Friday, September 30, 2011

NIMEONA NISIWE MCHOYO:- KARIBUNI TUJUMUIKE MLO WA MCHANA HUU AMBAO NI SUPU YA SPINACHI!!!

Nimerudi toka kazini huku nikawa na hamu kweli kweli ya supu...baadaye nikakumbuka nina spinachi. Kwa hiyo hapa, ni supu ya spinachi ambayo ni:- spinachi, maji, na chumvi. Inaandaliwa kwa dakika 10...Kwa anayetaka anaweza kuweka nusu kikombe cha maziwa au cream. na katika kula unaweza kula na kipande cha mkate pia yai moja la kuchemsha. Ila Kapulya hapendelei sana vitu hivyo kwa hiyo anakula kama ilivyo. KARIBUNI SANA TUJUMUIKE!!!!

MAPENZI NI MKUKI AU MATESO? IJUMAA NJEMA JAMAN!!!I
NGOJA TUMSILIKIZE NA KAKA KIDUMU NA NA WIMBO HUU WA MAPENZI!!!

Thursday, September 29, 2011

WAKATI WA WATU KUNUNA UNAKARIBIA, VICHEKO VYOTE NA TABASAMU VYA SUMMER VYAFIKIA UKINGONI!!!/HÖST/AUTUMN = MAJIRA YA BARIDI YA KUPUKUTIKA MAJANI BRRRR!

Mmmmh! Kazi inaanza sasa. Kaziiiii kwelikweli, maana mtu unavaa nguo na mwisho unaonekana kama una kilo elfu kumi. Haya ngoja niache.

Ila pia ni wakati mzuri sana hasa miti inapopata rangi nzuri kama huu hapo juu inapendeza kusema kweli...Tatizo humwoni mtu ...pia ni kipindi kizuri kwenda mstuni kuchuma uyoga ila unatakiwa kujisitiri kweli .... huu mti rangi zake nipezipenda sana ila muda si mrefu majani yote yatapukutika na kuuacha na vijiti tu au mti unakuwa "uchi":-(


Wednesday, September 28, 2011

MASUALA YA UBAKAJI NA KUPIGA WANAWAKE LINAZIDI KUWA KUBWA

Kama kawaida kile kipengele chetu cha marudio ya Makala/mada, picha au kwa ujumla tusemematukio mbalimbali kitujiacho siku ya kila siku ya JUMATANO ungana nami kujadili jambo hili.Ukitaka kusoma maoni yaliyotolewa na wasomaji mara ya kwanza bonyeza hapa.
Kweli huu ni ubinadamu jamani?
Dunia imeharibika watu wanazidi kupotoka, angalieni haya mambo yanavyozidi kuenea. Mambo kama vile unyanyasaji, kuna ukatili mwingi sana hapa duniani ambao zaidi ni juu ya wanawake na watoto. Hao ndio wanaopata shida zaidi. Ukatili ni kinyume na haki za binadamu na uko ukatili wa aina mbalimbali. Kuna vipigo, matusi, kulazimishwa kufanya mapenzi, kuna baadhi ya mila potofu kama vila ndoa za lazima, kuolewa ukiwa na umri mdogo, kurithi wajane nk.
Bado sijaelewa ni kitu gani kinawafanya wanaume wengine wawapige wanawake. Kwanini umpegi mwenzi wako? Je usipompiga uanaume wako utapotea? Na kuna raha gani kumpiga mwenzako kama mnyama? Na hata mnyama hairuhusiwi kumpiga. Hili suala la kubaka utasikia raha gani wakati mwenzako anapata maumivu yasiyo kifani. Na pia hajapenda.
Je? Mnafikiri hii inaweza kutokana na wengi wanaume wanafikiri wao ndio waamuzi wa kila kitu ndani ya nyumba? Na kwa nini watu wawili waliooana wasikaa chini na kujadiliana na kuona kosa liko wapi. Je? Ingekuwa kinyume ingakuwa sawa?

Au labda wengi wanafuata maandishi haya:- Mwanzo 3:16 Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako, kwa uchungu utazaa watoto na tamaa yako itakuwa kwa mumea, naye atakutawala.
Ndugu wasomaji/wanablog naomba mnisaidie kunipa jibu.

HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA KAKA YANGU SHABAN KALUSE!!!

Shaban Kaluse atimiza miaka 40 leo!Napenda kuchukua nafasi na KUMPONGEZA KAKA YANGU WA HIARI SHABAN KALUSE kwa siku yake ya kuzaliwa. Shaban Kaluse ni kaka mmoja ambaye ni mshauri mzuri sana , msikilizaji, sio mbinafsi. nk. Nikuambieni kitu kimoja? Ni hivi mimi au pia watu wengine wanafikiri kaka, dada au ndugu ni yule uliyezaliwa naye tumbo moja yaani mama mmoja na baba mmoja. LA HASHA. Kaka huyu amekuwa KAKA kweli na amekuwa mwema sana katika familia ya akina NGONYANI. HONGERA SANA KWA KUTIMIZA MIAKA 40 NI MIAKA MINGI MWENYEZI MUNGU AKULINDE NA AKUJALIE AFYA NJEMA!!!

Tuesday, September 27, 2011

Makamu Wa Rais Dr Bilal Atoa Mhadhara Chuo Kikuu Cha Uppsala, Sweden!!!!

Pichani: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Watanzania, waishio nchini Sweden wakati alipokutana nao katika mkutano Septemba 25, katika Ukumbi wa Hoteli ya Gillet Clarion iliyopo Uppsala Sweden. Kushoto ni kiongozi wa Jumuiya ya Watanzania wa Sweden, Prof. Lodhi. Picha: Muhidin Sufian.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ametoa mhadhara kuhusu changamoto za kisayansi katika maadhimisho ya miaka 50 ya Idara ya Sayansi za Kimataifa kwa kifupi ISP ya Chuo Kikuu cha Uppsala kilichopo Uswidi ambapo amefafanua kuwa, mchango wa wanasayansi kutoka katika chuo hiki una manufaa makubwa katika kukuza teknolojia katika sayansi kwa nchi za Afrika.
Makamu wa Rais ambaye alikuwa mhadhiri wa somo la Fizikia katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kabla ya kuingia katika siasa, amealikwa na wanasayansi wa kariba yake katika maadhimisho haya yaliyo na lengo la kutanua uwanda wa tafiti katika nchi za Afrika na hasa Tanzania, ambayo kwa sasa imeanzisha chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela kilichopo Arusha.
Katika ziara hii ambayo Makamu wa Rais ameambatana na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Telezya Huvisa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim pamoja na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Profesa Burton Mwamilwa.
Ujumbe wa Makamu wa Rais ulifika hapa na kupata nafasi ya kuzungumza na Watanzania waliopo Uppsala ambao wengi walitaka kujua kama Tanzania imejipanga vema kukabiliana na tatizo la umeme nchini. Makamu wa Rais ambaye katika ziara hii amekuwa akikutana na wanasayansi mbalimbali wa Sweden na hasa waliobobea katika sekta ya nishati aliwaeleza Watanzania waliokuwa katika mkutano naye kuwa; kama taifa tuna kila sababu ya kukubali kuwa tulifanya makosa huko nyuma kwa kutotambua utanuaji wa vyanzo vya umeme wa uhakika hali inayotuumiza sasa lakini pia akawaambia kuwa serikali imejipanga vema kuhakikisha kuwa tatizo la umeme linapata tiba katika kipindi kifupi na pia kuwa na umeme wa uhakika katika miaka miwili ijayo.
Maeneo makubwa ambayo Makamu wa Rais amekuwa akiwasikiliza kwa ukaribu wanasayansi wa Uppsala na Sweden ni kuhusu vyanzo mbalimbali vya uzalishaji wa umeme vikiwemo vile vya upepo na maji ya bahari huku pia ikiwa Tanzania imeshasaini mkataba wa uzalishaji wa umeme wa makaa yam awe na kampuni ya kutoka China, mkataba uliosainiwa wiki mbili zilizopita katika ya NDC na kampuni ya China ambazo zitashirikiana katika miradi mikubwa katika ukanda wa Mtwara.
Eneo jingine ambalo Makamu wa Rais amekuja kulihamasisha ni juu ya uhusiano wa chuo hiki kikongwe katika uwanja wa Sayansi na namna chuo hiki kitakavyozidisha ushirikiano wake katika kusomesha wataalamu wa Tanzania katika ngazi za Shahada za Uzamivu na mchango mkubwa ukiwa kukipatia uwezo Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela kilichopo Arusha.
Katika ziara hii ya kitaaluma aliyoalikwa Makamu wa Rais inayochukua siku mbili, Makamu wa Rais pia atakutana na Waziri wa Mambo ya Jamii wa Uswidi Ulf Kristersson na Waziri wa Mahusiano na Maendeleo Gunilla Carlsson. Katika ratiba hiyo pia Makamu wa Rais atatembelea Taasisi ya Mazingira ya Uswidi sambamba na kuzungumzia mafanikio ya Kilimo Kwanza kwa wadau wa maendeleo wa Uswidi.

EINSTEIN:- MTAZAMO WA DUNIA UNAPOTIKISWA!!!!


Mara nyingi kama kuna habari nzuri au hata ya kusikitisha na haipo kwa lugha ya kiswahili huwa najaribu kutafsiri. Na nimejaribu kutafsiri hii hapa natumaini nitaeleweka.

Einstein labda alikuwa sahihi. Watafiti nchini Italia madai kwamba aliona neutrinopartiklar kusafiri kwa kasi zaidi kuliko mwanga.
Je, matokeo yake ni imara, fizikia ya kisasa katika mwendo.

UKWELI: Einstein NA MWANGA
Wazo kwamba hakuna kitu kinaweza kusafiri kwa kasi zaidi kuliko mwanga katika utupu - 299 792.5 kwa kila kilomita kwa sekunde - ni wazo la Einstein.
Lakini kulingana na watafiti wa Italia, wafanyakazi katika maabara ya Gran Sasso alisafiri neutrinopartiklarna katika majaribio yao kwa mwendo wa kasi ya kilomita 300,006 kwa sekunde.
- Kama ni kweli, ni kubwa sana. Katika kesi hiyo, Einstein ilikuwa na makosa. Kwa hiyo hii sio kama tunavyoona na, kuamini, anasema Bengt Lund-Jensen, profesa wa fizikia katika Chuo Kikuu cha Ufundi Stockholm (KTH).
Kasi zaidi kuliko mwanga?
Neutrinos ni aina ya chembe ya msingi na ni kwamba ni electrically neutral, na mara chache sana kiutendajihushirikiana na chembe nyingine. Uzito ni mdogo sana., moja ndogo sana. Bilioni kadhaa hupita kila wakati kupitia miili yetu.
Watafiti wa Italia, ambao walitangaza matokeo yao katika CERN, Shirika la Ulaya kwa ajili ya Utafiti wa nyuklia nchini Uswisi, kipimo mihimili ya chembe kama wao alisafiri kutoka CERN mpaka maabara nchini Italia, umbali wa km 730.
Matokeo: neutrinos iliwasili sekunde 60 kasi zaidi kuliko mwanga.
Mtafiti kiongozi Antonio Erradito anasema kwamba kila mtu ametishwa kwa matokeo, lakini wao wana uhakika kwamba inawezekana kuwa. Vipimo vimefanywa zaidi ya miaka mitatu.
Hofu kubwa
Wafanyakazi wenzao kote duniani wamekuwa waangalifu kwa maoni/mtazamo. Hofu kubwa inaweza kuwepo katika hali ya sasa.
- Kuna hatari ndogo ya wao kuchukua mudai wao kwenda nje kwa njia hii. Ni tofauti ndogo sana kwa muda huu mfupi. Lakini kama ni kweli, ni lazima tupata maelezo mapya, anasema Lund-Jensen.
Watakaoathirika zaidi ni wenye masomo ya ulimwengu. dhana ya muda ikiangukia mbali na muda wa kusafiri ungekuwa kinadharia iwezekanavyo.

chanzo:-NI HAPA .

Monday, September 26, 2011

MWANAMKE WA SHOKA WANGARI MUTA MAATHAI AMETUACHA!!!

(1 April 1940 -26 September 2011)
Nimepatwa na mshtuko wa aina ya pekee nilipopata habari ya kwamba mwanamke huyu wa shoka hayupo nasi tena ..ni mwanamke wa shoka, mwanaharakati ...pumzika kwa amani mama yetu..Mungu alitoa na Munga amechukua... habari zaidi soma hapa.

MIAKA 50 YA UHURU TANZANIA!!!!

Mimi leo nataka tutumie maazimisho ya miaka 50 ya uhuru wa nchi yetu kujadili swali lifuatalo :-
Baba wa Taifa hayati mwalimu Nyerere, aliamini na kuja na falsafa ya maendeleo iliyokuwa inasema ili tuendelee kama taifa tunahitaji mambo muhimu manne(4) watu, ardhi, siasa safi na Uongozi bora. Lakini pia akasisitiza ili hayo maendeleo yafikiwe tunahitaji kufanya kazi kwa bidii na maarifa.
Kwa zama hii tuliyonayo pamoja na kuwa na hivyo vitu vinne kumeongezeka suala la UFAHAMU NA MAARIFA.
Swali katika ngazi ya familia na koo zetu za Kitanzania tunahitaji mambo gani ya msingi ili kuendelea.
Maana kwa hali ilivyo hasa kwa sisi watanzania tumebobea katika kulaumu, kulalamika na kulaani wakati hata siku moja kulaani na kulalamika hakujawahi kuwa suluhu ya kile unacholalamikia, kulaani na kulaumu.
UJUMBE HUU:- Nimetumiwa na kaka yangu pia msomaji wa MAISHA NA MAFANIKIO SALEHE MSANDA AMBAYE NI MKAZI WA NJOMBE. TUJADALI PAMOJA....

Sunday, September 25, 2011

TUMALIZE JUMAPILI YA MWISHO YA MWEZI HUU KWA WIMBO HUU!!!

Wiki hii nimekuwa nikitafuta tafuta nyimbo za asili asili...nikakutana na huu ...wanaimba kiswahili lakini mwishoni sielewi wanaimba nini ..Ila nahisi ni KIBENA AU KIHEHE maana nimeelewa maneno kama WINOME.....Mtani Fadhy upoooo nisaidia na wengine WOTE MLIOELEWA ...NATANGULIZA SHUKRANI...
NA NAWATAKIENI JUMAPILI NJEMA SANA WOTE....NDINGI NDINGINDI NDINGINDI WINOMEEEEE!!!!!!!

Saturday, September 24, 2011

UJUMBE WA JUMAMOSI YA LEO!!!

Binadamu ni kama baisikeli, ikisimama inaanguka chini.
NAWATAKIENI WOTE JUMAMOSI NJEMA BINAFSI ITAISHIA KWENYE MAJUKUMU:-(

Friday, September 23, 2011

HII NI HABARI YA KUSIKITISHA SANA WATOTO WAWILI WAUWAWA NA MAMA YAO MZAZI NCHINI SWEDEN!!!

WATOTO WALIO UWAWA NA MAMA YAO MZAZI, ELIAS (KUSHOTO) MIAKA 4 NA TEVIN MIAKA 8.WALIUWAWA KWA KUZAMISHWA KWENYE MAJI.TUKIO LILITOKEA TAREHE 18 SEPTEMBER SIGTUNA SWEDEN.

Kwa undani zaidi unaweza kusoma hapa na pia hapa.

IJUMAA YA LEO INATUFIKISHA MPAKA HUKO UNGONINI YAANI NA NGOMA YAO YA ASILI LIZOMBE..


Hii nadhai wote tumewahi kuisikia..Sasa leo bwana katika kukumbuka kunyumba/nyumbani nikakutana na .....


....hawa kaka zangu hapa wakiienzi NGOMA hiiiYA LIZOMBE kwa kweli nimefurahi sana tena mno...ingekuwa ni hapa niishipo ningeungana nanyi na tungeanzisha kikundi chetu na kuvuta watu wengi..HONGERA SANA NA ENDELEENI NA MOYO WA KUENZI NGOMA ZETU ZA ASILI. IJUMAA NJEMA KWA WOTE....YAANI WE ACHA TU...

Thursday, September 22, 2011

WAZO LA LEO :- USIKIVU WA WANAUME NA WANAWAKE KATIKA MAISHA YA NDOA/ULIJUA KWAMBA...

...Kama unataka kupata usikivu wa mwanamme kitu muhimu ni kumgusa? na pia ulijua kama unataka usikivu wa mwanamke basi mnongóneze!!! TUTAKUTANA/ONANA TENA KESHO!!!!

Tamasha Maalum la Kumuenzi Hayati Dr. Remmy Ongala

Salam,

http://www.youtube.com/watch?v=huNcBwH9_UQ

Aziza Machozi Ongala na mumewe Miael McGeachy, mzawa wa Jamaika, wakiongea na Urban Pulse na Freddy Macha kuhusu shughuli zao kuimarisha kumbukumbu na kazi za mwanamuziki Remmy Ongala aliyefariki Desemba 2010, mjini Dar es Salaam.
Mahojiano yalifanywa katika Ubalozi wa Tanzania, London.

Habari zaidi bofya : http://www.thedkremmyongalafoundation.com/

Asanteni,

URBAN PULSE CREATIVE Wakishirikiana na Freddy Macha

PICHA YA WIKI:- CHUPA ZA MAJI NA MAANDISHI YA MAISHA .....

.....sikuweza kuacha kuzifotoa kwa vile zinalingana na jina la blog hii MAISHA NA MAFANIKIO
nadhani wote mnakumbuka mwanzoni blog hii ilikuwa ikiitwa MAISHA TU:-)

Wednesday, September 21, 2011

YASINTA NGONYANI NA JOHARI YA MATUMAINI

Kama kawaida kile kipengele chetu cha marudio ya Makala/mada, picha au kwa ujumla tuseme matukio mbalimbali KUTOKA BLOG HII YA MAISHA NA MAFANIKIO NA BLOG NYINGINE MBALIMBALI. Ni kipengele kitujiacho kila siku ya JUMATANO. Leo nimefanya upekuzi na nimekukutana na simulizi hii kwa vile inanihusu nimeona ni vema niiweka hapa kama kumbukumbu/mkusanyiko. Ukitaka kusoma maoni yaliyotolewa na wasomaji mara ya kwanza bonyeza Nyasa. karibuni sana.
Nafungua anuani pepe nakuta ujumbe, najiuliza kulikoni ni nani huyu? Alaah kumbe mwana wa nyasa, aliye ughaibuni? Ni mwanzo wa kumbukumbu, furaha na burudani. Mzaha wa hapa na pale kustawisha gumzo. Mtandaoni kwa saa nyingi mazungumzo yasokwisha hamu? Hatimaye ndiyo huyu tupo uso kwa uso tunazungumza tunapiga gumzo hapa na pale najiuliza maswali kadhaa kuhusu huyu mtu lakini najua ni mungu ajuaye mengi.
Mawazo yangu yaavaa uhodari wa kujua na kutaka kuona kile ninachoamini. Siku zinapiga miezi, mwaka na saa zote. Nipo ghorofa ya pili, nasoma ghafla ujumbe mfupi unaingia katika simu, salamu toka ughaibuni, najiuliza nitende vipi kwa mwandada huyu? nafunika vitabu na daftari, namtazama mwenzangu pembeni ananikodolea macho anashangaa vipi naacha kusoma halafu nachezea simu? Namweleza kuna jambo, nataka kuongea na mtu kwanza.Tayari tunajadili hili na lile najadili mambo kadhaa yenye maudhui ya nyasa, halafu tunakumbushana mambo ya Lundo na maisha kwa ujumla.
Inawezekana usinielewe msomaji wangu mpendwa, lakini mantiki yangu ni kukupa mwanzo wa YASINTA NGONYANI na MARKUS MPANGALA. Ni kama andiko la wakristo la yesu alivyowaambia msihangaike kwa lolote wala msibebe vyakula bali mwendako mtajaziwa. YASINTA ni kiumbe mwenye sifa ambazo kila siku naziwazia, najaribu kutafakari, nakumbuka stori zetu za hapa na pale, nakumbuka yale mambo ya WAOOOOOOOOOOO!!!!1 Hee kumbe hatuko peke yetu, tunatulia na kutafakari, tunaleta mzaha kidogo na kustawisha gumzo, mambo ya hapa na pale. Usisahau tupo umbali wa maili nyingi lakini ikawa dakika kuwepo ana kwa ana.
Mimi sinywi soda, situmii pafyumu, wala mafuta makali, siweki dawa nywele zangu daima ni rasta. Nauliza swali aaaahh ndiyo maana Erick naye anapenda sana Rasta siyo? Kicheko kidogo..., namtazama kwa shauku ya kujua mengi....LAKINI nagundua kama kile alichosema Koero kuwa YASINTA NGONYANI ni binti wa kitanzania. Sifa moja kubwa aliyonayo ni MAZOEZI na ukimtazama ni unaweza kubabaika ukasema umri wake ni 23 au 26 hivi kumbe huyooooo.
Hapa nyumbani nina bustani ya matunda na mambo mengi ya nyumbani wala siwezi kubabaikia hayo mambo ya wazungu. Mi hee unaweza kudhani mtu unayezungumza naye anatania lakini kukweli ni binti mwenye itikadi msimamo mkali. Nakumbuka nipo Mbeya, nikabandikwa maaswali lukuki, stori nyingi lakini kikubwa ni faraja za hapa na pale.Msomaji wangu, huyu Yasinta nina mengi ya kumwelezea lakini nafupisha na kutoa vipande ili upate msingi kamili. Hata hivyo nimemlazimisha kucheza muziki wa KWAITO anacheza usipime kabisaa, majuzi nikamwambia ebu selebuka na MYEKE BABA ya Mandoza... akacheka kidogo.
Nikumbushe msomaji YASINTA ni mkarimu, mtulivu, mkali, mwenye upendo, smikivu, mdadisi ndiyo maana nilimwita Mama Maswali magumu, mchokonozi. Nakumbuka kuna kitu alinichokonoa lakini nikajua udadisi ukaanza.... tusijali hayo lakini nakwambia kama huwezi kuishi na YASINTA basi wewe ni kiumbe wa ajabu. Mara nyingi utamsikia Markus mdogo wangu unatakiwa kujali muda wa kupumzika, utulivu na kujenga afya kwa kufanya mazoezi....Wakati mwingine inakuwa kama unaota kulala gizani na kulamba mchanga halafu huchafuki kumbe upo ukwelini na unawaza ukweli uleule wa siku zote.
Sikiliza mimi nataka kufanya kitu fulani katika blogu, nifanyeje? Ahh tunachapa gumzo tunafundishana haya na yale. Na fundsho letu kuu la mwisho lilikuwa pale ufkweni kuhusu NeoCounter. Ni mambo matamu ya teknolojia.SWALI UNAJUA ALIANZAJE KUBLOGU NA KUIJUA BLOGU YA KARIBUNI NYASA?Kuna kisa cha YASINTA katika blogu yangu hii ambayo naomba msomaji ukitafute. na mara nyingi amenihimiza kuandika tena kwani amevutiwa nacho.Kumbe kuna siku alikuwa akitafuta akina YASINTA wenzake wapo wangapi duniani, .... ndiyo hapo akutana na KARIBUNI NYASA na kisa kile cha Yasinta mwenzake. vilevile nilimpatia kazi ya kuchoma samaki kama unakumbuka msomaji kuna TANGAZO LA KAZI NYASA, yeye ndiye alishinda. Ila anapenda sana kula MAEMBE halafu na tabia yake ya KUNYWA CHAI ISIYO NA SUKARI yaani CHINGAMBU ni moja ya vionjo vyake na ambavyo nakiri ni MTANZANIA.Nikamwambia niseme au nisiseme kile kitu fulani....... aaaah Msomaji wangu utanichoka nadhani unaweza kudhani nafanya mzaha. Lakini kiini chake ujue tu ni binti ambaye naona tofauti yake na wengine ni mtazamo na misimamo yake isiyotetereka. Ni mdadisi sana huyu kiumbe, hachoki kujifunza kila mara lakini ndoto yake ilikuwa SISTA yaani wale watawa... utakumbuka ndoto yangu ilikuwa kuwa Padre lakini yamepita...SAHAU. Nakumbuka nikawa namlazimisha kumsoma kaka Ansbert Ngurumo....
Upendo wake na namna anavyoweza kujadili na watu ni kitu ambacho kinanifanya wakati mwingine nimwambie nina wivu sana, na hilo sifichi na nimesema daima ana anajua hilo. Mungu kamleta kwa kusudio la kupendwa na watu wala hana mengi. JE UNATAKA NIKUWEKEE PICHA TULIZOPIGA? aaaaaaahh msomaji nadhani hii stori ndogondogo ni habari kamili ingawaje imekaa mshazari. mtanisamehe kwa kutoweka picha tulizopiga.....Watoto wake anawaeleza kabisaaa..... nakumbuka anasema na Camilla.... mwanangu funga kanga , lazima kutii utamaduni wetu sawa? Camilla huyoooo anatoka ndani ya bwawa... anaiendea kanga.... mrembo huyu anachukua na kuifunga mwendo wake wa maringo taratibuuu kama twiga najongea mezani. Pembeni Erick sijui kiswidi chao wanasema Irik au? Kijana mpenda mazoezi kama mamake... anafuga rasta.... lakini siku hizi kazinyoa bwana...... a ha ha ha ha!
YASINTA GERVAS NGONYANI.... ngoja nikutaji jina leke jingine..... aaaah hapana siyo ruksa ni mimi tu nalijua au vipi usitake kujua sana. Ni kweli Yasinta mpenzi wa lugha ya nyumbani na bahati nzuri ni mtundu wa kujua lugha za wengine, najua ni wachache wanamudu hilo... lakini ameweza kujifunza lugha za wanyasa wale wanaongea kama wamalawi.... zile MULIBWANJI.... halafu tunahamia mazungumzo katika kimatengo... kingoni chenyewe, kimanda, kimpoto.... kinyakyusa..... nk. ukitaka kufanikiwa maishani ni lazima ujue utamaduni wako na kuheshima na utajua wapi unatoka.....YAKO MENGIIIIII SAANAAAAAAA............................... tutahabarishana siku nyingine.... manake kuna siri, mafanikio, shubiri na mwenendo mzima wa maisha yake.... harakati zake........ NITAKUMEGEA MAMBO MSOMAJI WANGU, na usisahau kumsoma pale kwa dada Koero( huyu naye subiri simulzi zake nimekuandalia ndugu msomaji na nitajibu maswali ya wanablogu fulani walioniuliza kuhusu YASINTA na hata huyu Koero) sawa? we tulia tuuuuuu Mwisho wa juma mwema!!! NA TUONANE TENA JUMATANO IJAYO!!!!

Tuesday, September 20, 2011

KUMBUKUMBU YA MAREHEMU BIBI YETU VALERIANA NGONYANI!!!

ILIKUWA MARA YANGU YA MWISHO

KUONANA NA BIBI 2005 MWEZI WA NNE

Leo ni tarehe 20/9 ni miaka mitano na miezi minne imepita tangu bibi yetu mpendwa Valeriana Ngonyani atutoke.Alifariki 20/5/2005 katika hospitali ya Liuli. Sisi wajukuu wako wote, watoto wako ndugu na marafiki wote wanakukumbuka daima. Bibi Valeriana ni huyo aliyejifunika kitenge, katikati nadhani mnajua au basi ni mimi na mwishoni ni mama yangu mdogo, mdogo wa mama. TUTAKUKUMBUKA DAIMA KWA NJIA YA SALA ZETU. USTAREHE KWA AMANI AMINA.

Monday, September 19, 2011

MIAKA 50 YA UHURU TANZANIA

NGOJA TUANZE WIKI NA WIMBO HUU!!!

SWALI HIVI TUPO HURU KWELI? NA KWELI TUNA AMANI ? HAYA JUMATATU NJEMA NDUGU ZANGU.....

Sunday, September 18, 2011

NAPENDA KUWATAKIENI WOTE JUMAPILI HII KWA SALA HII!!!!

Mdada akiwa Silver Sands
Mungu nakuomba unisaidie niwakumbuke wenye njaa ninapokuwa na chakula, wagonjwa nianpokuwa na afya nzuri, wote wanaoteseka kwa sababu ya vita ninapokuwa na amani, wasio na nyumba ninapokuwa nimelala na pia kuwa ndani ya nyumba yenye joto, pia nakuomba unisaidia niwakumbuke yatima kila ninapokuwa na wazazi wangu.

Na pia nakuomba:Bikira Maria mama wa msaada na uibariki familia yangu, kaka zangu, dada zangu, wazazi wangu na watu wote dunia hii katika dhambi: AMINA

Tumalizie kwa wimbo huu kwa ajili ya maombolezo ya wenzetu waliotutangulia ..NJIA YETU NI MOJA...

Saturday, September 17, 2011

UJUMBE WA JUMAMOSI YA LEO!! MATATIZO KATIKA MAISHA!!

Ujumbe huu wa leo naambatanisha na wimbo huu wa Dogo A Matatizo:-(Ulijua kwamba:- Matatizo ni mazuri kwa vile hukufanya uwe mbunifu. Pili huwezi kukwepa matatizo kama unaishi hapa duniani. Matatizo ni sehemu ya maisha, tatizo kubwa linakuja jinsi unavyoliona tatizo, ukiliangalia tatizo tofauti basi tatizo huwa kubwa zaidi na ukiliangalia tatizo kama sehemu ya ufumbuzi au ubunifu au hamasa ya kufanikiwa na kupiga hatua basi ukipata tatizo badala ya kulalamika na kuona unaonewa utachangamka na kuanza kushughulikia. Nahisi matatizo yangu ninayokutana nayo ni makubwa kuliko yako ila naamini yangu ni yangu na nikiyashinda tu nitakuwa mbali zaidi na nitakuwa mtu wa mafanikio.
Mara nyingi matatizo nayo huwa yanazalisha stress sana kwa hiyo inabidi daima uwe imara kuyatatua lakini siyo matatizo ambayo yanakufanya uumie huku wanaokuumiza hawana chembe ya haki ya kukuumiza angalia usianguke.

Friday, September 16, 2011

BREAKING NUUUUUUUUUUUUUUUUZ: SOKO KUU LA SIDO JIJINI MBEYA LINATEKETEA KWA MOTO HIVI SASA

Hii ni hatari jamani
Kaka Selafim Ngonyani akiwa kwenye ofisi yake na wajomba zake pia dada yake ilikuwa mwaka huu 2011 mwezi wa sita mwishoni

Nimepata na mstuko .Muda si mrefu nimepata habari kutoka kwa kaka yangu hapo kwenye picha mwenye shati nyeupa..kuwa ofisi yake imeungua moto...ila amebahatika kuokoa baadhi ya vitu. Na yeye mwenyewe yupo salama..Hapo ilikuwa mwaka huu nilipokuwa nyumbani tulipita Mbeya mpaka hapo Ofisini kwako yeye ni Fundi viatu...habari zaidi unaweza kusoma hapa na hapa

KARIBUNI KIKOMBE CHA CHAI...NINYIME VITU VYOTE LAKINI SIO CHAI!!!


You´re Just my Cup of Tea,

Our Love Warms my Heart.

Najua wote mnajua mie ni mpenzi sana wa chai tena ile isiyo na sukari(Chingambu) :-).

Kichwa cha habari hapo juu kinasema kuwa "NINYIME VITU VYOTE LAKINI SI CHAI" Duh ! naungama ni kwamba nimesema uongo kwani mimi ni mdhaifu/mpenzi sana wa smaki pia kama ilivyo kwenye chai......Ngoja tusikilize wimbo huu wa Nuru ft Mr Chocolate Flavour - Muhogo Andazi!!!
NAPENDA KUWATAKIENI WOTE MWANZO MWEMA WA MWISHO WA JUMA ....MUWE NA AFYA NJEMA , AMANI NA FURAHA ZITAWALE NYUMBANI MWENU/WAKO.......IJUMAA NJEMA!!!!

Thursday, September 15, 2011

KUMBUKUMBU NILIPOKUWA MDOGO/KACHIKI!!!

Mti wa mbura ukiwa na matunda yake bado mabichi

Leo nimekumbuka nilipokuwa kabinti kadogo (kachiki). Wakati huo nikiishi Lundo kando ya ziwa nyasa. Lundo kwa asili kuna miti mingiii sana ya mibuni/mbura, hii ni aina ya miti inayozaa matunda madogomadogo ya njano.

hapa zikiwa zimeiva tayari


Matunda haya huliwa kama yalivyo, pia nakumbuka tulikuwa tukiyatwanga kwenye kinu ili kupata urahisi wa kupata juice yake ambayo ni tamu haswa.
Pia hizi mbura zikikauka ni karanga tamu sana zipo ndani yake. Namna ya kuzipata hizo karanga hizo, ni kwamba:- unaweza kuzibangua kwa kutumia shoka, au jiwe (kienyeji).
Sasa siku moja mchana, kama sikosei hata shule nilikuwa sijaanza maana nilikuwa bado kachiki, lilinitokea tukio ambalo kamwe sitakuja kulisahau katika maisha yangu.
Naomba muungane nami katika simulizi ya mkasa huo, maana naona mnaanza kujiuliza ni nini kilimtokea binadamu huyu?
Ilikuwa hivi…….Nilikuwa na rafiki yangu aitwaye Puna Mahecha, huyu alikuwani shoga yangu hasa maana tulikuwa kama Kurwa na Doto. Basi Bwana, siku hiyo ya tukio, nakumbuka ilikuwa ni baada ya kuushindilia Ugali kwa Samaki na Matembele, tukatoka na shoga yangu kwenda kutafuta hizo Mbura. Sasa baada ya kukusanya Mbura zetu za kutosha, si mnajua mambo ya kitoto, tukaanzisha mchezo wa kulenga shabaha kwa kutumia zile Mbura ili kupima kama ni nani mwenye shabaha zaidi ya mwingine. Tukawa tunawekeana zamu………Puna-Yasinta, Puna -Yasinta nadhani tulifanya hivyo zaidi ya mara mia moja.
Ikafika zamu yangu tena, mara hii Puna akalenga bwana… Tapu……... Weee bwana wee kulichirizika damu.! Hapo ujanja wote ukaniishia na kilio kikawa kikubwa kweli. Bahati mbaya zaidi ilikuwa ni mkono wa kulia. Kwa hiyo sikuweza kula ugali kwa siku kadhaa kwa kutumia mkono huo. Sijui kama ningekuwa nimeanza shule ingekuwaje?...Nimekumbuka kisa hiki kwa vile nilikuwa nafanya kazi fulani nikajitonesha na kuhisi maumivu……….Mweh…hata baada ya miaka yote hii? Kweli michezo ya utotoni ina raha na hasara zake.Puna kama upo popote pale na unasoma simulizi hii nitafute rafiki yangu. Nitafurahi sana. Rafiki ni bora kuliko Mwanasesere.

KUSAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO UBALOZINI SWEDEN!!!


THE EMBASSY OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

SIGNING OF CONDOLENCE BOOK

The Embassy of Tanzania in Sweden will open a book of condolences following the tragic ferryboat accident that occurred in Zanzibar on Saturday, 10th September, 2011.

The book of condolences will be open for signature at the Embassy of Tanzania, Näsby Allé 6 183 55, Täby on Friday, 16th September, 2011 from 2:00pm to 6:00pm and Saturday, 17th September, 2011 from 11:00am to 16:00pm.

---------------------------------------------------------------------------------------------

KUSAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO

Ubalozi wa Tanzania hapa Sweden utafungua kitabu cha maombolezo kufuatia ajali ya kuzama kwa meli iliyotokea Zanzibar siku ya Jumamosi tarehe 10 Septemba 2011.Kitabu cha maombolezo kitafunguliwa kwenye Ubalozi wa Tanzania, Nasby Allé 6 183 55, Täby siku ya Ijumaa tarehe 16 Septemba, 2011 kuanzia saa 8 mchana mpaka saa 12 jioni na Jumamosi kuanzia saa saa 5 asubuhi mpaka saa 10 Jioni.

Wednesday, September 14, 2011

JUMATANO YA KIPENGELE CHA MARUDIO LEO HII TUWE NA HUYU DADA NA MITINDO YAKE:- UKIJIPENDA MWENYWE NA WENGINE WATAKUPENDA=MAISHA

Ndiyo, ndiyo! Ndugu wasomaji wa blog ya Maisha na Mafanikio kile KIPENGELE chetu cha marudio ya mada, picha, au nisema MATUKIO MBALIMBALI ambayo huwa kila JUMATANO...leo nimeona tuangalie picha hizi za huyo madada. Ambazo tulishawahi kuziona hapa. Ila leo ana swali moja maana si mnajua huyu ni Kapulya...Je ni picha gani wewe imekupendeza? unaweza kutoa sababu pia.:-)

Hapa mwanadada ametinga kimgolole/kimasai.


Hapa nilikuwa nafikiria nifunge mtindo upi? Kabla sijaamua picha ikapigwa...kaaziii kwelikweli!!!
Hapa nikaona nikumbuke nilipokuwa mdogo maana nilikuwa napenda sana kufunga nguo (Lubega) shingoni. Lubega na ndala si mbaya au mnasemaje.... Ahsanteni wote TUONANE TENA JUMATANO NYINGI /IJAYO KATIKA KIPENGELE CHETU HIKI CHA MARUDIO YA MATUKIO MBALIMBALI!!!!!

Tuesday, September 13, 2011

KISA CHA KOMBA NA AKINA KOMBA!!!!!

DADA YASINTA!
LEO NI KUPE KILE KISA CHA RAFIKI YANGU AITWAE FULKO KOMBA NA WATANI WAKE AKINA NJAIDI NA MASASI HAWA KAMA MAJINA YAO WOTE NI WATOKA KUSINI MWA TANZANIA MASASI NA RUVUMA HAWA NI WATANI WA JADI HALISI,.BASI SIKU MOJA HUKO ZAMCARGO KURASINI SASA MJI HUU UMEVUNJWA NA KUPISHA MRADI WA UPANUZI WA BANDARI. ILIKUWA SIKUKUU YA KRISMASI, KWA KAWAIDA HAWA AKINA KOMBA WALIKUWA NA KIKUNDI CHAO CHA NGOMA YA HUKO NYUMBANI SONGEA. HAWA WANATOKA PALE NJIA PANDA YA SONGEA NA PERAMIO KAMA UNAKWENDA CHIPOLE. JINA LIMENITOKA KIDOGO NIKIKUMBUKA NITAKUTAJIA .,BASI KILA MWISHO WA MWAKA AU KRISMASI HUWA WANAPIGA NGOMA ZAO NA WANAKESHA .BASI ...BWANA ..MWAKA HUO MKESHA ULIKUWA NA MVUA NYINGI KIASI KUWA MPAKA SAA TISA USIKU
WATU WALIKUWA WAMELALA, ILA KWA HAWA JAMAA WA MASASI KULIKUWA NA KIGROSARI NA KULE KURASINI KULIKUWA NA SIFA YA KUUZA MAFUTA YA MAGENDO YAANI PETROLI AU HATA MAFUTA YOYOTE HATA YA KULA ILIKUWA NI DILI. VIJANA WA KILEO NDIYI LUGHA YAO, BASI HAPO KWA MASASI WALIKUWA WALEVI WOTE NDIYO KISEBULE CHAO HATA USIKU WE GONGA TU NATAKA BIA UNAFUNGULIWA.
NA UNAPEWA UNACHOTAKA KWANI SIKU DILI IKIKUBALI BASI HAPATOSHI. KWAHIYO SIKU HIYO WATU WALIKUNYWA MPAKA MANANE. NA UJUWAVYO MLEVI ANAPOKUWA AMEPATA MARA ATOKE KWENDA HUKO MARA KULE BASI NJAIDI ALIKWENDA KUFUATA SIGARA PALE ZILIISHA , ALIPOTOKA MBELE KIDOGO ALIKUTA MNAZI, NA KUKUTA KINYAMA KOMBA ,, KINAPUMUA KWA MBALI ... KIMELALA ..BASI ALIRUDI NDANI NA KUWAAMBIA KUWA JAMANIEEE KOMBA KALALA PALE ,KOMBAAA,,,, NDIYO KOMBAA ANAUMWA AU ,,,JAMAA AKAJIBU SIJUWIII...TWENDE .. WAKAENDA KUMWONA WAKAKUTA KALE KANYAMA ..BASI MMOJA WAPO AKAWAAMBIA WALE WENZAKE KWAVILE HUYO KOMBA NA NDUGU ZAKE WAPO KARIBU BASI TWENDE ZETU TUKAWAAMSHE WAMPATIE MSAADA ,AU SIYO JAMANI.EEE WAKA JIBU ,,SAWAAA BASI WOTE WALE VIJANA WA MASASI WAYAO WAKAENDA KWA WANGONI ,,,NGOO NGOOO HODI ...MLANGO,,, NANI WEE ... AKASEMA ALOO KOMBA, FUNGU ...NDUGU YENU KOMBA KALALA PALE HAJIWEZI ,,,AKAULIZA KOMBAAA... NDIYO
YUPO WAPI ,,,PALE KWENYE MNAZI ,,,,,YEYE BILA KUHOJI ZAIDI AKAENDA KUMWAMSHA FULKO, NA NDUGU YAKE BOSCO WAO NAE AKAMFUATA THEO ILA KWAKUWA ENEO LILE WALIKUWA FAMILIA ILE WANAKAA PAMOJA WAKASEMA BASI TUKAMWAMSHE MUJESHI ,,KAKA YAO ,HUYU ALIKUWA MWANAJESHI ,BASI WOTE TIMU MZIMA WALIONGOZANA NA WALE VIJANA MPAKA PALE ALIPOLALA KOMBA ,..YUPO WAPI???? ...SWALI .. HUYU HAPA,,,, WAKAONYESHWA KOMBA MNYAMA, NDIYO HUYU?? ..NDIYO ,,,,,,HUYU NDIYO ,,,,,,,,,,,,
KWANI HUYU ANAITWA NANI??? WOTE WAKAJIBU KOMBA .........BASI NDIYO HUYO NDUGU YENU ,,,,,,,,,,WALE WAYAO WAKAONDOKA NA KUIACHA TIMU MZIMA YA WANGONI NA MAJINA YAO YA WANYAMA NA NDUGU YAO KOMBA MLEVI WA TEMBO,...... KUMBE KOMBA ANAKAWAIDA YA KUPANDA JUU YA MMNAZI NA KULINYWA TEMBO LA MNAZI HIVYO NAE SIKU ILE ALIBAHATIKA KUPATA POMBE YA MNAZI AKASHEREHEKEA VIZURI SIKUKUU YA MWAKA MPYA NA KUWAFANYA NDUGU ZAKE AKINA KOMBA WAACHE VITANDA VYAO NA KWENDA KUMWANGALIA NA KWAMAWAZO YA WANGONI KWANI WALIPOSIKIA KOMBA KALA WALIJUA KUWA NDUGU YAO KOMBA
AMEPIGWA BILA KUCHUNGUZA NI KOMBA GANI ??? HUYO ,
HIVYO NDICHO KISA CHA KOMBA NA AKINA KOMBA
NA IPO SIKU ITATOKEA KISA KAMA HICHO CHA NYANI NA AKINA NGONYANI................KWANI HAKUNA MAJINA YOTE YALIISHA ,,,,,,,,,,,, KOMBA, NYOKA , NDANDALA, MAPUNDA.,,,N.K POLENI WATANI ZANGU WA PALE LIPOKELA KITAI , NTYAN"GIMBOLE, LIPUMBA MATILI, HALALI PALE KIGONSERA , NGOMBO AU MBAMBABAY POLE KILOSA AKINA NCHIMBI ,MBUNDA KULE UMATENGONI
ASANTE MIMI MYAO SIYO MUYAO MAANA KWETU PALE NI MUHOGO UNAITWA MAYAO YAKIWA MENGI
HUU NI UTANI WA MAKABILA MAJINA NILIYO TUMIA NI YA KWELI YAWATANI ZANGU ILA HAIKUWA HIVYO NA WALE WA MASASI NI BINAMU ZANGU KWELI WANAITWA MAJINA HAYO.

-------------------------------------------------------------------------------------------------

KISA HIKI NIMETUMIWA NA MSOMAJI WA MAISHA NA MAFANIKIO KWA JINA LA ISSACK CHE JIAH KWA VILE ALIONA JINA LANGU NI NGONYANI AKAPENDA "KUNITANIA" NAMI HUWA SIPENDI KUFAIDI MAMBO KAMA HAYA PEKE YANGU NIKAONA NIWEKE HAPA ILI NANYI WENZANGU MFAIDI.

Harambee nchini Uingereza kuchangia wahanga wa Zanzibar!!!

http://www.youtube.com/watch?v=QGZFnZXAGvY

Jumuiaya ya Watanzania nchini Uingereza TANZ-UK ikishirikiana na TANZ-UK Jumuiya ya Wanzanzibar waishio Uingereza (ZAWA) Urban Pulse na Miss Jestina George Blog imeandaa fundrising maalum kwa ajili ya kuweza kuwasaidia waathirika wa ajali ya meli ya Spice Islander iliyotokea Nungwi njiani kuelekea Pemba. Fundrising hii itafanyika katika Ubalozi wetu hapa London tarehe 17 Septemba 2011 Kuanzia saa nane mchana.


Tunawaomba Watanzania wote mlioko hapa nchini Uingereza kutoka jumuiya mbalimbali,vyama vya kisiasa, wafanyabiashara, wanafunzi na hata wasio Watanzania mjitokeze kwa wingi ili kuweza kujumuika nasi na kufanikisha zoezi hili. Hivyo basi tunaomba mwenye fedha au chochote kile cha kuweza kuthamanishwa tunaomba tuweze kuja nacho na kitafanyiwa mnada. Mfano, wenye biashara wanaweza wakaleta bidhaa kiasi ambazo zitafanyiwa mnada ambapo ziada itakayopatikana itakuwa sehemu ya mfuko tutakaokuwa tunautafuta.


anwani ni; 3 Stratford Place, London, W1C 1AS. Muda ni saa nane mchana (2pm sharp).

Kwa maelezo zaidi tunaomba uwasiline na ............... Mwenyekiti Tanz-UK 07766856565, ZAWA 07538063536,TA London 07404332910


UKIONA TANGAZO HILI TAFADHALI MTAARIFU NA MWENZAKO. WOTE TUNAKARIBISHWA,


Mungu ibariki Zanzibar, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Africa . Zaidi sana Mungu wabariki Watanzania wote popote pale walipo duniani.


ASANTENI

MWENYEKITI,

TANZ-UK-Monday, September 12, 2011

NI JUMATATU NYINGINE TENA NA JUMATATU HII KUNA UJUMBE WAKE

Jumatatu yangu meanza safi sijui wewe mwenzangu ebu tumsikiliza Juma nature na wimbo huu wa kila siku za wiki ni mikikimikiki

Jumatatu njema

Sunday, September 11, 2011

Taifa Msibani, Umoja wetu na Utu wetu shakani - Zitto


Ndugu zangu salaam kwenu,naomba mnifikishie ujumbe huu kwa watanzania. Natanguliza shukrani zangu za dhati.
(Nimeandika makala hii nikiwa katika Benchi la Hospitali ya Mnazi Mmoja hapa Zanzibar. Mniwie radhi kama kuna spelling mistakes kwani nilitaka hisia zangu ziwe as raw as possible - Zitto Zitto and not Zitto a Politician).

Jana asubuhi tarehe 10 Septemba 2011 Taifa liligubikwa na habari za kushtusha za maafa. Mwanzoni taarifa zilisambaa kwamba zaidi ya watu 2000 walikuwa kwenye Boti MV Spice Islander lililopinduka na kuzama mbele kidogo ya Nungwi likielekea kisiwani Pemba. Habari hazikuwa za uhakika sana kwani vyombo vyetu vya habari na hasa Televeshini ya Taifa havikuwa vikitoa habari juu ya ajali hii.

Habari zilisambaa kupitia mitandao ya intaneti na kufuatia uchu wa habari nilianzisha #ZanzibarBoatAccident katika mtandao wa twitter ili tuweze kufuatilia kwa karibu habari zote za ajali hii.
Habari zilisambaa kuwa Televisheni ya Taifa ilikuwa inaonyesha muziki wa Taarab na Baadaye vipindi vingine vya kawaida bila kutoa habari kwa Umma kuhusu msiba huu.

Watanzania waliokoa wakiwasiliana kupitia twitter na facebook walikuwa na hasira sana na kituo cha TBC1 kutoonyesha au kupasha habari juu ya ajali hii. Mpaka saa moja jioni kituo hiki cha Televisheni ya Taifa kilikuwa kinaonyesha watu wakicheza muziki wa Kongo, wanawake wakikatika viuno na hata ngoma za asili.

'Hallo, washa TBC1 uone Televisheni yenu inachoonyesha' yalikuwa ni maneno ya Mwakilishi Ismael Jussa Ladhu aliponipigia kuonyesha kusikitishwa kwake na kituo hiki. Mpaka jioni tulikuwa tumepata taarifa kuwa Watanzania wenzetu 198 walikuwa wamepoteza maisha. 570 hivi walikuwa wameokolewa.

Binafsi nilipotembelea Hospitali ya Mnazi Mmoja niliweza kumwona Binti aliyeitwa Leyla, akisoma darasa la Nne huko kisiwani Pemba. Leyla alipona, aliokolewa. Nilimwambia leyla atapona na kurudi Shuleni. Mpaka ninapoandika tumeambiwa kuwa Watanzania 240 wamegundulika kupoteza maisha na zaidi ya 600 wameokolewa.

Napenda kuwapongeza sana waokoaji wetu, wavuvi wa kijiji cha Nungwi na vijiji jirani, wamiliki wa mahoteli waliojitolea vifaa vyao kwenda kuokoa watu na wanajeshi wetu wa majeshi ya ulinzi na usalama kwa kazi hii kubwa ya kuokoa. Kwa kweli tumeokoa watu wengi kuliko ilivyotarajiwa. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imejitahidi sana, ilitulia na kuonyesha uongozi dhabiti katika juhudi za uokoaji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akafuta ziara yake huko Canada, ziara iliyokuwa imeandaliwa muda mrefu na kwa gharama. Lakini Rais aliona ni vema kupata hasara kuliko kuwa nje ya Nchi kipindi hiki. Hakutaka hata kumtuma Makamu wa Rais au Waziri Mkuu. Alifuta. Akatangaza siku 3 za kuomboleza.

Hata hivyo waandaaji wa Miss Tanzania waliona hasara kubwa kuahirisha shindano la Urembo usiku huo. Wangepata hasara! Hata wafadhili wao Kampuni ya simu za mkononi ya vodacom ambao miongoni mwa waliofariki wamo wateja wa vodacom, waliendelea na shindano hili. Jumatatu, tarehe 12 Septemba 2011 ni siku ya khitma ya kuwaombea marehemu wetu.

Nimeamua kutotumia simu ya ngu ya Voda kwa siku nzima, sina njia ya kuiadhibu Kampuni hii isipokuwa kugoma kutumia simu yao japo kwa siku moja kuonyesha kutoridhishwa kwangu na uamuzi wao wa kutojali msiba huu kwa Taifa.

Misiba huweka jamii pamoja. Msiba huu uliotokea Zanzibar ni jaribio kubwa kwa Umoja wa Taifa letu. Shirika la Utangazaji la Taifa limeshindwa jaribio hili la kudhihirisha Umoja wetu katika kipindi hiki. Nataraji wakubwa wa Shirika hili linaloendeshwa kwa kodi watawajibika au kuwajibishwa!

Jumla ya Majeruhi na marehemu sasa inafikia zaidi ya Abiria 800! Asubuhi ya jana 10 Septemba 2011 tuliambiwa na Serikali kwamba uwezo wa Boti la MV Spice Islander ilikuwa ni abiria 500 na wafanyakazi 12. Pia tumejulishwa kuwa boti hili lilikuwa la Mizigo na sio la Abiria.

Natumai mara baada ya kumaliza maombolezo haya ya siku tatu Wakuu wa Mamlaka zinazohusika na usafiri wa Majini wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar watawajibika au kuwajibishwa. Mkuu wa Bandari ya Zanzibar Mustafa Aboud Jumbe na Waziri wa Miundombinu Hamad Masoud wanapaswa kufukuzwa kazi mara moja kama hawatawajibika wenyewe kwa kujiuzulu.

Kufukuzwa kwao kazi hakutarudisha ndugu zetu duniani bali itakuwa ni somo kuwa hatutarudia tena kufanya makosa yaliyoleteleza ajali kama hii.

Mwenyezimungu atupe subira wakati huu wa msiba mkubwa katika Taifa letu. Alaze roho za marehemu wetu mahala pema peponi na awape unafuu wa haraka majeruhi wetu.

Zitto Kabwe.

JUMAPILI YA LEO TUWAOMBEE MAREHEMU WOTE KWA SALA HII!!

Baba yetu uliye Mbinguni,
Jina lako litukuzwe,
Ufalme wako ufike,
Utakalo lifanyike ,
duniani kama Mbinguni.
Utupe leo mkate wetu wa kila siku,
Utusemehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea.
Usitutie katika vishawishi, lakini utuokoe maovuni.
(Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele Amina)

Pia Mwenyezi Mungu twakuomba uwape nguvu wafiwa waliowapoteza ndugu zao jana, katika meli iliyotoka UNGUJA kwenda PEMBA ambayo imezama jana. Uwalaze mahali pema PEPONI marehemu hao.AMINA. TUPO PAMOJA!!

Saturday, September 10, 2011

poleni sana ndugu zetu wa zanzibar kwa msiba huu mkubwa!!!

Meli ya Mv Spice iliyokuwa ikitokea Pemba kuelekea Unguja imezama usiku wa leo maeneo ya Nungwi ikiwa na abiria wanaokadiriwa kufikia zaidi 1000, wengi wao wanaofiwa kufa maji.
Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari, vinasema meli ilikuwa imepakia mizigo na nabiria kuliko uwezo wake.
Poleni sana ndugu zetu wa Zanzibar, Mwenyezi Mungu awape moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu cha majonzi, zaidi tuzidi kumuomba yeye ili manusura wengi wapatikane. Ameeni
picha na maelezo toka hapa.

Friday, September 9, 2011

CHAKULA CHA MCHANA WA IJUMAA YA LEO...KARIBUNI TUJUMUIKE NDUGU ZANGUNI!!

Ni kawaida yetu kila Ijumaa kufanya manunuzi ya chakula kwa wiki nzima. leo nilipokuwa dukani nikakuta mahindi haya . Sikuweza kuyaacha nikayanunua ili yawe mlo wa mchana . Hapa nimeyaandaa tayari kwa kuyachemsha......


.....na hapa ndipo tayari nimeyapanga kwenye sufuria na yanachemka taratibu...
......dakika kumi baadaye walaaaa... mahindi tayari yameiva na sasa.......
.....mwanadada kwa raha zote anatengeneza barabara ya kwenda Afrika....nadhani wote mnakumbuka mchezo huu wa kula mahindi. Yaani enzi hizo miaka orobani na saba wakati wa utoto . Kaka, dada au hata baba au mama wakati wa msimu wa mahindi kulikwa na msemo au mchezo wakati mkila mahindi basi wanasema "leta muhindi wako nikutengenezee barabara ya kwenda LITUMBANDYOSI". Na kwa akili ya utoto basi unampa tu kumbe mwenzako yale mahindi anakula na anakuachia mistari miwili tu...hahaaaaaa!! leo nimekumbuka mbali kweli. KARIBUNI JAMANI NA IJUMAA NJEMA PIA:-)

Thursday, September 8, 2011

MATITI NI CHAKULA CHA MTOTO AU?

Sijui kwa ajili ya kukosa watoto au Kweli huu ni UUNGWANA kweli kumnyonyesha mbuzi?Na huyo naye anamnyonyesha mtoto wa ndama kisa? Sijui akimngáta hapo atasema nini?
Hapa sawa, mama akimpa mtoto chakula ambacho ndicho chakula bora sana kwa watoto wachanga. Ila kuna simulizi nimeisikia kuwa, wanaume wengi huwa wanaona WIVU sana wakati mama/mke wake amnyonyeshapo mtoto. Hasa mtoto wa kiume. Sijui wenzangu nanyi mmewahi kusikia? Na kama kweli kwanini sio anyonyeshwapo mtoto wa kike?

Wednesday, September 7, 2011

Made in Mbinga: Kijana wa Kitanzania mwenye elimu ya darasa la saba afanya uvumbuzi, atengeneza magari manne kwa kutumia vipuri vya pikipiki na vyuma

Katika pitapita nimekutana na habari hii ya kufurahisha na nikashindwa kuiacha nimeipata hapa

Moyo wangu!!

Kama kawaida yetu na bila kusahau leo ni ile siku ya KIPENGELE chetu ambayo hutujia kila JUMATANO na leo siku hii inawapelekeni mpaka hapa kwa diwani ya fadhili....karibuni sana..


Usiuache mpweke, maumivu kuufika,
Siufanye uteseke, machozi yakanitoka,
Ufanye ufarijike, upe moyo uhakika,
Moyo wangu.

Upatie unafuu, upunguzie mawazo,
Uweke daima juu, sikalie matatizo,
Siupige kwa miguu, na kuupa mizevezo,
Moyo wangu.

Uondolee karaha, siuweke taabuni,
Ufanye kuwa na raha, sizamishe majonzini,
Utawalwe na furaha, cheko tupu maishani,
Moyo wangu.

Usiutendee hivyo, moyo wangu taumia,
Ukitenda ndivyo sivyo, kitanzi utautia,
Vyovyote vile iwavyo, elewa wakuzimia,
Moyo wangu.

TUKUTANE TENA JUMATANO IJAYO KATIKA KIPENGELE CHETU HIKI.....KILA LA KHERI.

Tuesday, September 6, 2011

Monday, September 5, 2011

NANGOJA ANIUE, NIKIONDOKA WANANGU WATATESEKA!

Kama mnavyojua kuwa hivi karibuni nilikuwa huko nyumbani Tanzania, na nilikuwa pande za huko kwetu Ruhuwiko Songea ambapo nilikaa majuma kadhaa hivi.

Kusema kweli yapo mengi ya kushangaza, ya kutisha na yenye kufurahisha ambayo niliyashuhudia, na kusema kweli kuna mengi nimejifunza.Lakini labda niseme tu kwamba aina ya maisha niliyoyakuta huko kijijini, kwa kweli yalinipa picha kwamba bado kuna safari ndefu sana katika kuufikia ukombozi wa huyu kiumbe mwanamke.

Ninayo mifano mingi lakini tukio nililolishuhudia siku moja nikiwa katika matembezi yangu liliniacha mdomo wazi, na labda niseme kwamba limenikaa hadi leo akilini nikijaribu kuwaza na kuwazua lakini sipati jibu.

Sijui nianze vipi?...Ahh! Kuna siku katika matembezi yangu nikakutana na kundi la akina mama wamekaa wakipiga gumzo, lakini nyuso zao zilikuwa zimegubikwa na huzuni. Nilishikwa na tashwishwi, nikajongea pale walipo ili kujua kama kuna jambo gani limetokea kiasi cha kuwakusanya pale huku wakiwa na nyuso za huzuni.

Si mnanijua tena mie KAPULYA MDADISI. Nikawauliza, ‘jamanindugu zanguni, kulikoni mmekaa na nyuso za huzuni, JE KUNA MSIBA?’
Wote waligeuka kuniangalia, lakini walionekana kusita kunijibu, na ndipo mmoja wao akaniambia kuwa usiku wa jana kulitokea kutoelewana kwa wanandoa wanaoishi hapo mtaani kiasi cha mume kumpiga mkewe mpaka akapoteza fahamu.

Niliuliza sababu ya ugomvi wao, na ndipo nilipoelezwa kwamba, sababu kubwa ni kwamba wanandoa hao wana watoto wanne ambao bado ni wadogo na mume anataka kuongeza mtoto wa tano, lakini mkewe hataki kwa kuwa hali ya uchumi hairuhusu, na pia bado wanalo jukumu la kuwalea hawa watoto wanne ambao kwa kweli ni wadogo. Hata hivyo alimshauri mumewe wavute subira kwanza ili watoto hao wakue.

Mume hakukubali ushuri wa mkewe na ndipo ugomvi ulipoanza.Walibainisha kwamba ugomvi wao ni wa mara kwa mara na sababu kubwa ni hiyo ila ugomvi wa safari hii ulikuwa ni mkubwa na kama sio majirani kuingilia kati basi mume yule angemuua mkewe.

Nikataka kujua kama anapata kipigo cha aina hii kila mara kwa nini aisrudi kwao?
Wakanijibu kuwa, kwanza hana nauli ya kurudi kwao kwani si mtu wa Songea. Pili anaogopa watoto wake watateseka.

Mh! Nilishusha pumzi, ujinga gani huu. Hivi sisi wanawake ni nani ameturoga, yaani unakubali mtu anakutesa na kukunyanyasa kiasi chakutaka kukutoa roho lakini wewe umo tu! Ukiulizwa sababu unadai, eti watoto wangu watateseka!

Bado najiuliza hivi watoto wanne bado hawatoshi? Hili tukio kwa kweli nimekuwa nikijiuliza tangu nirudi huku Sweden, na mpaka leo sijapatajibu kwamba tatizo ni nini? Kutokuelewa haki zetu, ujinga au ni nini?

Pima-Maji Ya Mjengwablog; Nani Ataibuka Kidedea Igunga?

Kuna wagombea watatu wenye kuchuana vikali Igunga; Dr Peter Kafumu ( CCM), Leopard Mahona ( CUF) na Joseph Kashindye ( CHADEMA). Blogu yako ya Jamii Shirikishwa, Mjengwablog, imekuandalia Pima- Maji ili utoe maoni yako kwa kupiga kura. Zimebaki siku sita za kupiga kura. Swali ni hili; Je, ni nani ataibuka kidedea Igunga? Piga kura juu kulia kwenye http://mjengwa.blogspot.com

Sunday, September 4, 2011

Jumapili ya leo inatupeleka mpaka Mkoani Njombe katika Kijiji cha Uwemba/kanisa la Uwemba!!!

Hapa ni kanisa la UWEMBA. Kijijini Uwemba Wilayani Njombe.
Jengo hili ni sehemu ambayo mifugo ipo pia ni jikoni.

Na jengo hili ni sehemu ambayo mapadere wanapumzika pia ni sehemu ya kula chakula.
Duh! siku zinakimbia kwelikweli mara hii ni tarehe 5/9 ni jumapili ya kwanza ya mwezi huu kaaazi kwelikweli....JUMAPILI NJEMA WANDUGU:-)

Saturday, September 3, 2011

TUSISAHAU UTAMADUNI WETU. JE? UNAMTAMBUA HUYU ANAYEIMBA/CHEZA HAPA?
JUMAMOSI NJEMA. NA FURAHIA MAPIGO YA MZIKI HUU ....TUTAONANA BAADAYE KIDOGO:-

Friday, September 2, 2011

CHAKULA NILICHOANDAA na KULA JIONI LEO/IJUMAA HII KARIBUNI TUJUMUIKE!!

Kwenye sahani hii ni :- Wali (mchele wa kutoka nyumbani tena kule kunakosemekana ni mchele bora kuliko yote hasa Tanzania sio kwingine tena ni KYELA).... mshikaki wa kuku na kachumbali ..kitelemshio ni maji lakini usiogope kuna vinyaji vingine kwa anayependelea. KARIBUNI TUJUMUIKE ..JIONI NJEMA...

HAKUNA BINADAMU ALIYE MKAMILIFU!!

Habari jamani!
Leo nimeona si vibaya kama nikiongelea jambo hili, katika maisha kuna kupenda/kumpenda mtu na kuna kuchukia /kumchukia mtu. Yaani kumtendea mtu mema na kumtendea mabaya. Hii huwa inakuwa ni ngumu sana kwa sisi binadamu kusema /kutamka hili neno SAMAHANI/NISAMEHE. Basi mimi leo nimeona sina budi kuomba msamaha kwa yeyote yule ambaye nimemkosea/nilimkosea, nimemkwanza/nilimkwaza yule ambaye nilimwahidi jambo na sijaweza kulitimiza. Kwani naamini mimi pia ni binadamu na ni rahisi kukosa/kukosea. NISAMEHENI NDUGU ZANGUNI!
Habu TUENDELEE na WIMBO huu WA kaka BONNY mwaitege NISAMEHE....

TUPO PAMOJA DAIMA TUSISAHAU HILI NA WOTE MNAPENDWA!!!!IJUMAA NJEMA:-)

KARIBUNI KATIKA BLOG YA WANAFUNZI WOTE POPOTE TANZANIA (MATUKIO NA WANAVYUO)

Kwanza tunapenda kuwasalimu sana Ndugu walimu na wanafunzi na wadau wote mliopo popote nchini Tanzania na Duniani kwa ujumla, Kwa heshima na Taadhima tunapenda kuwatambukisha kwenu Blog mpya kabisa inayo kwenda kwa jina la MATUKIO NA WANAVYUO ambapo lengo kubwa ni kuwakutanisha wanavyuo wote Nchi nzima na kubadilishana mawazo pia kujua nini kinaendelea kila wakati kupitia mtandao huu, Hatuna mengi sana ya kuandika hapa kwa maana mtandao wenu unajieleza vizuri kabisa, pia mtandao huu ni wanavyuo wote waliopo vyuoni sasa na wale walio maliza pia ni wa watanzania wote kwa ujumla kwa maana kuna mambo yanayo wahusu na muhimu. Tunawaomba mpitie kila kona ya mtandao huu na kutoa maoni kama yapo nini kiongezwe ama kuboreshwa zaidi, Tunawakumbusha tena mtandao huu ni wako. sisi tunaongoza tuu kwa mawasiliano zaidi tutumie Barua pepe kupitia
( twanavyuo@live.com)tunatanguliza shukrani zetu pia atakae pata taarifa hii ampe na mwenzake
Asanteni sana.
Matukio na wanavyuo Crew

KUTEMBELEA MTANDAO HUU BOFYA HAPA http://tzwanavyuo.blogspot.com/

Thursday, September 1, 2011

Baada ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika​, je Tanzania inakuhitaj​i?

Mwaka 2011, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasherehekea miaka ya uhuru wa serikali ya Tanganyika, taifa lililomezwa April 26, 1964 baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kwa hesabu za haraka haraka utaona miaka hamsini ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaadhimishwa April 26, 2014. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar una faida na kasoro zake, lakini leo nitajadili mada inayouliza kuwa “baada ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika, je Tanzania inakuhitaji?”.

Magwiji na wataalamu wa falsafa ya imani duniani, wanatuaminisha kuwa hakuna nguvu inayozidi upendo, wakidadavua zaidi husema kuwa penye upendo uliopea Mungu yupo. Hata ukitafakari maisha ya mahusiano tunayoishi, huna budi kumpenda mtu kwanza kabla hujaenda mbele zaidi kumpa nafasi ya kuwa mwenzi wako wa ndoa, katika muktadha huo ni kawaida kumwona kijana mwanamke akitoka bara la Amerika kufunga ndoa na kijana mume toka Mwanza, vivyo hivyo haishangazi kuona vijana wakivuka bahari na mito, milima na mabonde kutoka bara moja kwenda bara jingine kutafuta mapenzi yanayojengwa na upendo.

Hakika upendo ni nadharia ambayo hakuna maelezo yanayotosha kuidadavua kwa kilele chake. Bila shaka yoyote upendo miongoni mwa Watanganyika na Wazanzibar ndio uliozaa taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa mtazamo wangu, upendo ule uliozaa muungano hapa Tanzania miaka 47 iliyopita, naona umepoa kama sio kufifia na kuchuja. Makala hii haitojadili nani amefifisha upendo huu hapa Tanzania.

Nakumbuka siku ile, taifa lilipotangaziwa kuhusu afya ya baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, kuwa hali yake sio nzuri, Watanzania tuendelee kumuombea, mwili ulinisisimka kwa hofu. Nikapata baridi na hofu kuu, maswali mengi yalinikaba hasa nikijiuliza, itakuwaje nchi yangu bila “a great man, father of the nation?”. Hakika Mwalimu Nyerere alikuwa “great man”. Hata viongozi waliomzunguka wao pia walikuwa “great people”. Watanganyika hawa “great people” kizazi chao shurti kiwe “great generation”.

Wahenga walipata kusema kuwa “macho ni dirisha la fikra na ujasiri alionao mtu”, ukweli huu nauona kila ninapowatazama machoni Watanganyika nami nawaona kuwa na “great people”. Ujasiri huu tulionao hausemwi sana siku hizi, hivyo ipo haja ya kufanya kampeni ya makusudi miongoni mwa vijana wa Kitanganyika, hivyo upatapo fursa ya kushikana mkono na rafiki yako, vema ukamtazama machoni kwa walau dakika moja, kisha umwambie “you are a great person” kwa vile kila Mtanganyika ni kizazi cha “great people” ambacho ndio kiliasisi taifa la Tanganyika linalotimiza miaka 50 ya Uhuru tarehe 9 Desemba mwaka 2011.

“Great people” wale wakiongozwa na “great man” Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere walifanikisha kujenga misingi ya Taifa la Tanganyika na kufanikisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964, kwa vile upendo baina yao ulipea, vivyo hivyo waliipenda nchi yao na watu wake. Ukweli ni kuwa Watanganyika ni "great people", japo utamaduni wa kuambiana ukweli huu haupo tena nchini Mwetu. Nasisitiza kuwa Watanganyika ni kizazi cha “great people” kwa vile Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliweza kuwakaripia viongozi wa mataifa yenye nguvu za uchumi kama Amerika na Uingereza haya Israel pale alipoona matendo ya mataifa hayo yanaathiri kwa makusudi ustawi wa nchi zenye uchumi mdogo, kwa Mwalimu, kigezo cha ubinadamu hakikuwa uchumi bali ubinadamu wenyewe.

Mwalimu Nyerere hakuishia kukemea mataifa makubwa pekee, bali alikemea pia viongozi wa ndani ya Tanganyika ambao nia zao binafsi zilikuwa zinakinzana na maendeleo ya nchi yetu. Mwalimu hakusita kuanika udhaifu, uchafu na tamaa za viongozi hao na akasisitiza kuwa watu hawa wasipewe uongozi kwa hawana nia thabiti ya kuweza ustawi wa jamii ya Mtanganyika. Bila shaka yoyote, msimamo huu wa Baba wa Taifa ndio ulikuwa msimamo wa serikali yake yote, ndio ulikuwa msimamo wa viongozi wengine wote, Mwalimu Nyerere amekuwa “father figure” kwa viongozi wengi wa Tanganyika kwa kuwa na maneno machache na matendo mengi, nakumbuka tulipata kuwa na wimbo wa kusifia matendo ya Baba wa Taifa kuwa “Raisi wetu hapendi kusema, raisi wetu Nyerere baba, anaonesha mfano kwa vitendo”.

Mwalimu Nyerere alikuwa na shamba lake kule Butiama, shamba la Mwalimu lilikuwa mfano kwa wanakijiji wenzake, ukubwa wa shamba hili la Mwalimu haukuwa nusu ya ardhi ya kijiji, bali alichukua sehemu kidogo ili kila mwanakijiji mwenye nia ya kufanya kilimo naye apate ardhi. Hapa utaona fahari ya Mwalimu Nyerere haikuwa kujilimbikizia mali, ndio maana uwepo wa Tanzania ulimhitaji sana Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Swali linabakia, je baadhi ya viongozi tulionao ambao kujilimbikizia ardhi na mali kwa njia za ufisadi na kuuza mali asili zetu, Tanzania inawahitaji?

Kwa vile utamaduni wa kuambiana kuwa “sisi ni great people”, imekuwa kawaida kuona Watanganyika wa leo tunaishi kama pimajoto -thermometer- ambayo inabadilisha kizio cha joto kadiri unavyoiweka kwenye nyuzi joto tofauti. Ni kawaida kwa pimajoto kusoma nyuzi joto za juu ukiiweka kwenye mazingira yenye joto la juu, pia ni kawaida sana ikiwa pimajoto itatolewa kwenye mazingira ya nyuzi joto la juu na kuwekwa kwenye barafu itasoma nyuzi joto sifuri ama chini ya sifuri. Mfano huu unamaanisha kuwa Pimajoto inaathiriwa na mazingira, hali inayotokea sana kwa Watanganyika wa leo bila kujali elimu zetu, vipato vyetu ama namna yoyote ya uelewa uliokolea, tumekuwa tunaathiriwa sana na mabadiliko ya agenda ama mazingira, kwa mfano bei za bidhaa zinapopandishwa kiholela tunalalamika lakini hatuchukui hatua kukemea na kukomesha hali hiyo, zaidi tumekuwa ni walalamikaji tuliojaa woga wa kuuliza kwa nini hali ipo hivi, nashangaa sana tumekuwa sio “great generation” tuliozaliwa na “great people” chini ya uongozi wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ambaye agenda yake ilikuwa kukemea uoza huu.

Mwalimu Nyerere na Waasisi wa Taifa letu hawakuishi kama Pimajoto, fikra zao hazikubadilishwa na mazingira kama ilivyo Pimajoto bali wao ndio walipambana kubadilisha mazingira magumu waliyokuwa nayo wakati huo hawakukubali chochote kilichodhalilisha utu wao, kilichobeza ubinadamu wao ama kilichodidimiza ustawi wa Tanganyika ama Watanganyika. Kwa kutunza heshima na utu wa Mtanganyika walisisitiza sana elimu ya ujamaa na kujitegemea. Ukitazama wengi wa viongozi tulionao Tanganyika ya leo wengi wanaishi maisha ya Pimajoto, wanabadilika badilika ili kufanikisha nia zao binafsi zinazokinzana na mahitaji ya mustakabali wa Taifa letu Tanganyika, baada ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyija, Watanganyika tunaoishi maisha ya Pimajoto, Tanzania inatuhitaji?

Miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika imeshuhudia awamu nne za maraisi wa Tanganyika, huku awamu ya kwanza ikiongozwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, awamu ya tatu iliongozwa na Mzee Benjamini Mkapa na awamu hii ya nne usukani umeshika na Raisi Jakaya Kikwete. Katika awamu zote nne, serikali imepambana na changamoto mbali mbali za maendeleo, pia imetumia fursa nyingi za maendeleo ili kuwezesha maendeleo ya kiuchumi, kisisasa na ustawi wa jamii. Yatokanayo na jitihada hizi na changamoto zake sio muktadha wa makala hii.

Kwa makala hii, miongoni mwa maswali ya kujiuliza ni:- je serikali ikiwa ni mzazi wa kila Mtanganyika, inawapokea Watanganyika na matatizo yao na kuwaongoza kutatua shida zao? Kwa maana jitihada zilizofanywa na awamu zote, miaka 50 baada ya uhuru wa Tanganyika zimefanikiwa kiasi gani kutatua matatizo yanayokabili ustawi wa jamii ya Mtanganyika? Je, miaka 50 inatosha tu inaalika sherehe na karamu ya kujivunia uhuru ama ni fursa kwetu kutafakari wapi tulipojikwaa kama Taifa badala ya kulalamikia wapi tulipoangukia? Maana miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika haijatosha kutatua shida za msingi kama uhaba wa madawati mashuleni, uhaba wa madawa, vitendanishi tiba na watumishi hospitalini, kukosekana kwa nishati ya umeme ya uhakika na mambo mengine mengi.

Kwa bahati mbaya sana miaka 50 baada ya uhuru wa Tanganyika , taifa letu linashuhudia matumishi ya ujuzi na utaalamu wa baadhi ya viongozi wenye tamaa, ulafi na ubinafsi vikitumika kuzidisha umaskini miongoni mwa jamii kubwa ya Watanzania, je, Tanzania itakapofikisha miaka 50, hapo tarehe 26 April 2014 itakuwa bado inahitaji viongozi wa namna hii?

Nihitimishe kwa kusema kuwa, kila tunapotazama tulipotoka, hasa baada ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika, vema tukijua kuwa sisi Watanganyika ni “great people” mambo yaliyofanywa na waasisi wa Taifa letu ni mfano hai wa hiki ninachosema. Changamoto tuliyonayo leo hii ni kuishi maisha ya Pimajoto, ambayo ni kinyume na silika ya “great people” maana “great people” wote huwa wanabadilisha mazingara yao na kuyafanya kuwa bora zaidi kwa ustawi wa taifa lao na vizazi vijavyo. Serikali haina budi kusimamia sheria zake ili wajanja wachache wasitumie maarifa waliyoyapata kuihujumu serikali, badala yake wataalamu hawa watumike kusaidia kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Taifa, tukifuata njia hii ndiposa tutajibu hoja ya Miaka 50 baada ya uhuru wa Tanganyika, je Tanzania inanitaji?
Imeandikwa na,
Barnabas Mbogo.
Nyamagana, Mwanza
.

Picha ya wiki:- Kuelekea miaka 50 ya Uhuru!!!!
Sijui itakuwa hivi mpaka lini? Maana sasa tunaelekea miaka 50 ya uhuru lakini hali ni ile ile......sijui mwenzangu mnasemaje??