Sunday, June 29, 2008

JUNI 29,2008 THAMANI YA MSICHANA (KUTOKA KITABU UTIMILIFU WA MSICHANA)

Siku hizi kuna wataalamu wa aina na mambo mbalimbali. Hao wameendelea sana katika ufundi wa ujuzi wa mambo mengi. Tunafurahi kwani maendeleo hayo ni kwa ajili ya saida na manufaa makuu ya binadamu. Tulipewa akili ili tukautawale ulimwengu na kuufanya kuwa mahali bora pa kuishi binadamu. Kwa sababu ya utaalamu huo mwingi, mambo mengi hupimwa kwa darubibini na mbinu mbalimbali, mbinu tofauti na zile tulizozizoea katika maisha yetu ya kla siku; hasa kadiri walivyoishi wazee wetu. Mabadiliko yatokanayo na mbinu na darubini hizo mara nyingi hutufanya kujisahau na kutojua tutokako wala tuendako.

Leo hii, wataalamu hao wamefikia kiwango cha kusema kuwa mwili wa binadamu unatengenezwa tu na mchanganyiko wa madini mbalimbali. Kama vile chumvi chumvi pamoja na chembe chembe za hewa-Carboni, Oxigeni na kadhalika. Hayo yote, wanadai wataalamu hao. yanaweza kununuliwa na kuuzwa dukani. Thamani ya mwili mzima wa binadamu kwa kufuatana na vipi mo hivyo inakisiwa kuwa karibu shilingi ishirini tu. Hakika, mbinu zimetofautiana. Wengi wanashtushwa na msemo huo wa wataalamu kwani wanafahamu, japo hawana utaalamu wa kisayansi, kuwa mwili wa binadamu na zaidi ya madini na michanganyiko ya mambo hayo ya kiulimwengu. Sasa basi, wewe dadangu, hebu jipime na ufikirie juu ya thamani yako ya kweli. Tafiti kwa unyofu wako wote juu ya umaana, ubora na thamani ya kweli ya usichana wako. Ugunduzi huo mdogo utakaoufanya, nakuhakikishia, utakuwa huo mdogo utakaoufanya, nakuhakikishia, utakuwa wa mafaa makubwa kwako kuliko ugunduzi wa wataalamu wengi ambao wameingia kwenye mkondo wa kushusha hadhi ya utu wako. Pale unapojisikia ukiwa, unapojiona kuachwa, hata na marafikizako na unapokuwa na wasiwasi moyoni; jizatiti na kwa unyofu ujichunguze, utapata faraja ya kweli na kufanya ugunduzi mkubwa kwa maisha yako. Hata unapojiona si kitu mbele ya wenzuo bado una nafasi na thamani ya pekee. Mimi najaribu kukunyoshaea msitari tu wa kufikia ugunduzi huo. Hata hivyo, ni wewe tu unaweza kuukamilisha, hakuna mwingine.

Mungu Baba yako anafurahi anapokuona ukitafiti juu ya umaana na thamani yako ya kweli. Ufanyapo hayo kwa nia ya kujitambua kweli, na kujikuza kimwili na kiroho, yeye mwenyewe atakuwa tayari kukusaidia ili ufikie lengo lako. Yeyote ajisaidiaye husaidiwa. Hasa kwa vile kwa kufanya hivyo unajofunua kwake na kuangalia ni nini nafasi yako ya pekee kama msichana, nafasi ambayo hakuna mwingine awezaye kukupatia bali yeye mwenyewe.

Unapojisikia mwenyewe fungua macho yako ya ndani, jikusanye kimawazo, legeza maungo yako ili usitawanye nguvu zako ovyo na uwe na nia ya kweli ya kufahamu ukweli wa maisha juu yako mwenyewe. kwanini hasa U MSICHANA!

Wewe U msichana mwenye uhai, mzuri na mpendeka. maisha hatuna budi kuyazatiti, si kwa sababu yatuletea vituko au hata furaha, lakini hasa kwa sababu mara tu tuzaliwapo tunakuwa tumewekwa kwenye msafara ambako tutapambana tutake tusitake na milima na mabondo- yaani magumu ya maisha. Kisha kuzaliwa kwako, utakuwepo mpaka milele, hutaisha tena. hata unapokufa kama walivyodai wengine, huo hautakuwa mwisho wa safari au kuwepo kwako. Baada ya kifo cho utakuwepo kwake Yeye akupendaye kiutimilifu, yaani Baba yako wa mbinguni ndiyi aliyekuumba.

Hata hivyo, dadangu mpendwa usiogope. hutakuwa peke yako katika msafara huo. Wazazi, jamaa, marafiki na wasichana wenzio na hata yule atakaye kuwa mteule wa moyo wako atakuwepo katika msafara huo pamoja nawe. Hutasikia ukiwa ikiwa ulitumia busara wakati wa safari yako. Juu ya hao wote, yeye aliyekupa uhai yupo akikutazama na kukuchekelea kama mama mzazi anavyofurahia apapokiona kitoto chake kinajaribu kutembea kwa mara ya kwanza. Kitoto kinapokuwa hatarini mara mama yu tayari hata kama kufanya hivyo kungelikuwa hatari kwake. yeye Baba huyo wa mbinguni ndiye, kiu cha maisha yako, japo hutakuwa umekitambua dhahiri.

Hiki kitabu kimenielemisha na nakipenda sana.

Na; Yasinta Ngonyani

JUNI 29,2008 Upendo

Leo nimekumbuka sana nilipokuwa msichana mdogo au nisema miaka 18-20 kama hivi nilipatwa na mtihani mkubwa sana kama wasichana wote, yaani kumchagua nani atakuwa mume wangu katika maisha yangu. Eeeh ndugu zanguni ilikuwa kasheshe sana maana kila kijana aliyekuja wazazi wangu walisema hafaii. Basi mwisho nilimpata huyu mume wangu aliyenioa, ila cha kusikitisha ni kwamba hakuna mtu aliyenisaport kwa hiyo nilikuwa peke yangu. Yaani hapa nataka kusema shida kubwa ilikuwa ni kwamba kati ya hawa vijana walionichumbia watatu walikuwa ni familia moja kwa hiyo ilikuwa shida sana kuamua ni nani atakuwa mchumba wangu kwani wote walinipenda na walikuwa vijana wazuri. Kwa hiyo kwa hasira na uchungu niliamua kukubali kuolewa na huyu mume wangu sio kwamba sikumpenda hapana nilimpenda na yeye alinipenda na bado tunapendana. Lakini kuna kipindi bado nawakumbuka wale vijana watatu je kuna msomaji anaweza kuniambia kwa nini bado nawakumbuka. kwani katika hii ndoa nina watoto wawili na pia tunapendana sana. Naomba maoni yenu ndugu zangu.



Na ;Yasinta Ngonyani

JUNI 29,2008 KUOA NA KUOLEWA

Dakika, saa, siku, wiki, miezi pia miaka imepita bado sijapata jibu kwa nini baadhi ya dini kwa mfano waislam wanaoa wake wengi. Au pia kwa nini watu wanaoa wake wawili? Kwa nini wanawake wasiolewe na wanaume wengi au wanaume wawili. Kuna tofauti gani naomba wasomaji mnisaidie kufafanua kwani kichwa kinaniuma sana. Inaonekana kama sisi wanawake hatuna thamani au?




Na; Yasinta Ngonyani

JUNI 29,2008 VIATU (SANDOS)


Nimekumbuka nilipokuwa mdogo nimevaa kweli hivi viatu(makubasi) ila mwaka jana niliona watu wengi wanavaa imekuwa kama ni mtindo kwa sasa . Ila miaka ile ukionekana umevaa basi watu walisema huyu ni fukara si mnajua tena.

Friday, June 27, 2008

JUNI 27, 2008 CHAKULA


Ugali , maharage na chainizi . huu ulikuwa mlo wangu mwaka jana wakati nilipokuwa TZ Ninawashauri watu wote kula chakula hiki ni kitamu sana. Isipokuwa kama umezoea kula samaki na dagaa itakuwa ngumu kidogo.
Na; Yasinta Ngonyani

Tuesday, June 24, 2008

JUNI 24,2008 Taarifa ndogo ya ukweli kuhusu Tanzania

Najua wote mtasema nani asiyejua hiyo taarifa ndogo kuhusu Tanzania sawa lakini mimi nawakumbusha tena.

Jamhuri ya muungano wa Tanzania
Tanzania kwa kifupi TZ
Ukubwa wa eneo la nchi ni 945000 km za mraba
Uwingi wa watu (20069 ilikuwa 37,9 milioni
Mji mkuu ni Dodoma
Lufha zinazotumika mara nyingi ni kiswahili na kiingereza
Utawala ni Jamuhuri
Rais Jakaya Kikwete
Waziri mkuu ni Mizengo Pinda
Shiling moja = 100cent
Kwa kifupi inaandikwa TZS
Namba ya nch ya simu ni 255
Tofauti wa masaa ukilinganisha na sweden ni +2
Siku ya Taifa (kupata Uhuru) 26 april 1964

MAZINGIRA;

Ardhi itumikayo; misitu asilimia (38%) kilimo (10%) malisho ya wanyama (52%)

Mlima; kilimanjaro ambao urefu wake ni 5895

Maziwa makubwa; ziwa viktoria lina upana wa mita 69800, ziwa Tanganyika upana wake ni mita 32900 na ziwa malawi upana wake ni mita 31000

WAKAZI
2006 kulikuwa na watu 40 katika kila eneo km za mraba

Miundo ya miaka 2005) 0-14 (45%), 15-64 (52%) na 65-(3%)
Kima cha kuishi (2005) ni miaka 44, wanaume miaka 43 na wanawake miaka 45
Kati ya watoto wanaozaliwa wanaopona ni 68 kati ya 1000.
Inasemekana mwaka 2050 kutakuwa na watu milioni 71,4.
Tofauti ya watu 2005 -50 ni 96%
Watu na miji tajiri (2005) ni Dar es Salaam (2,7 milioni) Mwanza (436800) Zanzibar (403700)

MAZAO YA CHAKULA NA UCHUMI

Usafirishaji 2005, 1,581 milioni US dolla
Mazao muhimu yanayosafirisha, dhahabu, kahawa na korosho.
Nchi ambazo Tanzania zinazosafirisha bidhaa ni India, Usipania na Uholanzi
Uingizaji (2005), 2391 milioni US dolla
Vitu muhimu vinavyoingia ni mashine, na vyombo vya usafiri pia mafuta
Nchi muhimu zinazoingiza ni Afrika kusini, China na India.

Na; Yasinta Ngonyani

Saturday, June 21, 2008

JUNI 21, 2008 UBAGUZI WA RANGI

Bado sielewi kwa nini binadamu tunabaguana, Kwa nini wazungu wanaona wao ni bara zaidi kuliko watu weusi. Wakati wote tukiumia au kujikata maumivu ni yale yale, pia wote damu inatoka. Wakati mwingine unaweza kufikiri ya kuwa kuna mungu wawili au niseme wao wanafikiri hivyo mungu mzungu na mungu mwafrika. Kwani zamani nilikuwa nasikia tu ya kwamba kuna ubaguzi nilikuwa sielewi, lakini sasa naelewa kwani naona mwenyewe kwa macho yangu. Halafu sasa sio wanwabugua watu weusi tu hapana wote ambao si wazungu kwa mfano waarabu, wahindi, wachina n.k.. Yaani wanaogopa hata kukua jirani wakati mpo kwenye basi anakubali kusimama kuliko kukaa siti moja na mwafrika. Wao wanasema wanaogopa wakikaa siti moja basi wao pia watabadilika na kuwa weusi. Wakati mwingine hata kusalia wanaogopa, yaani kushikana mikono. Nasema tena kwa uchungu mwingi sana inaumiza sana tena sana kuona watu wana roho mbaya kiasi hiki. Kwa hali hiyo mtu kila siku unaishi tu yaani siku ikiisha shukuru mungu. Natamani ile ndoto ya Mrtin Luther King ingekuwa kweli, kwamba siku moja mtoto mzungu na mtoto mwafrika watashikana mikono na watacheza pamoja. Je? wasomaji ni kweli sisi waafrika tupo nyumba sana kwa kila hali(jinsi)? Sababu gani wao wanasema waafrika ni wajinga wanakaa tu wanasubiri kupewa wao ni wajinga HAKUNA MTU ANAWAAMBIA WAAFRIKA WANGU WAJINGA. Kwa kweli naumia sana

Na; Yasinta Ngonyani

Wednesday, June 18, 2008

JUNI 18,2008 mziki wa kale


Hapa jamani mnaona akina mama na akina baba katika mavazi maalum. Hapo zamani haya ndio yalikuwa mavazi ya hapa sweden. Na hapo ndo walikuwa wanapiga huo mziki wa asili kama ville Lizombe, zeze au kama umewahi kumsikia Marehemu ZAWOSE yule mgogo alikuwa akiimba na kupiga malimba nk. hiyo instument inaitwa FIOL.
Na; Yasinta Ngonyani

JUNI 18,2008 MIDSUMMER EVE






















Sasa nadhani mtashangaa na kusema ametuletea nini sasa sawa ngoja niwaambie:- Imekuwa ni mila na desturi hapa Sweden. Yaani wakati huu ni katikati kabisa ya mwaka: Na siku hii hapa watu wanasema hivi uchume maua na uweke chini ya mto kisha ulala na usiku ule utaota nani atakuwa mchumba wako. sasa ngoja nikuambia chakula kinacholiwa siku hii, ni samaki wabichi yaani waiopikwa au kuchomwa. Samaki wabichi ambao wamewekwa kwenye maji na viungo maalum kama mwaka hivi. Bila kusahau viazi mviringo (matosani) vya kushemsha na vyakula vingine vingi. Na halafu siku hii watu wanakunywa sana pombe na hasa pombe kali, na pia nisisahau kunakuwa midsummerdance kama mnavyoona katika picha, wanatengeneza (msalaba) huuu kwa majani na maua kidogo. Maana ya huu msalaba kwa lugha ya hapa unaitwa (STÅNG) nitakuelezeni siku nyingine.Baadaya kupeleleza nimeambiwa sababu kubwa ya kuadhimisha au nisema kukumbuka mila hii ni kuwaomba miungu ili mazao (mavuno ) yapatikane kwa wingi . Lakini cha kushangaza ni kwamba wao(waswidi) hawaamini kuna mungu Je? sasa watapataje mazao mengi kama hawaamini? Wanasema hata kama hawaamini lakini hii siku ni safi kwani wanakula chakula na kingi na kunywa mpaka kulewa. Sijui wasomaji mmeelewa kama hamjaelewa basi nitadadisi na kuwaeleza kwa kirefu zaidi siku nyingine.


Na ; Yasinta Ngonyani

Juni 18, 2008 SHAIRI (KWA NINI?)

Kwa nini vitu kama hivi vinazaliwa,
Yaani ambavyo havihitaji kuishi.

Kwa nini vitu kama hivi vinaota
ambavyo havitakiwi kuvunwa

Kwa nini mimi kila wakati nakuwa nimeshiba
wakati wengine wengi hawana chakula

Kwa nini zinatengenezwa silaha nyingi sana
kwa ajili ya kuua?

Kwa nini hatuwezi kufunzana
vipi kupokea shida za wengine

Kwa nini hatuwezi kujifunza kuwa waangalifu
kwa yetu wetu ulimwengu na yetu paradiso

Kuna maswali mengi,
ambayo hayana majibu, duniani hapa na yenye ahadi za uongo


Na; Yasinta Ngonyani

Monday, June 16, 2008

Juni 15,2008 MAHITAJI/CHAKULA/ USAFIRI

Tumwombe mungu ili hali hii isiendelee; Yaani Bei ya chakula imepanda, bei ya mafuta imepanda pia. Usafiri umekuwa ghali eeh jamani mbano tutakufa sasa kwani hatutaweza kwenda hospitali. Na je? tutalalaje bila mafuta ya taa? Na je tutapikaje bila mkaa angalia pia ada za shule kweli tutaweza kusoma? Kama nakumbuka vizuri watu wa zamani walisema ukiishiwa sana usikose chumvi ndani ya nyumba lakini sasa hiyo chumvi itapatikanaje? Je? hizo bajeti haziwezi kurudiwa kupangwa tena kwani watu tunaumia.


Na; Yasinta Ngonyani

Sunday, June 15, 2008

JUNI 15,2008 AKILI NYINGI HUONDOA MAARIFA

Sijui mngekuwa wenzangu mngesema /fanya nini? Ni hivi kuna rafiki yangu mmoja ameniomba msaada/ ushauri ya kuwa katika familia yake hakuna mawasiliano. Kila mmoja anafanya kama anavyotaka. Na hivi leo ninavyosema ameniambia amepatwa na mshtuko kusikia kanisani wanatangaza tangazo la kwanaza la ndoa kati ya baba yake na mwanamke ambaye hajapokelewa katika familia. Labda, sijasema tangia mwanzo huyu rafiki yangu mama yake mzazi alishafariki na sasa baba yake anataka kufunga ndoa na mwanamke mwingine baada ya miaka mitatu tu na huyu mwanamke hajakubalika na watoto wa huyu baba. Je? ungekuwa /mngekuwa wewe /ninyi u/mngemshaurije ili nimpe jibu huyu rafiki yangu?


Na; Yasinta Ngonyani

Juni 15, 2008 TANGAZO: Vitabu Vinauzwa

Habari za leo ndugu wasomaji, ndio najua mtasema huyu mtu vipi. Sio kitu hapa ni baadhi ya vitabu yaani vya hadithi;-


1. Upeo wa mapenzi kimetungwa na; Nyehana Justin
2. Maisha ni safari ndefu na; J.D Ukason na B.G. Mbele
3. Hasusa ya shetani na; Manfred Chr. Mahundi
4. Mdundiko wa maisha na; Joachim Gatahwa
5. Anasa hunasa na; Deusi .C. Masunzu
6. Nakulaumu wewe na Frederick Mbabagu Titi
7. Lazima unioe na; H. Kusare Mboya
8. Nambie Nikuambie na; S.A. Mpinga
9. Salome maskini na; Bernard Mapalala
10. Talaka siku ya ndoa na; S. F. Shija
11. Hadith za wangoni cha kwanza mpaka cha nne na: Angela Amandus Haule
12. Nimekugundua! na; Anania Mbawala
13. Tamaa mbaya na; Kayafa H. Mwangoka
14. Penzi Chungu na; C. Abdul Ntandu
15. Kwa nini iwe jumapili na; Marco Malilo Kaluma
16. Kizazi gani hiki na; Patrick M. Kija
17. Wimbi la aibu na; Amina S. Mlele
18. Simba wa Tunduru na; B.Z. Mkirya

Na vingine vingi vingi ambavyo havipi kwenye orodha haya sasa wahi usichelewa kwani nadhani kuna wengi ambao wana hamu sana yakusoma. Kwa hiyo chukua nafasi kabla sijabadili mawazo. Bei ya kitabu kimoja ni euro 9,99. Kazi kwako sasa.


Na ; Yasinta Ngonyani

Saturday, June 14, 2008

Juni14,2008 Gari


Ya nini kupoteza pesa kuwanunulia watoto vifaa vya kuchezea wakati inawezekana kutengeneza. Yaani hapo vitu vinavyohitajika ni dungu baada ya mafuta ya kula kwisha, mwanzi, ndala zilizochoka kwa ajili ya matairi bila kusahau ufundi. Haya basi kimbia gari halingoji mtu.............tena bei nafuu kabisa.
Na; Yasinta Ngonyani

Friday, June 13, 2008

jun i 13 2008 Picha


Juni 13,2008 LIKIZO

Leo ni siku ile ambayo shule zote ulimwenguni zimefungwa. Ila sasa sikiliza, wanafunzi hapa wao wanalikizo ndefu sana wiki kumi. Yaani mpaka mwezi wa nane tarehe 19. Sababu kubwa ni kwamba hakuna kipindi kingine watu wanaweza kufurahia joto, kuonana, kula na kunywa na marafiki. Ooh nilitaka kusahau kitu muhimu sana kuogelea kwani si mnajua tena, baridi yaani kuanzia mwezi wa tisa mpka wa nne(tano) ni baridi tu nadhani nimeandika kuhusu Hali ya hewa kwa hiyo rudi nyuma na usome tena kama umesahau. Yaani hapa watu wanaona jua (joto) miezi mitano(sita) kama hivi. Sasa labda watu wataonekana nje, kwani hatuonani kabisa wakati wa baridi kila mtu ndani tu. Maisha ya Ughaibuni ndugu zanguni mmmmmmh ..........tuache hivyo hivyo kwani waswahili wanasema ukikuta wanyeji wanatembea uchi basi nawe tembea.

Na; Yasinta Ngonyani

Friday, June 6, 2008

Wimbo wa Taifa

Bila kusahau kumshukuru mungu

Mu ngu ibariki Tanzania,
Dumisha Uhuru na Umoja,
Wake kwa waume ume na watoto,
Mungu ibariki,
Tanzania na watu wake,
Ibariki Tanzania,
Ibariki Tanzania,
Tubariki Watoto wa Tanzania.

najua mtasema nimechanganyikiwa kwani kila mtu TZ anaweza kuimba wimbo wa taifa sawa lakini mimi leo nimekumbuka sana Tanzania yengu. Naipenda sana nchi yangu Tanzania.



Na; Yasinta Ngonyani

Nembo ya Taifa


1. Mwenge huwapa tumaini waliokufa moyo, heshima kwa wale wanaonyanyaswa na amani pale palipo na chuki.
2. Bendera ni alama ya Tanzania huru,
3. Silaha,; mkuki, mshale na shoka ni silaha za kilinda na kujenga Taifa.
4. Mlima Kilimanjaro ambao ni mrefu kuliko yote katika Afrika upo Tanzania
5. Mazao ya pamba na kahawa kuonysha utajiri wa kilimo kama uti wa mgongo wa uchumi
6. Pembe huonyesha utajiri wa wanyama wa asili katika Tanzania.
7. Mume na mke huonysha usawa, ushirikiano na umoja wa watu katika kujenga Taifa
8. Na mwisho ni Uhuru na Umoja ndiyo wito maalum wa Taifa.
Na; Yasinta Ngonyani

CCM

hapa ni bendera ya CCM








Na; Yasinta Ngonyani

Juni 6, 2008 Nchi Yetu Tanzania




Jamani nyumbani ni nyumani leo nimekumbuka kweli nyumbani yaani Tanzania. kama mlikuwa mmesahau maana ya rangi basi nawakumbusha:
1. Nyeusi - huonysha watu na Jamhuri ya Tanzania.
2. Kijani - huonyesha mimea na ardhi ya Tanzania
3. Njano - huonysha utajiri wa mali na asili
4. Bluu - huonyesha bahari inayoziunganisha sehemu za Jamhuri ya Muungano
Na; Yasinta Ngonyani














Juni 6, 2008 Afrika inahamaia Ughabuni

Sasa hali ya hewa hapa Sweden kama nyumbani Afrika. Kusema kweli sijui wapi ni nyumbani kwangu nikiwa hapa nasema nakwenda nyumbani na nikiwa TZ (Ruhuwiko) nasema nakwenda nyumbani yaani hapa sweden. Ebu nisiwachoshe na hayo ya kutojua wapi ni nyumbani kwangu. niwasimulie ambacho nataka kuandika, ni kwamba leo nimefurahi sana, kwanza kabisa ni kwamba nimekula samaki najua mtashanga ni nini cha ajabu kula samaki hapana sio hivyo ni samaki wa kutoka ziwa nyasa amesafiri mpaka huku. Pia furaha imeongezeka kwani nimenunua majani ya viazi yaani matembele(kilugha nabwaka) Najua wengu wanaona nimepungukiwa hapana nina zangu timamu kabisa. Ni hivi mwanzoni nilipata sana shida yaani nilikuwa natamani sana vyakula vya nyumbani TZ hasa samaki na ugali. Lakini sasa naweza kununua hadi majani ya viazi, karanga, mihogo, ila bado sijaona njugu au mboga ya mabogo(kilugha likolo la nanyungu) na kisamvu hivi navitamani sana. Kwa hiyi ninaweza kupata karibu kila aina ya chakula. Lakini hata hivyo havinogi kama vya nyumbani(TZ) kwa sababu ni safiri ndefu mno mpaka kufika huku pia kama samaki sio moja kwa moja toka ziwani. ukitaka kujua ukweli nenda hapo lundunysa.blogspot.com atakuambia utamu wa vyakula hivi.

Na; Yasinta Ngonyani

Juni, 6, 2008

Kama ulikukuwa hujui basi leo utajua. Ni kwamba hapa sweden leo ni sikukuu ya Taifa. Watu wengi wanapumzika tu leo na pia bendera zinapepea. Kwa bahati imeangukia siku nzuri yaani hakuna baridi jua linawaka sana kwa hiyo watu ambao wana mapumziko wamejianika kama mihogo tayari kwa kuota jua ili wapate rangi.

Na; Yasinta Ngonyani