa Sungura alikuwa hodari, kila siku alileta ndege aliowanasa kwa mitego yake. Jambo hili lilimfanya mke wa Sungura aamini maneno ya Mbwa Mwitu. Mke wa Sungura alipoona hayo, ugomvi ukazuka kati yake na mumewe. Ugomvi huu ukaendelea siku baada ya siku. Mbwa Mwitu alikuwa ibilisi mbaya sana. Sungura alijua haya yote yalitokana na fitina ya Mbwa mwitu. Hakusema neno. Alivumilia kwa sababu alifahamu kuwa njia ya mwongo ni fupi.
Majira ya kupanda yalipowadia Mbwa Mwitu alimwendea tena mkwewe kuomba aina mbalimbali za mbegu akapande shambani mwake. Akapewa. Mbwa Mwitu alipokwenda shambani, alichukua kigae. Akakoka moto, kisha akakaanga zile mbegu kwenye kigae, akala akashiba , halafu akalala fofofo. Mbegu zilizobaki akaziweka akiba mpaka kesho yake. Asubuhi ya siku iliyofuata aliendelea na mambo yale yale. Kama waswahili wasemavyo, "Chovya chovya humaliza buyu la asali", hivyo Mbwa Mwitu alimaliza mbegu zote.
Sungura hakwenda kwa mkwewe kuomba mbegu. Hii ilimfanya Mbwa Mwitu azidi kutia fitina, hata Sungura akawa anachukiwa sana. Hata hivyo akaendalea kuvumilia. Baada ya kununua mbegu za kila namna kwa fedha alizojiwekea akiba, Sungura alikwenda shambani mwake akapanda. Punde si punde, mvua kubwa ikanyesha na mbegu zote zikaota vizuri sana.
Wakati wa kupalilia ulipotimia, Mbwa Mwitu akaendelea na mchezo wake ule ule wa pembea. Lakini Sungura alifanya bidii mpaka shamba lake likawa safi kabisa. Alifanya kazi hiyo kwa juhudi kubwa, akayafuata mashauri ya wataalamu wa kilimo. Juhudi yako pamoja na maarifa ndivyo vilivyokuwa msingi wa kulipata shamba kubwa lenye mimea mizuri.
 Mbwa Mwitu alikwenda kisirisiri kuangalia shamba la Sungura. Uzuri wake ulimshtua sana, naye akazidi kumwonea wivu. Alikata shauri kuliharibu. Akakusanya majani makavu na kueneza katika shamba ya Sungura, ili ayatie moto na kuliunguza shamba. Lakini kwa kudura za Mungu; Sungura aliwahi kugundua hila hiyo. Mbwa mwitu alipotaka kulichoma moto, Sungura aliwahi mapema shambani mwake. Mbwa Mwitu akashindwa kuliharibu shamba la Sungura.
Mbwa mwitu hakuchoka kumfanyia Sungura hila. Baada ya miezi kadhaa alipeleleza habari za shamba la Sungura akafahamu kuwa mazao yalikuwa tayari kuvunwa. Akakusudia kuyaiba mazao ya Sungura. Alijidai kwamba shamba lile lilikuwa lake. Akawaomba mkwe na jamaa wajitayarishe kwenda shambani kuvuna, lakini Sungura akazipata habari hizo.
Kesho yake asubuhi na mapema, Sungura akawahi shambani mwake akiwa na jamaa. Mbwa Mwitu alipogundua kwamba Sungura amewahi, akalazimika kuwapeleka wale aliokuwa nao shambani kwake. Walipowasili mahali Mbwa Mwitu alipopaita shamba lake, hawakuona dalili y yote ya mazao. Mkwe wake alihamaki, akamsaili kwa nini hakukuwa na mazao. Mbwa Mwitu alifedheheka akashindwa kujibu kwa aibu. Karibu na shamba chini ya mti mkubwa, wakaona mahali alipokaangia mbegu. Waligundua maganda ya karanga na mpunga yametapakaa huku na huko. Mkwe wa Mbwa Mwitu na jamaa wakarudi nyumbani wamekasirika sana.
Jioni ileile, Sungura alimwendea mkwe wake akamweleze kwamba angefurahi sana kama yeye pamoja na jamaa wangefika kuliona shamba lake. Mkwewe alikataa shauri hili. Akaeleza jinsi alivyotendewa na Mbwa Mwitu. Sungura akambembeleza sana mkwewe mwishowe akakubali.
Waliondoka asubuhi na mapema kwenda kuliona shamba la Sungura. Walipofika shambani wakaona mazao mengi yaliyostawi vizuri. Sungura akamweleza kwamba hilo ndilo shamba lake. Akawaomba waingie shambani kuvuna. Wote waliofika walifurahi sana. Zaidi ya hayo walishangaa jinsi Sungura alivyokuwa mvumilivu kwa fitina za Mbwa Mwitu. Mkwe wa Sungura akaona ni kweli kwamba matendo hukidhi haja maridhawa kuliko maneno. Mbwa Mwitu alikuwa amesema maneno mengi kujisifu na kumfitini Sungura lakini hakuna alilokuwa ametenda.
Jioni ile mkwa wao aliwaita Sungura, Mbwa Mwitu na jamaa wote, akasema, "Leo tumepata fundisho kubwa kwa vijana hawa wawili, Sungura na Mbwa Mwitu. Kwa juhudi na uvumilivu, Sungura amejipatia chakula cha kutosha. Kwa ajili ya fitina, Mbwa Mwitu hakuambulia cho chote. Nataka wote mjifunze kuwa "Juhudi ni Shina la Maendeleo," na ya kuwa kwetu tunayo ahadi isemayo " Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko," Kwa hiyo anamwonya Mbwa Mwitu aache fitina, uchochezi na uvivu. Badala yake afanye kazi ili afaidi matunda ya jasho lake."
Tangu siku ile Mbwa Mwitu alianza kujirekebisha. Akashirikiana na wanakijiji wenzake kuendeleza kijiji chao. Kutokana na hadithi hii twakumbuka maneno ya wahenga wetu yasemayo "Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu."
UJUMBE:- Hii  hutokea mara nyingi sana ..Tuache uvuvi, fitina na tufanye kazi ili kuendelea..Akina Sungura wapo wengi sana katika dunia hii.

Wednesday, January 8, 2014

MWANAMTINDO WA WIKI HII NI HUYU HAPA.....EBU MWANGALIE ALIVYOPENDEZA ..BINAFSI NIMEPENDA PICHA HII MNO:-)!!!!

Nimependa sana picha hii...ni kama ule wimbo wa Lady jaydee ..natamani kuwa malaika ..natamani tena kuwa mtoto..Miaka hii unaweza kuwapiga watoto wako picha na kuwa kumbukumbu kubwa sana ...Natamani huyu mtoto angekuwa mimi kwani sina picha ya umri huu...Picha hii ni kwa hisani ya dada Nancy Sumari nimeipata HAPA. MUWE NA SIKU NJEMA

Tuesday, January 7, 2014

NI JUMANNE YA KWANZA YA MWAKA HUU 2014 NAMI NIMEONA TUIANZA KWA MTINDO HUU:- METHALI ZETU!!! UNAZIKUMBUKA HIZI?:-)

1. Asiyekuwepo machoni, na moyoni hayupo.
2. Bendera hufuata upepo.
3. Chururu- si ndo, ndo, ndo.
4. Dua tupu haliachi kuvuma.
5. Fuata nyuki ule asali.
6. Hakuna msiba usiokuwa na mwenziwe
7. Heri kufa macho kuliko kufa moyo.
8. Ikiwa hujui kufa, tazama kaburi,
9. Jogoo la shamba haliwiki mjini.
10. Kimya kingi kina mshindo mkuu.
SIKU YAKO IWE NJEMA SANA NAWE KAMA UNA METHALI UIKUMBUKAYO KARIBU KUISEMA/ANDIKA.

Saturday, January 4, 2014

LEO NI SIKU YANGU YA KUZALIWA:-)

Siku  ya Ijumaa tarehe 5/1/1973 Mama na Baba Ngonyani walibarikiwa kumpata mtoto wa kike. Na Wakamwita mtoto huyu YASINTA. Na leo ile siku imejirudia tena ila leo ni Jumapili. Napenda kuwashukuru wazaz/walezi wangu kwa kunitunza/kunilea na sasa nimekuwa MAMA. Namshukuru kwa kuniepusha na mambo mabaya, magonjwa na pia vishawishi. Pia napenda KUMSHUKURU MWENYEZI MUNGU kwa kunilinda na leo natimiza miaka tena. Na halafu napenda kuwapa HERI YA KUZALIWA wote waliozaliwa mwezi huu waliotimiza tayari miaka na watakaotimiza siku zijazo.. Nachukua nafasi hii kuwashukuru WASOMAJI WOTE WA MAISHA NA MAFANIKIO KWA KUTONICHOKA. Mmenitia nguvu sana bila ninyi isingewezekana. 

NA AHSANTE SANA KWA MWAKA 2013. JUMAPILI NJEMA NA NASEMA NAWAPENDENI SANA:-)....AHSANTENI WOTE.

Thursday, January 2, 2014

HIVI NDINYO MWAKA 2014 ULIVYOPOKELEWA NA BAADHI YA WATU/TULIALIKWA NA MARAFIKI

 CHAKULA KILICHOANDALIWA,  VIAZI NYAMA NA ASPARAGUS
 SHEREHE INAENDELEA .....
 BADO TUNAKULA NA MAONGEZI YANAENDELEA ...................................
MAMA NA MTOTO WANATAFAKARI MWAKA 2013.......Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunilinda/kutulinda watu wote ambao tumeuona mwaka huu 2014. Kwa mara nyingine KHERI SANA KWA MWAKA MPYA 2014....UWE WENYE AMANI NA MAFANIKIO.