Tuesday, May 31, 2011

PAMOJA NA UBABE KUMBE HAWAJIAMINI!

Kwa utafiti wangu nilioufanya wanaume wengi hawajiamini katika nyanja za mapenzi na ni wakwepaji wakubwa wa kuwajibika fuatana nami ujue.
Ni wanaume wachache wanaoweza kuoa msichana aliyekwishazaa. Lakini pia ni wanaume haohao wanaowapa wachumba wao masharti ya kwamba mpaka ubebe mimba ndio nikuoe. Na wavulana pia hata kama yeye ni muhuni kupindukia atataka msichana atayemuoa asiwe na sifa ya kuchapa umalaya na hata akioa utasikia "usipoheshimu familia yangu tutakosana". Pamoja na mlolongo huo wote. Lakini kwa wanawake ni tofauti, wanawake wanajiamini sana katika mapenzi ndio maana pamoja na kuchagua wanaume watakaowaoa wao hujali zaidi, watathiminiwa kiasi gani? Mume awe ni mwizi, jambazi, mbeba zege au mfanya shughuli yoyote unayoiona ya hovyo. ATAMPENDA na KUMTHAMINI. JIFUNZE KUJIAMINI.

Monday, May 30, 2011

Swali/Fikirisho la jioni ya jumatatu hii:- UNAJUA/ULIJUA KWAMBA........

..........Wanawake ni wapesi sana kukumbuka sura za watu wengine kuliko wanaume? Hasa hukumbuka sura za wanawake wenzao. Je? Ni kwanini hasa?

BREAKINGNEWZZzz HALI SI SHWARI SEKONDARI YA TOSAMAGANGA IRINGA FFU WATUMIA MABOMU ..

Polisi wakiwaweka chini ya ulinzi wanafunzi eneo la Kitwiru nje kidogo ya na Manispaa ya ringa hapo ilikuwa ni kabla ya kuanza kupiga kurusha mabomu ya machozi.

Mwanakijiji kushoto akiwa na mwandishi wa habari wa Radio wa Ebony Fm wakifuta machozi kutokana na mabomu yaliyopigwa na askari na hao kuwatawanya wanafunzi hao.


Mwandishi wa habari wa Ebony FM akikimbia moshi wa mabomu ambayo yalikuwa yakipigwa na askari hao kutawanya wanafunzi hivi punde.


Wanafunzi wa Sekondari ya Tosamaganga wakikimbia moshi wa mabomu yaliyokuwa yakipigwa na polisi.


Hapa wakikimbia porini kunusuru afya zao chini ya vifaa vya wanafunzi vilivyotelekezwa


Hali ya usalama si shwari katika shule ya sekondari Tosamaganga wilaya ya Iringa mkoani Iringa hivi sasa wanafunzi zaidi ya 10000 wapo porini wakikimbizwa na polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia ambao wanatumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanafunzi hao ambao walikuwa katika maandamano ya amani kwenda ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa kuulalamikia uongozi wa shule hiyo.

Hadi hivi saa mabomu zaidi ya 10 ya machozi yamepigwa kuwatawanya wanafunzi hao ambao baadhi yao wanadaiwa kujeruhiwa kwa kuchomwa na miti wakati wakikimbia porini kukwepa mabomu hayo huku wananchi wa Mseke wakikimbia nyumba zao .

Polisi wamewazuia waandishi wa habari akiwemo mmiliki wa mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com ambao waliokuwepo eneo hilo wakifuatilia tukio hilo kuendelea kuchukua habari hiyo .
Picha na habari ni kwa hisani ya kaka Francis Godwin wa http://francisgodwin.blogspot.com/

Sunday, May 29, 2011

Na hizi ni zawadi nilizopata kwa siku hii ya akina mama!!!

zawadi kutoka kwa kijana Erik


Akisema:- Kwa mama,mama nakupenda, nakupenda kwa sababu wakati ninapokuhitaji upo. Unanisaidia, unapika chakula ktamu mmhh:-) nakupenda mama.Bila kupinga wewe ni mama bora.Mama wewe ni mwema, mwenye mawazo mazuri, mwenye furaha, mchekeshaji, cool, wewe ni bora na wewe ni wewe tu:-) HONGERA KWA SIKU YA MAMA NA WE NA SIKU NJEMA SANA YENYE FURAHA:-) NAPENDA KUKUKUMBATIA/Erik



Zawadi kutoka kwa binti Camilla na kijana Erik
Maneno hayohapo juu ya hiyo foronya ya mto yanasema hakuna kama wewe mama

Na hapa ni scarf:-) inapatikaka KappAhl



Camilla ametengeneza kwa mikono yake mwenyewe:-)



Na hapa ni zawadi zote nilizopata leo na nimekuwa na siku nzuri na nyenye furaha sana. Ahsante wanangu na pia Mume wangu kwa kuifanya siku hii ya MAMA kuwa njema.



NAWATAKIENI WOTE JIONI NJEMA NA NINA IMANI AKINA MAMA WENZANGU NANYI MMEKUWA NA SIKU NJEMA.

LEO NI JUMAPILI AMBAYO NI JUMAPILI YA KUSHEREHEKEA AKINA MAMA HASA HAPA SWEDEN: HONGERA KWA SIKU HII AKINA MAMA/GRATTIS PÅ MORS DAG!!!

Mama na wanae 12/7/2009

Kama kichwa cha habari kilivyosema hapo juu, leo ni siku ya kumsherehekea mama/ morsdag hapa Sweden. Nasi twapenda kumpongeza mama yetu ambaye ni mmiliki wa Maisha na Mafanikio. HONGERA MAMA KWA SIKU HII/GRATTIS PÅ MORS DAG. PIA HONGERA KWA AKINA MAMA WOTE, AKINA BIBI WOTE, shangazi na PIA AKINA BABA kwa uwepo wenu. Kwani Ninyi ni watu muhimu sana. Ni sisi Camilla na Erik.
-------------------------------------------------------------------------------------------------
SABABU KUBWA YA KUSHEHEREKEA SIKU YA MAMA/MORSDAG
Tarehe 29/9 ni siku ya akina mama hapa Sweden. Ni mila na desturi ya miaka mingi ambayo ilitokea na iliingia tangu maka 1919.
Siku hii ya mama/akina mama ni sikukuu muhimu inayoadhimishwa kila tarehe 29/5 hapa Sweden.
Hapa Sweden, kama nchi nyingine nyingi, siku hii ni maalum kwa akina MAMA. Kwa kupewa zawadi, maua na muhimu ya yote UPENDO.

Hapa Sweden siku hii inaangukia kila mara JUMAPILI ya mwisho ya mwezi huu wa tano na inasemekana mfumo huu umetokea USA.
Siku ya akina mama ilianzishwa huko Philadelphia 1908 na Anna Jarvis. Ilikuwa mwaka moja baada ya mama yake kufariki, Anna Jarvis, alikuwa amemkumbuka mama yake kwa misa. Siku iliyofuata habari zilienea haraka sehemu zote USA na miaka sita baadaye siku hii ya MAMA/MORSDAG ikawa sikukuu rasmi.
Miaka kadhaa baadaye Uingereza nayo ikawa katika mila hii ambayo baadaye ilikuwa maarufu katika Scandinavia. Kama nilivyosema mwamzoni kuwa kwa mara ya kwanza Sweden ilianza kusherehekea siku hii mwaka 1919 na ikiwa imeanzishwa na Cecilia Bååth-Holmberg. Lakini ilichukua kipindi cha miaka kumi/miongo kuazimishwa kuwa kum/kwasherekea mama/akina mama kitaifa.
Hapa ni baadhi ya nchi na tarehe zisherehekeazo siku hii:-
3/3- Gergia
8/3- Afghanistan, Romania, Ukaraine
9/3- Afrika kusin
21/3- Misri, Iraq, Lebanon, Sudan
15/5 - Paraguay
26/5- Poland
27/5 - Bolivia
12/8 - Thailand
22/12- Indonesia
Chanzo:- KH- aktuellt
JUMAPILI NJEMA NA HONGERA SANA KWA AKINA MAMA WOOOOTE NA TUWE NA SIKU NJEMA

Friday, May 27, 2011

MUDA WA CHAKULA CHA MCHANA AMBACHO NI MAKANDE

Karibu tujumuike , kwani ni muda wa kula sasa .... Msione kidogo na mkaogopa kuja kuna zaidi na si mnajua Makande hata ukila kiduchu yanashibisha sana....
Haya jamni Ijumaa njema basi
Baada ya mlo huu ili kuyeyusha chakula tuburudike na kibao hiki cha Innocent Galinoma.....

Thursday, May 26, 2011

HAWA WAMEANZA WEEKEND LEO! KAAZI KWELIKWELI HAPA!!!

Sijui mpaka mwisho wa juma itakuwaje?Nawatakieni wote mwisho wa juma mwema na nawaombeni muwe waangalifu na ugimbi...na usisahau kuwa usiendeshe kama umeonja ugimbi....KILA LA KHERI KWA WOTE!!!!!!

LEO TUANGALIE BAADHI YA MISEMO AMBAYO IPO KWENYE VAZI LA KANGA!!

Na hapa inakuja baadhi ya misemo ambayo nimeipata kwenye kanga ambazo ninazo:-
1. Yote fanyeni maskini mkumbukeni.
2. Ahsante mama Mungu akupe kheri Daima.
3. Usigeuze sikio kusikiliza ya wenzio.
4. Upendo na Amani ametujalia Mungu.
5. Nakuridhiya kwa kila hali ujuwe nakupenda kweli.
6. Ya mitaani uyajue wewe yako ayajue nani?
7. Furaha yako ni faida kwangu.
8. Nilijua kiroho kitawauma.
9. Ukinienzi ni wako ukinidharau kazi kwako.
10. Tuishi milele tusifanye kelele.
Hivi kwanini kunakluwa na misemo kama hii kwenye kanga? Haiwezi kuwa kanga tu bila maneno/misemo au methali?

Wednesday, May 25, 2011

KUAMINI KUWA WAMEKAMILIKA NI KUJIDANGANYA BURE!

Tunayo mengi ya kujivunia


Ndugu zanguni kile kipengele cha kila Jumatano cha marudio ndio leo KARIBUNI!!
Wiki iliyopita na wiki hii nimekumbuka sana nyumbani, nadhani ni kwa sababu wiki iliyopita tarehe 17 ilikuwa ni tarehe ambao mama yangu alifariki na wiki hii 23/5 imetimia miezi miwili tangu Mdogo wangu alifariki. Kwa kweli nam-miss sana mama yangu pia mdogo wangu.

Nakumbuka ilikuwa kila nikienda likizo, nilikuwa natumia muda mwingi kuwa jikoni na mama yangu nikizungumza naye simulizi za kale za enzi ya utoto wangu.

Ni simulizi ambazo kwa kweli kila nizikumbukapo huwa natamani yale maisha yajirudie kwani kuna mengi ya kufurahisha na ya kuhuzunisha ambayo kwangu mimi nimejifunza mengi kwako.

Lakini lipo jambo moja ambalo nimelikumbuka, ambalo kwa kweli huwa linanifikirisha sana. Jambo lenyewe ni kuhusiana na baadhi ya marafiki zangu kule nyumbani.

Kusema kweli ule ukaribu niliokuwa nao na baadhi ya marafiki zangu umepungua kiasi cha kukatisha tamaa.

Sababu kubwa ni kutokana na kile walichodai kwa nimewatupa kutokana na kutowasaidia kupata wachumba wa Kizungu. Yupo rafiki yangu mmoja mbaye yeye aliwahi kunitamkia wazi kuwa mimi ni mbinafsi kwa kuwa ni mara nyingi ameniomba nimtafutie mchumba wa Kizungu kwa kuwa ninaishi huku ughaibuni lakini nimeshindwa kumtafutia.

Nakumbuka nilimweleza ukweli kuwa siwezi kumsaidia juu ya jambo hilo kwa sababu liko nje ya uwezo wangu, lakini kutokana na labda tuite ufinyu wa kufikiri, nilimpoteza rafiki huyu kwa sababu ya kushindwa kumtafutia mchumba wa kizungu……..yaani kaaaazi kweli kweli.

Hata hivyo nilijiuliza swali moja, kuwa hivi hakuna wanaume huko nyumbani mpaka mtu aamue kutafuta mchumba wa Kizungu? Je ni mapenzi au ni Uzungu unaotafutwa hapo?

Lakini kwa upande mwingine sikumshangaa sana kwa sababu kwa huko nyumbani ipo silka ya baadhi ya watu ambao wanaamini kwamba kuoa au kuolewa na Mzungu ni jambo la kujivunia sana. Huwa nimezoea kauli za baadhi ya watu kule nymbani kila niendapo likizo wakisema, ‘siyo mwenzako yule, kaolewa na Mzungu’ .

Yaani mpaka leo hii bado kuna baadhi ya watu wanaamini kuwa kuoa au kuolewa na mzungu ni jambo la kifahari na la kujivunia. Kinachotafutwa sio mapenzi tena ni huo uzungu..

Kuna baadhi ya watu wamefikia hatua ya kuamini kuwa sisi waafrika ni duni na wenzetu weupe ni bora na waliokamilika.

Lakini nadhani makosa hayo hayakuanza leo, yameanzia mbali sana. Kwani kizazi na kizazi tumekuwa tukiaminishwa kuwa wazungu ni bora zaidi yetu sisi.

Kwa mfano, mtu kufanya mambo yake kwa umakini na anayefuata muda huyo ataitwa ni mzungu, au mtu asiyependa majungu, uzinzi, uasherati na umbeya naye ataitwa kuwa ni mzungu. Nakumbuka wakati nikisoma kule nyumbani, ilikuwa kama kuna mwalimu ambaye ni mwadilifu kwa wanafunzi na anayewajali, utawasikia wanafunzi wakisema, ‘yule mwalimu ni mzungu’

Yaani kipimo cha kufanya mambo kwa uadilifu na kuwajali wengine kimekuwa kikihusishwa na uzungu, mpaka imefikia mahali kila mtu anatamani kuolewa au kuoa mzungu wakiamini kuwa hao wamekamilika.

Hata huko makazini napo watu wanaochapa kazi kwa uadilifu wanafananishwa na wazungu. Wakati mwingine huwa nacheka kwa sababu naamini hao wanaoamini kwamba mtu kuwa mzungu anakuwa amekamilika ni wazi kwamba hawawafahamu watu hao.

Kwamba kuwa mzungu ni kutokuwa na tabia mbaya, kama uvivu, udokozi, kutojali muda, kusengenya, umbeya, wivu, au kijicho, uzinzi, uasherati, ushoga na tabia zote mbaya tunazozijua hapa duniani, nikujidanganya bure.

Nasema kuamini hivyo ni kujidanganya, kwa sababu kwa wale wanaoishi huku ughaibuni au wale wanaofanya kazi na hawa wenzetu huko nyumbani, watakuwa ni mashahidi wangu.

Kama mlikuwa hamjui ni kwamba hawa wenzetu nakubali kuwa wapo waadilifu na wenye tabia nzuri, lakini pia wapo wenye tabia za ajabu kama uvivu, udokozi, kutojali muda, kusengenya, umbeya, wivu, au kijicho, kutojiamini, uzinzi, uasherati, ushoga na tabia zote mbaya tunazozijua hapa duniani.

Ule udhaifu tulio nao pia wenzetu hawa wanao tena wenzetu hawa wamepitiliza. Ila kutokana na kudanganywa na TV na hizo kauli za wazee wetu tumejikuta tukiamini kitu ambacho hakipo.

Mie wakati mwingine huwa nashangaa pale ninapokutana na baaadhi ya Watanzania wenzangu ambao wanaishi au wamewahi kuishi huku ughaibuni wanapozungumza kwa kubana pua kama hawa wenzetu. Wanashindwa kujua kwamba ile ni lafudhi ambayo inatokana na lugha yao. Ni kama pale unapokutana na Mmakonde, Mngoni au Msukuma au Mpare anapoongea Kiswahili kwa lafudhi ya lugha yao.

Mbona wenzetu kwa mfano Wanaijeria au Wakenya wanaongea kwa lafudhi ya lugha zao. Ni rahisi sana kumtambua Mkenya au Mnaijeria kutokana na lafudhi yake pale anapoongea Kiingereza, tofauti na sisi ambapo Tunajitahidi kubana pua mpaka tunajisahau hata pale tunapoongea Kiswahili.
Na ndio maana kuna baadhi ya wanawake huko nyumbani na hata huku ughaibuni wamefikia hatua sasa wanaukataa uafrika na kuanza kujichubua kwa mikorogo ili kuutafuta weupe.

Kuna wakati nilipokuwa huko nyumbani nilishangaa kuwaona baadhi ya wasichana ambao nawajua kabisa rangi zao kuwa ni weusi kama mimi lakini wamekuwa weupe mpaka wanatisha! Tabu yote hiyo ni ya nini?

Tumefikia hatua sasa kila jambo linalofanywa na hawa wezetu tunaiga, na ndio sababu siku hizi tabia kama za ushoga, usagaji na tabia nyingine chafu tunazozishuhudia huku zimetamalaki huko nyumbani.

Sisi kama Watanzania tunazo tabia nzuri ambazo hawa wenzetu wanazitamani sana tofauti na tunavyodhani. Kwa mfano, sisi ni kawaida mtu kuamka na kupita nyumba mbili tatu na kuwajulia majirani zake hali, au kuingia nyumba yoyote na kama akikuta chakula akala bila wasiwasi.

Kwa upande wa Misiba au harusi watu wamekuwa wakichangiana na kusaidiana kwa hali na mali, yaani tumekuwa na ushirikiano wa hali ya juu tofauti na wenzetu hawa.

Kuwa mzungu haimaanishai kuwa mwadilifu wala kuwa na tabia nzuri, bali tabia nzuri inatokana na tabia ya mtu na malezi kwa ujumla wake, hakuna mahusiano yaliyopo kati ya uadilifu, tabia nzuri na uzungu. Nasisitiza kuwa hakuna kitu kama hicho, ni kujidanganya bure.

Inashangaza kuona kwamba, badala ya kujivunia tabia hizi nzuri tulizo nazo ambazo hata hivyo wenzetu wanazitamani, tunatamani za kwao ambazo nyingi ni mbaya na zenye kuumiza.
Tubadilike………………

Tukutane tena Jumatano ijayo...

Tuesday, May 24, 2011

BLOG MPYA KUANZISHWA/TWAPATA MJUKUU!!

Kwanza samahani kwa kutomtangaza mjukuu huyu kwa muda uliotakiwa. Ni kutokana na sababu za kifamilia ndizo zilizonifanya nishindwa kuwapa taarifa mapema kuwa Mwanamke wa shoka mtarajiwa kaibuka. Na si mwingine tena ni binti yake Mama Maisha na Mafanikio. Da´Camilla zaidi unaweza kumtembelea Bahati .....Nimekuwa bibi.....LOL

Monday, May 23, 2011

TUIANZE JUMATATU HII KWA MSEMO/ UJUMBE HUU!!!

Macho yangu yanameremeta, midomo yangu ina tabasamu,

Lakini huzuni ndani yangu hakuna awezaye kuona....

Jumatatu njema!!!!!

Sunday, May 22, 2011

JUMAPILI NJEMA :- ACHA KULIA NDUGU,MAMA,BABA!!!

Mwimbo huu nimeusikiliza mara kadhaa na kila nikiusikiliza unaniliza kinamna hebu sikiliza na wewe na uniambie kama nawe unalizwa:-( na Jehova Niss Tunduma!!!!

JUMAPILI NJEMA KWA WOTE!!!

Friday, May 20, 2011

Changamoto ya ijumaa ya leo!!!

Nimetumiwa ujumbe huu kutoka kwa msomaji wa Maisha na Mafanikio ambaye ni mkazi wa Njombe. Pia naweza nikamwita kama kaka yangu kwa jina anaitwa Salehe Msanda. Sitaki kuwa mchoyo nimeona ni vema nikiweka hapa ili tusaidiane kwa pamoja kwani kwenye wengi ni pazuri. Pia umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Kaka Salehe alianza kama ifuatavyo:-
-------------------------------------------------------------------------------------

Dada Yasinta naomba tusaidiane katika suala hili lifuatalo

Kwanini tulio wengi tu wazito wa kuthubutu katika nyanga fulani za msingi na muhimu kwa ustawi wa mtu mmojammoja, familia na jamii kwa ujumla?. Mfano tu-wagumu wa kuwekeza kwa ajili ya kuweza kupata mahitaji yetu ya msingi katika maisha ya kila siku (chakula, mavazi, malazi na uhakika wa afya zetu) au kubadilika kutoka katika mazoea yanayohatarisha ustawi wa familia na jamii na familia, lakini tu wepesi wa kuthubutu na kutenda mambo yanayohatarisha maisha na ustawi wa mtu na jamii.

Nini kifanyike kuibadili hali hii hasa kwa sisi waTanzania? Maana nionavyo mimi katika hii dunia ya UFAHAMU NA MAARIFA, wakati wenzetu wanaendelea kugundua mambo mapya kila siku sisi tumejikita zaidi katika burudani na starehe.
Kuna umuhimu wa kukumbushana katika kuifuta lugha ongozi ya kipindi au zama hizi za ufahamu na maarifa ambayo ni kuwa na taarifa na maarifa kadiri ya uwezo wetu.
Ijumaa njema!!!!!!!

Thursday, May 19, 2011

WAKATI HUU JOTO LIANZAPO UKIONA SIPATIKANA BASI UJUE NIPO MAENEO HAYA:-)

Anaandaa ili apande maua mengine...
Haya aliapenda mwaka jana na ameshapalilia ....

Hapa pia na sasa yameanza kuchanua chanua.....



Dada huyo hatosheki na maua tu.....


Hapa ni Rabarber au RHUBARB...unaweza kutengezeza kinywaji , pia kutengeneza pei "paj" ila sasa kinachoniuma ni kwamba haya majani ni mazuri mno kwa kutumia/kula ma mchicha vile:-(


Na ukinikosa sehemu hizo zoooote basi nitakuwa hapa kwenye terrace "altan" napumzika huku nikinywa chai yangu. Na pia kusoma chochote ambacho kitanifanya nipumzike angalao kwa dakika chache kuupumzisha "mgongo"....Kwa hiyo maua/bustani ni vitu ambavyo napenda sana ni "HOBBY" zangu......

JAMANI KWELI HUU NI UUNGWANA??

Haya ndiyo maisha ya kawaida ya wakazi wa jijini Dar Es Salaam. Ambapo akina mama wajawazito ni nadra kupishwa kwenye viti vya daladala. Pichani ni jambo la kusikitisha ndani ya daladala moja kuona uonavyo. Jamani huu ni uungwana kweli?.....Picha hii imenikumbusha siku moja nilichukua daladala kutoka Ruhuwiko nikiwa na safari ya kufika Peramiho na mara kwenye daladala akaingi bibi mmoja na hakuna aliyenyanyuka kwenye kiti chake . ...isipokuwa mimi na wasafiri wengine wakaniambia kama daladala ile ni ya kwangu au nimepanda bila kulipa nauli?

Jibu langu lilikuwa kwamba nimejiona mimi mwenyewe ndani ya bibi huyu maana baada ya miaka kadhaa nitakuwa hivi na nitapenda kukua kwenye siti ....sijui kama walinielewa....Je wewe unaelewa ? Na je ungekuwa wewe upo ndani ya daladala na mamamjamzito, mama aliyebeba mtoto mgongoni bibi au babu wanaingia ndani ya daladala je ungempa siti yako?

Wednesday, May 18, 2011

JAMANI HII NI NDOA AU NDOANO?

Haya basi ile siku imefika ni Jumatano kama nilivyotoa Taarifa... kwa hiyo basi leo tuanze na hii mada ambayo nilisha iweka yenye kichwa cha habari kama kisemavyo hapo juu.
-------------------------------------------------------------------------------------


Je? kuna upendo hapa?


Ndugu wasomaji na wanablog wenzangu, leo nina jambo moja ambalo ningependa tulijadili kwa pamoja.
Kuna msomaji mmoja wa blog hii ambaye ningependa kumuita Mlachaombwani (Sio jina lake halisi) amenitumia email akinitaka ushauri kutokana na kile alichoita jinamizi linaloitafuna furaha ktk ndoa yake.

Kusema kweli, hata mie nimejikuta nikishikwa na kizunguzungu maana mambo ya maunyumba haya yanahitaji umakini pale unapotakiwa ushauri.

Kaka Mlachaombwani anasema kuwa ameishi na mkewe kwa takribani muongo mmoja sasa na wamejaaliwa kupata watoto wawili katika ndoa yao hiyo. Maisha yao kwa ujumla ni mazuri kiasi, kwani ni familia iliyojitosheleza kwa kiasi cha mboga. Awali ndoa yao iloanza kwa bashasha zote ilikuwa na amani na utulivu na kila mmoja alimpenda mwenzake.

Lakini mwaka 2003 mkewe huyo alimbadilikia sana na akawa hawapendi kabisa ndugu zake, yaani ndugu wa mume. Hataki kuwaona wazee wa mumewe wala ndugu zake. Pamoja na ushauri toka kwa viongozi wa dini yao mkewe huyo alishasema kuwa ‘hata kama akija MALAIKA kumshauri hataweza kubadili msimamo wake kwa kuwa akishamchukia mtu basi ni mpaka kiyama’! Kibaya zaidi kafikia hatua anamnyima mumewe huyo unyumba au labda niseme chakula cha usiku, na sasa maisha yao ya ndoa yamekuwa kama vile sio wanandoa, yaani hakuna kupeana lile tendo la ndoa kama ilivyokuwa zamani wakati wanaoana.

Anasema hata kama akiamua kumpa tendo ni pale anapoamua yeye (mwanamke) yaani akipenda yeye na hii inaweza kuwa ni baada ya mwezi au baada ya miezi. Nilipomuuliza kama anapopewa, je wanafanya kwa ile hali ya mapenzi kufurahia tendo la ndoa au vipi? Akasema ni mradi kutimiza tu wajibu lakini hakuna raha yoyote ile. Ni kama vile anabakwa ama anabaka vile.

Nikukumbushe msomaji wangu kuwa ndani ya miaka hiyo kuanzia 2003 ilisababisha huyo kaka Machaombwani kuingia katika ‘mahusiano yasiyofaa’ nje ya ndoa ambayo yalisababisha kupatikana watoto wengine wawili. Nadhani ni baada ya kuona hapati haki yake hapo nyumbani.

Hata hivyo amebainisha kuwa tatizo jingine kubwa linaloitafuna ndoa yake ni wivu usiofaa aliokuwa nao mkewe huyo. Anasema mke wake amekuwa akimlinda sana akijaribu kumpeleleza kama ana wanawake wengine nje ya ndoa (nyumba ndogo?) hata baada ya mume kukiri kilichokwisha kutokea. Kwamba pamoja na kumnyima tendo la ndoa lakini bado anamuonea wivu, na kumlinda. Na cha ajabu pia pamoja na mume kusema kuwa kwa muda wa miaka 2 sasa hamjui mwanamke mwingine nje ya ndoa hataki kusikia chochote ikiwa ni pamoja na kumzuia mumewe kutoa matunzo kwa watoto hao waliozaliwa nje ya ndoa kutokana na ‘ujinga’ wa wanandoa hao.

Tatizo lingine ni matusi, yaani anamtukana hadharani mbele ya watoto bila hata ya aibu. Kuhusu malezi ya watoto, watoto wanalelewa kana kwamba wako ktk kambi ya mateso kwani ni matusi (kama vile mbwa wee, kunguni, mjinga, taahira n.k) na mangumi kwa kwenda mbele. Heshima ndani ya nyumba imepungua na hakuna amani kabisa. Kwamba unaweza kuwakuta wanacheka lakini ni vicheko vya kebehi na ukiwaona leo baada ya saa moja ukiwakuta utadhani ni maadui wa siku nyingi.

Kaka Mlachaombwani anadai kuwa amani yake yeye ni pale anapokuwa kazini, safarini au kwa marafiki zake tu, lakini nyumbani kila siku moto unawaka. Amekiri kuwa sasa wakati wake mwingi anaupotezea katika kompyuta kwa kuwa hapo ndio hupata farijiko huku akijifunza mambo mengi kadha wa kadha ili kupoteza mawazo.

Nimemuuliza kwa nini asimuache huyo mwanamke na kumfukuza kama hali yenyewe ndiyo hiyo naye amenijibu kuwa yupo kwa SABABU ya WANAWE na si vinginevyo. Anasema kuwa muda ukifika ataondoka yeye tu na kumwachia kila kitu huyo mkewe! Yaani pamoja na mahusiano haya mabaya bado yupo tu? Na atakaa kwa muda gani akiyavumilia hayo? Kuna haja ya kuondoka? Kuna haja ya kuoa mke mwingine? Afanye nini?

Wenzangu kwangu mimi huu ni mtihani maana hata sijui nimshauri nini kaka Mlachaombwani.

Swali langu kwa ndugu zangu wasomaji:- Je ndoa ni kupendana kati ya wanandoa au ni tendo la ndoa? Je ni kipi kinachowaunganisha wanandoa, ni upendo au ni tendo la ndoa?
Je kweli kuna upendo kati ya wanandoa hawa na ni namna gani tunaweza kuwasaidia wanandoa hawa?

Na ukibonyeza KAPULYA utakuta maelezo ya kaka Mlachaombwani. TUKUTANE TENA JUMATANO IJAYO....!!!

Monday, May 16, 2011

OMBENI NANYI MTAPEWA!!!!!

Fataki kampa lifti dada mmoja aliyekuwa akitoka kanisani. Kwa kuwa dada kabeba biblia Fataki akajua dada huyo ameokoka. Ndani ya gari Fataki kila akibadili gear anashika mapaja ya dada. Dada akamwambia kasome Mathayo 7.7. Fataki akajua amelaaniwa na hata alipomfikisha dada anapokwenda hakuomba namba yake ya simu. Fataki kufika nyumbani akasoma andiko kwenye biblia akapiga kelele, Duh! Nimekosa kijinga, maana andiko linasema OMBENI NANYI MTAPEWA!!

Ebu tuangalie na hapa....

Sunday, May 15, 2011

TAFAKARI YA JUMAPILI YA LEO!!

Wakati mwingine tunaweza kuyaona maisha hayana maana/hakuna haja ya kuishi. Lakini hakuna Mungu ambaye kila wakati yupo kwa kubadili hali hiyo. Tusipoteze imani/tumaini yetu/letu kwa Mungu. Kwani mwisho atakuja kubadili hiyo hali. Hata kama mti uliukata kuna tumaini/imani siku moja utaota tena. TUKUTANE TENA JUMAPILI IJAYO ......MPAKA HAPO MWENYEZI MUNGU AWE NANYI NA ATAWALE NYUMBANI WENU/MWAKO DAIMA.....!!!!!

Muda si muda nikapita hapa na kukuta habari hii nikavutiwa nayo hebu nawe fungua hapa ufaidi. Tujifunze Kusini . Ahsante sana kwa hili.

Saturday, May 14, 2011

JUMAMOSI NA JIONI NJEMA KWA WOTE KWA WIMBO HUU MPYA WA DADA SAIDA KAROLI!!!

FURAHIA BURUDANI HII...


Dada Saida Karoli amerudi tena uwanjani, na mambo mootoo kweli kweli. Endelea dada Saida Karoli kuiwakilisha Tanzania, Afrika Mashariki na jamii zotw za kiBantu popote tu/walipo!!! JUMAMOSI NJEMA WANDUGU

Thursday, May 12, 2011

TAARIFA:- BLOGU YA MAISHA NA MAFANIKIO NA KIPENGELE KIPYA KILA JUMATANO!!



Blog ya MAISHA NA MAFANIKIO inapenda kuwataarifu kuwa, kuanzia wiki ijayo itakuwa na KIPENGELE kipya ambacho kitakuwa ni kipengele cha MARUDIO YA MADA/MAKALA mbalimbali. Zitakuwa ni mada/makala zangu na pia za bloggers wengine. (kama wamiliki wa blogu nyingine wapo radhi nifanye hivyo) .Kwani katika kuwaza na kuwazua nimeona mtu kama unarudia kusoma/kufanya kitu mara nyingi huwa kinabaki kichwani. Nikiwa na maana ya kwamba unakuwa ndio unaelewa kwa urahisi na kumbukumbu inabaki kwa muda au milele. Pia kuna mada/makala nyingine hazijasoma na wasomaji wote. Kwa hiyo kila JUMATANO KIPENGELE HIKI KITACHUKUA NAFASI YAKE. AHSANTENI!!

Wednesday, May 11, 2011

WANAMITINDO WA WIKI HII NI HAWA HAPA!!

Huwa nafurahi sana nionapo utamaduni wetu wa KIAFRIKA unaendelezwa yaani kuvaa kama vile kanga na vitenge. Na sasa naona KANGA zinakuja juu kwa kushona magauni, mashati, mikoba nk. UTAMADUNI WA KIAFRIKA UDUMU!!!

Ebu angalia hapa, yaani kuangalia tu unaona jinsi UAFRIKA HALISI na mavazi yako unavyopendeza. BINAFSI NIMEPENDA/NINAYAPENDA SANA MAVAZI KAMA HAYA. Je? wewe unapenda mavazi ya aina gani?



Monday, May 9, 2011

TOFAUTI ZETU:MWANA​MKE NA MWANAUME

Wiki iliyopita niliweka mada hii hapa na baadaye nikakumbuka kuwa nina kitabu cha Maisha Na Mafanikio kilichoandikwa na Marehemu Munga Tehenan. Ambacho nilikuwa nimekisoma nikaona nikipitie tena na nikakuta mambo mazuri ambayo nina uhakika wengi tutafaidika, tutajifunza na pia kujitambua. Nikaona ni bara ninukuu kidogo hapa na pale na hapa chini ni nukuu kutoka kitabu hicho haya karibuni sana kusoma.






"Tofauti za kijinsia zinatokana homoni, homoni za kike humfanya binaadamu kuwa mwanamke na zile za kiume humfanya binaadamu kuwa mwanaume.
MTU ANAJULIKANA KUWA MWANAUME AU MWANAMKE KWA KUTAZAMA SIFA FULANI ZA KIMWILI ambazo ni matokea ya kazi za homoni. Tofauti za kihisi pia matokeo ya homoni.
Kuna tofauti za kijinsia ambazo zinatokana na mapokeo ya kijamii, nyingi huonyesha kuwa mwanamke kama kiumbe dhaifu.
Kuna mambo yanayoweza kutusaidia kujifahamu vizuri kati ya jinsia hizi mbili yaani mwanamke na mwanaume
Masuala hayo ya tofauti kati ya mwanamke na mwanaume kwa mtazamo tafauti na kibailojia husaidia kuboresha mahusiano. Tulio wengi hatuzielewi au hata kama tunazielewa lakini huwa hatuzikumbuki na mwishowe hupelekea kuyumba katika uhusiano au kutokea ugiligili(kukatishwa tamaa na kushindwa kufikia matarajio yetu katika uhusiano na kuwa na hasira kwa wenzetu na kudhani kuwa wenzetu wanatakiwa kuwa kama sisi. Huwa tunadhani kuwa wenzetu wanatakiwa watake ambacho sisi tunakitaka na kuhisi ambacho sisi tunahisi.
Huwa tunaamini kuwa kama kweli wenzetu wanatupenda watafanya na kuonyesha mambo fulani kwetu, mambo ambayo sisi tunayafanya au tungeyafanya kuonyesha jinsi tunavyowapenda. Kutokana na kutofaoutiana kwetu hayo huwa hayafikiwi na huwa tunavunjika moyo.
Mara nyingi wanaume ,wanawake kimakosa tunatarajia wenzetu wafikiri, wawasiliane, wajibu na kuhisi kama tunavyofanya sisi.
Kutarajia huko kunatokana na kutofahamu au kusahau kwetu kuwa wanawake na wanaume tukotafauti kimaumbile na kihisia. Kwa kutarajia na kushindwa kuyaona matokeo, uhusiano na ndoa zetu zimejaa misuguano na migongano ambayo siyo ya lazima au haina maana.
Hiyo inathibitishwa na kauli zetu za mara kwa mara mfano wanawake huwa wanasema wanaume hawaeleweki na wanaume kusema wanawake wanajua wenyewe tabia zao wala usishindane nao. Katika hali halisi tunashindwa kuukubali ukweli wa hicho tunasema na kumaanisha. Pamoja na kutoa kauli hizi tunashindwa kufahamu tunatofautiana katika nini au kivipi?
Kama kila mmoja wetu atazifahamu tofauti hizi n i zipi migogoro na migongano katika ndoa na uhusiano vitapungua.
Mara nyingi watu kabla hawajaoana au mara baada ya kuaona migogoro na migongano huwa michache kutokana ukamili wa hisia za wahusika ambao penzi bado mbichi, hili ni suala la kibailojia. Tunapokaa na kitu kwa muda mrefu hujitokeza hali inayoitwa uchovu wa hisia au ukinaifu kwenye mapenzi nako ni hivyohivyo. Kuchoka kwa hisia hutofautiana kati na mtu na mtu wengine huchukua muda mfupi na wengine huchukua muda mrefu. KUTOKANA NA KUCHOKA KWA HISIA hutokea kila mmoja kutarajia mwenzake afikiri na kutenda kama yeye. Ndipo tofauti kati ya mwanamke na mwanaume hujitokeza waziwazi na si hatuzioni isipokuwa tunahisi athari zake. Wengi huwa tunadhani kuwa penzi limekwisha, bali huwa tunashindwa kufahamu kuwa sisi ni tofauti. Kwa kuwa tunatarajia kuona wenzetu wakifanya kama sisi na kuhisi kama sisi na hawafanyi hivyo huvunjika moyo na kudhani kuwa hatupendwi tena , na kwa kutokujua hilo migogoro huanza na kuifanya kuwa mikubwa,kila mmoja humwambia mwenzake hunielewi wakati ukweli kuwa wote hawaelewani kwa kuwa hakuna anayeelewa kuwa yu tofauti na mwenzake.
Tofauti za kimaumbile kati ya mwanamke na mwanaume ziko nyingi lakini kuna zile za msingi ambazo huwa tunakumbana nazo kila siku katika uhusiano wetu na wenzetu. Kwa kuzifahamu chache tunaweza kabisa kuzikabili na linapotokea tatizo tutakuwa tayari na ufunguo wa kufungulia mlango wa kufahamu wengine wakoje na sisi tukoje kimaumbile.

1. Wanaume na kufundishwa.
Wanaume ni wababe na hivyo mara nyingi hujiona kuwa ni mashujaa na wala hawataki kuona wameshindwa na kutokana na hali hiyo huwa hawapendi kuelekezwa hasa na wanawake hata kama hawako katika husiano. Mfano katika suala la kutoa ushauri wa kujenga uhusiano na maisha ya baadae mwanamke anaweza kwa nia njema kumwambia mwanaume fedha unazopata tutumie sehemu yake kuweka akiba ili tununue kiwanja halafu tutafute fedha za kujengea nyumba. MWANAUME BADALA YA KUSHUKURU KWA USHAURI ATAJIBU UNADHANI NI RAHISI KIASI HICHO INGEKUWA NI WEWE UNAYETAFUTA FEDHA HIZI WALA USINGESEMA HIVYO. Nyie wanawake ndiyo matatizo. Na kufuatia na maneno mengine mengi ya ajabuajabu hadi mwanamke akanywea. Mwanamke hataona kosa lake na kudhani kuwa mume wake hampendi au upendo umekwisha, hamsikilizi, wala kumjali ni dikteta na haambiliki. Mwanamke ameshindwa kujua kuwa yeye na mwanamke ni tofauti na kuwa mwanaume hataki kufundishwa kama moto au mwanafunzi. Mwanaume anaposhauliwa bila kuomba husikia katika masikio yake kama anaambiwa kuwa hayuko kamili na hajimudu an hivyo analaumiwa.


2.Wanawake na kusikilizwa.
Wanawake wanaongozwa na hisia(Ushauri) na wala siyo majibu au suluhu.
Kwa mfano huwa inatokea mwanamke akamuuleza mume wake kuhusiana na tatizo linalomkabili la kuwa na shughuli nyingi za nyumbani na jinsi anavyochoka hapo huwa anaomba ushauri na siyo kutaka jibu au suluhisho. Kwa kuwa wanaume wamezoea kutoa majibu au suluhisho anakimbilia kutoa jibu au kutoa ufumbuzi wa tataizo . Mfano atasema kwanini usitafute msaidizi na kupunguza kazi kwa mwanaume kauli hii inatoka kwa dhati na kuamini kuwa anafanya kile mke wake anachotaka, wakati kwa mwanamke inakuwa tofauti na hivyo mwanamke kutokumuelewa mume wake,kwa kuwa mwanamke anataka kusikilizwa na siyo kupewa ufumbuzi. Kwa kumwambia oo pole sana kweli umechoka ikafuatia na kauli ya kutafuta ufumbuzi. Kwa kumwambia pole sana na kumsikiliza hufuatia na kauli kutoka kwa mwanamke we acha tu natamani hata kutafuta msaidizi wa kunisaidia kazi za ndani.
2.Wanaume na sifa
Mwanaume siku zote anauawa na sifa huwa anataka kuona mwanamke amuone kwamba yeye ndiye mwanaume bora kabisa na asiyeshindwa na jambo. Adui yake namba moja ni kukosolewa na wala siyo kwamba mwanamke anapokosolewa anafurahi hapana lakini hapati shida kama mwanaume. Mwanamke anapomkosoa mwanaume huwa anamdunga sindano ya sumu anamuuwa kisaikolojia. Na inaaminika katika ndoa amabyo mwanaume anakosolewa sana mwanaume katika ndoa hiyo huweza kupatwa na tatizo la kukosa nguvu za kushiriki tendo l a ndoa. Mwanaume anapokosolewa na mke wake huumia sana. Kuumia huko ambako hutokea katika mawazo ya kawaida na yale ya kina humfanya mwanaume kuona kama amenyanganywa uanaume wake. Maumivu haya huendelea mpaka kitandani.
Kwa mwanamke huwa tofauti kwa kuwa mwanamke amekuwa anakoselewa na kutupiwa lawama tangu enzi za kale kukoselewa kwake hakumpi tabu.
Kwa bahati mbaya wanawake hawalijui hilo na anatarajia mwanaume kuwa kama yeye na anapomkosoa anadhani na kuamini kuwa atambadili mwanaume.

3. Mwanamke na kupendwa/mwanaume kupotea
Mwanamke anajua na kuamini kuwa ni mtu wa kupendwa iwe kwa maumbile au kwa sababu za kimazoea ya mfumo dume.

Wanawake wanataka kujua na kuhakikishiwa kuwa wakati wote wanapendwa na kuhakikishiwa katika ndoa kuwa hawatakosea au kukosea na kusababisha upendo kuisha. Wanaweza kuhakikishiwa kwa kauli au kwa vitendo.

Wanaume hawajui jambo hili na huwa hawajali sana kauli zao na vitendo vyao. Na huwa hawajali kuwa karibu na wake zao..
Kauli za kutojali za wanaume kwa wake zao kama mwanamke anaweza kumtamkia mume wake nakupenda mwanaume akajibu najua.
Kwa upande wa pili wa wanaume huwa wanatamani wakati fulani kukaa peke yao hasa pale wanapokua na mambo mengi kichwani hujikuta tu wakitamani kuwa peke yao kwa muda fulani. Hali hii imepewa jina la kuingia pangoni au kisimani. Soma kitabu cha mtaalamu maarufu wa uhusiano Mmarekani John Gray katika kitabu chake maarufu cha Men are From Mars, Women are From Venus.
Inapotokea hali ya mwanaume kuwa pangoni wanawake hudhani kuna jambo wamewafanyia waume zao na kuanza kubabaika na kuamua kuwahoji waume zao n akuwafuatuafuata waume zao. Hali ya mwaume kuwa pangoni huomyeshwa na matendo kama kutaka kukaa pekee yake sebuleni, chumbani, ukumbini.
Kutokana na hali hiyo mwanaume huonekana kama anamkimbia mke wake wakati si kweli.
Tunatakiwa kufahamu kuwa tuna tofauti kati yetu na kukubali ukweli huo kwa kuufanyia kazi ili kupunguza migogoro na migongano kati uhusiano."

Sunday, May 8, 2011

SWALI :- HIVI HIZI SIKU ZA MAMA DUNIANI ZIKO NGAPI?

Mama wa Maisha na Mafanikio (aka Kapulya)



Habari za leo ndugu zanguni!
Namshukuru Mungu nimeamka salama. Ndugu zangu leo nina swali ambali nimeona niwaulize wenzangu kwani nahisi kutoelewa kidogo hapa. Ni hivi nimeamka leo nimefunga blog ya Maisha na Mafanikio na nakutana na vichwa vingi vya habari kuwa leo 8/5 ni siku ya AKINA MAMA DUNIANI. Je? ni duniani au? Maana niliposoma hapa pia hapa nk nimeona ni tofauti. Nikakumbua kama mwezi hivi umepita nilisoma kwa mwanamke wa shoka kuwa ilikuwa siku kama hii huku Uingereza. Halafu sasa nazidi kuupata utata kwani hapa niishipo hii siku itakuwa mwezi huu baada ya wiki kama mbili hivi.


Kusema kweli nahitaji msaada swali langu ni kwamba HIVI HII DUNIA SIO DUNIA MOJA ? NA KWA NINI KUNA SIKU/TAREHE TOFAUTI KAMA HIZI ZA AKINA MAMA NA AKINA BABA ? NIELIMISHENI MWENZENU....Kapulya!!

NAWATAKIENI JUMAPILI NJEMA WOTE!!!!



Mwka juzi nilipokuwa nyumbani kila jumapili nilikuwa nausikia wimbo huu na nikaupenda sana. Nikafanya jitihada kuutafuta na sikuupata na leo nimeupata nimefurahi sana . NAWATAKIENI JUMAPILI NJEMA SANA KWA WIMBO HUU....
JUMAPILI NJEMA WOTE!!!

Friday, May 6, 2011

TAFAKARI YA IJUMAA HII YA LEO!!!

Kila nikijaribu kusoma maandishi haya "Mpumbavu ni Mpumbavu 2 awe amesoma au hajasoma" nahisi kichwa changu kama kimechoka vile na mwisho nimeona afadhali niweke hapa kwani kila wakati palipo na wengi hapaharibiki neno... Halafu baada ya muda nakutana ....




.....na maneno haya tena "Fisi Akiwa Hakimu Mbuzi Hana Haki" nikaona hapa sasa kaaaazi kwelikweli ...Sijui nami niandike kwenye baiskeli yangu...mmmmhh TUTAFAKARI PAMOJA JAMANI....NA PIA NAWATAKIENI IJUMAA NJEMA PI MWISHO WA JUMA MWEMA PANAPO MAJALIWA TUTAKUTANA TENA!!!!

Thursday, May 5, 2011

HIVI HARUSI "NDOA" NI NINI?

Mara nyingi nimekuwa nikijiuliza hivi harusi "ndoa" ni nini? je ni mavazi, mwonekano, usafiri, chakula, vinywaji, muziki, watu, au ni UPENDO WA DHATI WA WATU WAWILI WAPENDANAO? Ebu angalia picha hizi hapa chini na sema unavyofikiri wewe karibuni ndugu zanguni:-

Picha hii ya kwanza mnaona wanaharusi ni harusi rahisi kabisa unadhani unaweza kufahamu yupi ni bibi harusi na yupi ni bwana harusi. picha toka kwa kaka Mjengwa

Na picha ifuatayo ni harusi "ndoa" iliyofanyika Ijumaa iliyopita kati ya Prince William na Kate.

Wednesday, May 4, 2011

HONGERA KWA SIKU YAKO YA KUZALIWA KAKA MANYANYA PHIRI!!!

Hongera sana kwa siku yako ya kuzaliwa na kubwa zaidi HONGERA KWA KUTIMIZA MIAKA 50. Kaka huyu siku ya kwenza kabisa kuingia katika blog hii ya Maisha na Mafanikio ilikuwa mwanzoni wa mwaka huu ilipokuwa siku yangu ya kuzaliwa kwa hiyo nami nimeona sina budi kumpongeza kwa siku yake ya kuzaliwa. HONGERA!!! Ukitaki kumzoma kazi zake unaweza kumtembelea:- goodmanmanyanyaphiri.blogspot.com


Najua wengi mtajiuliza huyu Kapulya alijuaje kama Kaka Manyanya anatimiza miaka leo? Ndiyi! nikwamba baada ya kutoa maoni yake katika mada hii ndo nilipogundua hili na nikaona ni kheri tumpongeze. http://ruhuwiko.blogspot.com/2011/04/yale-tuyaitayo-mabaya-ndiyo-hutufunza.html
Goodman Manyanya Phiri said...
Wewe Yasinta unatoka dunia gani? Mbona kila ukitoa kauli ni uhai mtupu? Ubarikiwe sana, Mwanadada!
Umekuwa malaika kwa wengi kutokana na nguvu za kalamu yako. Hasa kwangu nakuona malaika.
Saa iliopita nami nikiwa natangatanga jijini Pretoria kwa matatizo yangu mepya, nilikuwa nawaza: "kwanini maisha yangu Manyanya mie tangu ujana (16) hadi leo... tarehe 4 mwezi ujao (MAY) ninakuwa 50... ni vita tu na vita tupu?"
Hapo nikakumbuka maneno kuhusiana sana na msemo wako [kujifunza katika shida]...maneno kama haya http://pravstalk.com/pravs-world-gods-cup-of-tea/

["WE ARE LIKE TEABAGS, WHOSE STRENGTH COMES OUT WHEN WE’RE PUT IN HOT WATER. SO, WHEN PROBLEMS UPSET YOU… JUST THINK, YOU MUST BE GOD’S FAVOURITE CUP OF TEA!"]
Yule Mungu amekunywa ujana wote wangu... karibu nimtukane: "..Shenzi TYPE!". Lakini sitayasema hayo Kwake kwakuwa Yeye ni Muumba kwangu na malaika wake kama Yasinta wapo chungu mzima kunikumbusha [yote yanania na mwisho Kwake].
Hivi ndivyo nilivyogundua kuwa kaka Manyanya Phiri anatimiza miaka leo 4/5......
HONGERA SANA KWA KUTIMIZA MIAKA 50 MWENYEZI MUNGU AKUONGEZEE MIAKA 50 TENA NA PIA ZAIDI...!!!!!!

Monday, May 2, 2011

NIFANYE NINI ILI MUME WANGU AWE NA HAMU NAMI?

Mume wangu anasema ananipenda sana, nami nampenda sana. Tuna watoto wawili wa kiume. Nimejaribu kila kitu cha kumfurahisha, kama vile kuvaa vizuri, kuandaa chakula kizuri akipendacho na kinywaji lakini Lakini mwenzangu haonekani kuridhishwa na jitihada zangu.
Baada ya chakula cha usiku huwa tunakaa na kuangalia Luninga huku tukiwa na vinywaji. Lakini cha ajabu nikimsogelea na kutaka niwe karibu naye ananiepuka. Yaani HATAKI hata nimguse ni kama NINANUKA au ninamsumbua vile.
Je, tatizo ni nini hasa, Je nanuka? Najiuliza na jibu sipati….Alimalizia kusema huyu mama huko chozi likimdondoka…......
Naam mara nyingi hivyo ndivyo inavyokuwa kwa sisi wanawake pale tukutanapo, si jambo geni sana kwa sisi wanawake kushirikiana kihisia. Ni jambo la kawaida kabisa kukuta mwanamke akimsimulia shoga yake anayemuamini juu ya madhila yake. Yote hiyo ni katika kutafuta nafuu na kuondokana na msongo wa mawazo.
Mara nyingi simulizi nyingi zinazowakutanisha wanawake ni zile zinazohusiana na mambo ya Ndoa, mahusiano, watoto au mambo ya kifamilia kwa ujumla, mara nyingi tunatamani kupata mahali pa kulinganishia, ili kutaka kujua kama tatizo nililo nalo lina ukubwa kiasi gani.
Ni hivi majuzi nikiwa kazini na mfanyakazi mwenzangu ndipo aliponieleza kile kinachomsibu kwa muda mrefu sasa, inavyoonekana, ni jambo ambalo alikaa nalo muda mrefu akijaribu kupambana nalo kimya kimya huku likiendelea kumtafuna, dada huyu wa Kiswidish.
Ili kujiridhisha na kutaka kujua ukweli halisi nikamuuliza kama amemuuliza mume wake jambo hili akajibu amefanya hivyo na jawabu alilolipata ni kwamba, mume wake huwa anachoka. Yaani kazi zake ni nyingi pia malezi ya watoto yanamchosha. Nikamuuliza kama hawawezi wakati wa wikiendi watoke ili kuwa peke yao? Hapo nikapata jibu ambalo sikutegemea. Alidai kwamba akisema hivyo mume wake anaona kama yeye anaamua nini wafanye.
Huyu mama akaendelea kusema, mimi ni binadamu Yasinta.,,,,,,,,,, Na nahitaji tendo la ndoa na sitaki kutoka nje kwani nampenda sana mume wangu. Nami sikuachia hapo kama mnavyonifahamu na u-Kapulya wangu nikamuuliza kama tatizo hilo lina muda gani au limeanza siku za karibuni?
Mama yule akashusha pumzi, akaniangalia kwa jicho la huzuni, kisha akajibu kuwa inatokea wanafanya tendo la ndoa mara moja kwa mwezi na hapo ni ile ya haraka haraka na halafu baada ya hapo mume wake anampa mgongo na kulala .
Hapo….akasita kidogo …nikamuuliza ulitaka kusema nini? Akaendelea unajua Yasinta mwanamke anahitaji kuandaliwa kwanza, mimi huwa siandaliwi kabisa........ Mweh! Nikaona makubwa haya ......nilikosa Jawabu la kumpa kwa kweli, nikabaki kuguna tu.
Hata hivyo nilijaribu kumshauri aende kwa washauri nasaha wa masuala ya Ndoa na mahusiano, lakini akadai kuwa mumewe ni mkaidi na hawezi kukubali.
Mwenzenu swala hili limenishinda maana sijui nimsaidieje! Je Wewe kama msomaji unaweza kunisaidia ni ushauri gani nimpe mama huyu, ili awe na furaha katika Maisha ya ndoa yake?
Ushauri tafadhali...........