Monday, July 16, 2012

HADITHI HADITHI…..HAPA NI HADITHI YA MVUVI NA SAMAKI WA DHAHABU!!!

Nieipenda hadithi hii na nimeona nisiwe mchoyo ni hadithi nzuri hata kwa watoto wangu wamekisoma ....nimeisoma kwenye kitabu na mwandishi ni Alexander Pushkin. Haya karibuni.

---------------------------------------------------------------------------------------------------------
Hapo zamani za kale. Palikuwepo na mzee mmoja, aliyeishi na mke wake mzuri sana kandokando ya bahari yenye maji ya rangi ya mbingu na kina kirefu. Waliishi kwenye kibanda cha udongo na miti.
Walikuwa wameishi pale kwa miaka thelathini na siku thelathini. Baba Kizee akivua samaki na bibi mzuri akifuma nguo.
Siku moja baba kizee alitupa nyavu baharini, nyavu alizivuta juu zilikuwa zimejaa uchafu wa baharini. Alitupa tena nyavu baharini, nyavu alipozivuta juu zilijaa gugu-bahari.
Mara ya tatu, nyavu zikazamishwa tena majini nyavu alipozivuta juu :- Tazama! Alikuwemo samaki mmoja. Si samaki wa kawaida, bali ni samaki wa dhahabu.
Samaki wa shahabu, akaomba msamaha. Huku akisema kwa sauti ya binadamu ”Ewe baba kizee, nirejeshe baharini nitakulipa malipo mema, nitakupatia chochote utakacho.”
Baba kizee alipigwa na mghafala. Akaingiwa na woga. Alikuwa amevua maeneo haya kwa miaka mitatu na ushee lakini hata siku moja hakupata kumsikia samaki anayezungumza.
Akamwachia samaki uhuru wake huku akisema maneno ya huruma. ”Ewe samaki wa dhahabu enenda kwa salama katika njia zako huna haja ya kunilipa fadhila. Rejea kwenye kina cha bahari na kuogelea na kupiga mikambi utakayo.”
Baba kizee alirudi kwa mkewe mzuri akamwadithia kuhusu kioja.
”Leo nilimnasa samaki wa ajabu si wa kawaida, bali wa dhahabu samaki huyo alinena lugha yetu akanisihi nimrejeshe baharini na akaniahidi zawadi maridhawa kwa kunitaka nitaje nitakacho! Nami sikutaka ujira wake nikamrejesha baharini bila malipo.”
Mke akamwambia mumewe kwa karipio ”Kefule, mjinga kichwani we! Huwezi kupata pato la samaki ukashindwa hata kuomba kibeseni cha kuogea! Tazama kile cha kwetu kilivyoraruka katikati.
Baba kizee akaenda kwenye bahari ile ya maji ya mbingu tena yenye kina kikuu, akaona jinsi bahari ilivyochafuka akapaza sauti yake, akaita na mara samaki wa dhahabu akaja akiogelea ”Kulikoni baba kizee nieleze nami nijue!”
Kwa mwinamo wa hadhi baba kizee alijibu ”Ewe mwenye rehemu Ewe mkuu wa samaki! Mke wangu mzuri ana uchungu nami haniachii kwa kutaka utakalo ataka tuwe na beseni jipya la kuogea kwa kuwa la kwetu kongwe limeraruka hadi katikati”.
Samaki wa dhahabu naye akajibu sawia ”Usiwe na hofu kamwe ewe baba kizee na enenda sasa kwa amani huko uendeko. Utalikuta hilo beseni jipya!” Baba kizee alirejea kwa mkewe mzuri na kujionea mwenyewe baseni jipya liko pale. Lakini bibie ukali akazidisha Mjinga wahedi yaani hilo ndilo ombi lako kuu hilo beseni la kuogea! Kuna faida gani kamwe” Kuwa na beseni tu la kuogea? Hebu rudi himahima enenda kwa samaki mkuu. Uende umwinamie, umwombe kijumba kizuri. Baba kizee akashika njia kwenda kwenye ile bahari ya maji ya rangi ya mbingu. Sasa bahari ilikuwa nyeusi iliyoghafilika.
Baba kizee akapaaza sauti na kuita na samaki wa dhahabu akaja akiogelea ”kulikoni baba kizee hebu uniambie hima!
Kwa mwinamo wa hadhi baba kizee akajibu ”Rehema iwe kwako Ewe mkuu wa samaki mke wangu mzuri amesawijika zaidi haniachii huru ila kuningángánia hatatulia bila kupata kijumba kizuri.” Samaki wa dhahabu akajibu sawia ” Usijali baba kizee enenda sasa kwa amani utapata takwa lako la hicho kijumba kizuri.”
Baba kizee akarejea kwenye kibanda chao kikongwe, hakuona dalili yoyote ya kibanda kikongwe. Badala yake akaona kijumba kipya, kizuri mno! Kimepakwa chokaa, kina mnara mzuri wa kupitishia moshi. Na milango ya mpingo , pia na dirisha la nakshi.
Na katika kiti cha bustanini aliketi mkewe mzuri, huku akiwa hajitambui kwa mahasira yaliyomzonga ”Kefule, pumbavu wewe usiye na kitu kichwani! Yaani hicho ndicho ulichoomba kijumba hicho cha ovyo! Rudi tena kwa samaki mkuu mwinamie na kumwambia mimi sitaki kuwa mke asiye na hadhi bali mwanamke wa nasaba bora!” Baba kizee alikwenda tena baharini. Nayo bahari ikachafuka zaidi na kusikitika. Baba kizee akapaaza sauti, akaita na samaki wa dhahabu akamjia akiogelea. ”Kulikoni ewe baba kizee, hebu niambie nami nijue!”
Kwa mwinamo wa heshima baba kizee akamjibu sawia. ”Usijali neema, ee Mkuu wa Samaki! Mke wangu, kwa roho isiyosikia kitu haniichii nikapata pumzi. Sasa ameamua hatakuwa mwanamke dhalili yeye ataka kuwa mwanamke wa nasaba bora!”
”Usiwe na hofu, baba kizee enenda kwa amani sasa.” Baba Kizee alirejea kwa mkewe mzuri. Lo! Akaona nini? Jumba zuri na barazani mkewe amesimama , amevaa vazi la maridadi la nyoya jema. Na kichwani kavaa kilemba kilichotariziwa vilivyo na vito vyema vikimning´nia shingoni. Na pete za dhahabu zilipamba vidole vyake na viatu vyororo vyekundu vikimkubali miguuni….ITAENDELEA……

19 comments:

ray njau said...

@Yasinta;
Asante kwa hadithi iliyojaa mambo ya mafundisho kwa jamii.

emuthree said...

Hadithi hizi zina mafunzo na hekima kubwa

Anonymous said...

da yasinta bwana..utamu umekolea ndo umekatiza duh! tafadhali usikose kuendeleza hadith hii.
Dorothy,

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Hadithi kweli ni nzuri na tekenyeshi so to speak. Sharing is always a very spiffy thing.

Interestedtips said...

utamu uendelee jamani...mbona umepotea twahitaji muendelezo..ila hadithi huwa zina mafundisho sana

Simon Kitururu said...

Mmmmh!

Phocus Lukanazya said...

ASANTE KWA HADITHI YAKO NZURI, NIMEIPENDA SANA RAFIKI. JIONI NJEMA...

Anonymous said...

safi sana

Anonymous said...

Godfrey Msele.Dah Hadith Tamu Sana

Unknown said...

nzuri sana hiyo nimeipenda sana ubarikiwe kwa ujumbe huu naiendelee na tena

Unknown said...

Nzuriiiii

Cytotec said...

thanks for sharing

cytotec said...

thanks gan infonya.

obat telat bulan said...

thanks fos sharing"

obat cytotec said...

thanks gan.

obat vimax said...

terimakasih admin.

obat penggugur said...
This comment has been removed by a blog administrator.
Ulimwengu Habari said...

Nice. Hadithi

casinoxo said...

ดูหนังแสนสนุก Crawl คลานขย้ำ (2019) ต้องเข้ามาดูที่เว็บดูหนังออนไลน์ ดูหนังฟรีที่นี่เท่านั้น
https://www.doonung1234.com/